…………………………………………………………………………………………………..
UTANGULIZI 1.
Mheshimiwa Spika, naomba
kutoa hoja kwamba kutokana na taarifa zilizowasilishwa leo katika Bunge
lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti,
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria na
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI
zilizochambua Bajeti ya Mfuko wa Bunge na
Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge
lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi
za Serikali kwa Mwaka 2019/2020 na Mwelekeo wa Kazi za Serikali kwa
Mwaka 2020/2021. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na
Taasisi zilizopo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa Mwaka
2020/2021. - Mheshimiwa Spika, wakati tunapojadili Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa Mwaka 2019/2020 na Mwelekeo wa Kazi za Serikali kwa Mwaka 2020/2021 hatunabudi kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuendelea kutujaalia afya na uzima.
1
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2019/2020, Bunge lako Tukufu lilimpoteza aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Newala Vijijini, Mheshimiwa Rashid Ajali Akbar. Vilevile, Taifa letu lilikumbwa na majanga mbalimbali ikiwa ni pamoja na mafuriko na ajali za barabarani ambazo zilisababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.
- Mheshimiwa Spika, sambamba na kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa misiba iliyotokea, tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu awajaalie afya njema waliopata majeraha na azipumzishe roho za marehemu mahali pema peponi. Amina! Vilevile, nawashukuru kwa dhati wale wote waliojitolea kwa hali na mali katika kuwasaidia majeruhi na wahanga wa matukio hayo.
- Mheshimiwa Spika, kama tunavyofahamu, mwaka huu Serikali ya Awamu ya Tano inahitimisha kipindi cha kwanza cha miaka mitano kilichoanza Mwaka 2015. Kwa msingi huo, hotuba yangu itaeleza kwa muhtasari baadhi ya mafanikio makubwa ambayo Serikali imeyapata
2
katika kipindi cha takriban miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
- Mheshimiwa Spika, hotuba hii inaainisha baadhi ya kazi zilizotekelezwa na Serikali kwa kuzingatia mipango na mikakati mbalimbali hususan Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025. Mikakati na Mipango hiyo, inatekelezwa sambamba na mipango mingine ya kikanda na kimataifa kama vile Agenda ya Mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika na Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030.
- Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, tumeshuhudia mafanikio makubwa katika kuimarisha miundombinu, huduma za kiuchumi na kijamii, utawala bora, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi pamoja na kuhamasisha uwekezaji. Ningependa kutumia fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe
3
Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake mahiri wa Serikali ya Awamu ya
Tano katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya
Mwaka 2015 hadi 2020. Nawapongeza pia, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Ali
Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mheshimiwa Seif Ally Idd, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kwa kusimamia vyema utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
ya Chama Cha Mapinduzi.
- Mheshimiwa Spika, kipekee nakushukuru wewe binafsi, Mheshimiwa Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuliongoza vyema Bunge lako Tukufu katika kuisimamia Serikali kuhakikisha kuwa inatekeleza wajibu wake ipasavyo wa kuhudumia wananchi. Vilevile, natoa shukrani zangu za dhati kwa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kazi kubwa ya kupitia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara, Mikoa, Wakala, Idara zinazojitegemea na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kipekee, nawashukuru sana Wajumbe wa
4
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria chini ya uenyekiti wa Mhe. Mohammed Omary Mchengerwa,
Mbunge wa Jimbo la Rufiji; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya
UKIMWI chini ya uenyekiti wa Mhe. Oscar Rwegasira Mukasa, Mbunge wa
Jimbo la Biharamulo Magharibi na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti
chini ya uenyekiti wa Mhe. Mashimba Mashauri Ndaki, Mbunge wa Jimbo la
Maswa Magharibi. Maoni na ushauri wa Kamati hizo umesaidia sana
kuboresha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri
Mkuu na Mfuko wa Bunge kwa Mwaka 2020/2021.
- Mheshimiwa Spika, nawashukuru Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Wakuu wa Idara, Mashirika, Wakala na Taasisi zote za Serikali kwa ushirikiano mlionipatia katika kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha, nawashukuru wafanyakazi wote wa Serikali na Taasisi zake kwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi mkubwa na hivyo, kuwezesha Serikali
5
kutekeleza kazi zake kwa tija na
ufanisi. Vilevile, nawashukuru kwa michango yenu iliyowezesha
kukamilisha Mpango na Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2020/2021.
- Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisa, namshukuru Mhe. Jenista Joakim Mhagama, Mbunge wa Jimbo la Peramiho na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu); Mhe. Angellah Jasmine Kairuki, Mbunge wa Viti Maalum na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji); Mhe. Anthony Peter Mavunde, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira); Mhe. Stella Alex Ikupa, Mbunge wa Viti Maalum na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu Wenye Ulemavu); Makatibu Wakuu Bw. Andrew Wilson Massawe (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bibi Dorothy Aidan Mwaluko (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Bw. Tixon Tuyangine Nzunda (Waziri Mkuu na Bunge), Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi Binafsi ya Waziri Mkuu na Wafanyakazi wote kwa ushirikiano mkubwa
6
wanaonipatia katika kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
- Mheshimiwa Spika, napenda pia kuwashukuru washirika wa maendeleo zikiwemo nchi rafiki, taasisi na mashirika ya kimataifa, madhehebu ya dini na mashirika yasiyo ya kiserikali, kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kujenga uchumi wa viwanda na kuiletea nchi yetu maendeleo. Mchango wao umekuwa muhimu kuwezesha nchi yetu kupiga hatua kubwa kimaendeleo kulingana na mipango tuliyojiwekea.
- Mheshimiwa Spika, ninawashukuru wananchi wote kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano katika kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Aidha, nawashukuru wananchi wa Jimbo la Ruangwa kwa kuendelea kushirikiana nami na kwa kuniunga mkono. Niwapongeze na kuwashukuru kwa kutekeleza shughuli za maendeleo jimboni kwa ufanisi. Kipekee, namshukuru sana mke wangu mpendwa, Mary; watoto wangu na familia yangu kwa ujumla kwa upendo wao, uvumilivu na maombi yao
7
wakati wote ninapotekeleza majukumu yangu ya kitaifa. Nawashukuru sana.
Homa Kali ya Mapafu 13. Mheshimiwa Spika, hivi
sasa nchi yetu na dunia kwa ujumla inapitia katika kipindi kigumu.
Itakumbukwa kwamba, tarehe 11 Machi 2020, Shirika la Afya Duniani (WHO)
lilitangaza mlipuko wa Homa Kali ya Mapafu ijulikanayo kama COVID-19 inayosababishwa
na virusi vya CORONA kuwa ni janga la Kimataifa. Aidha, tarehe 16
Machi, 2020 Serikali ilitangaza kuwepo kwa mgonjwa wa kwanza nchini.
- Mheshimiwa Spika, tangu kugundulika kwa ugonjwa huo, Serikali inachukua hatua stahiki katika kukabiliana na ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kuimarisha ukaguzi na ufuatiliaji wa wasafiri wanaoingia nchini ili kubaini wasafiri wanaoonesha dalili za ugonjwa au wenye viashiria hatari. Kadhalika, katika kukabiliana na virusi vya CORONA, Serikali ilitoa maelekezo yafuatayo;
Moja: Kusitisha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili ya jukumu hilo zitumike kusaidia hatua
8
za kukabiliana na janga la virusi vya Corona;
Mbili: Kusitisha michezo yote
inayokusanya makundi ya watu ikiwemo ligi kuu ya Tanzania Bara, ligi
daraja la kwanza, ligi daraja la pili na aina nyingine za michezo;
Tatu: Kusitisha shughuli zote za elimu kuanzia elimu ya awali, msingi, Sekondari, vyuo vya kati hadi vyuo vikuu;
Nne: Kusitisha Semina, Warsha, Makongamano na Mikutano yote ya ndani na ya hadhara yenye kuhusisha mjumuiko wa watu wengi; na
Tano: Kuwaasa Watanzania wenye
safari zisizo za lazima kwenye nchi zenye maambukizi ya virusi vya
Corona, kusitisha safari hizo.
- Mheshimiwa Spika, niendelee kusisitiza kuwa sote tuzingatie maelekezo yaliyotolewa na Serikali toka tulipoanza kampeni ya kupambana na ugonjwa huu. Aidha, niwatake Watanzania
9
kuzingatia masharti ya afya kwa
kufuata ushauri unaotolewa na Serikali. Mgonjwa akithibitika, kutangazwa
ni lazima bila kujali cheo chake, awe Waziri, Katibu Mkuu au Mkurugenzi
atalala palipoandaliwa. Watanzania wenzangu tuendelee kupuuza taarifa
za uzushi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii.
MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO
Mheshimiwa Spika, tarehe
20 Novemba 2015 wakati akifungua rasmi Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliwaahidi wananchi
wote kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itawatumikia na kuwajali.
- Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza azma hiyo, ndani ya kipindi cha takriban miaka mitano mafanikio makubwa yamepatikana na yamesaidia kuimarisha hali ya kiuchumi na kijamii kwenye Taifa letu. Ujenzi wa miundombinu muhimu ya kiuchumi hususan ya usafiri na usafirishaji sambamba na uimarishaji wa huduma muhimu za kijamii ni miongoni mwa
1 0
masuala yaliyopewa kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Tano.
- Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge Railway), ufufuaji wa Shirika la Ndege la Tanzania, ufufuaji wa mali za ushirika mfano, UCU SHIRECU na Mamlaka ya Mkonge Tanzania, ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere, ulinzi wa maliasili na rasilimali zetu pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Elimu, Afya na Maji ni kati ya hatua za msingi zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo Mwaka 2025.
- Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki cha miaka mitano, tumeshuhudia miradi hiyo muhimu ikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Kwa mfano, ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa ambao hadi Machi 2020 umetumia Shilingi trilioni 2.96 na kukamilika kwa asilimia 75 kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na asilimia 28 kwa kipande cha Morogoro hadi Makutupora.
1 1
- Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huu umewezesha utoaji wa zabuni zenye thamani ya Shilingi bilioni 664.7 kwa wazabuni na wakandarasi wa ndani 640. Aidha, ajira zipatazo 13,177 za kitaalam na zisizo za kitalaam zimezalishwa. Kati ya hizo, ajira za kitaalam kwa wazawa ni asilimia 46.5 ikilinganishwa na asilimia 53.5 ya wageni.
- Mheshimiwa Spika, Serikali inatumia gharama kubwa katika kujenga miundombinu hiyo wezeshi ya kiuchumi kwa lengo la kulifanya Taifa letu kuwa na uchumi imara wa kujitegemea na wenye kuhimili ushindani. Fedha hizo pia zimekuwa chanzo cha ajira na zabuni kwa Watanzania zinazowasaidia kuongeza kipato.
- Mheshimiwa Spika, mradi huu utakapokamilika utaongeza ufanisi wa huduma za usafiri na usafirishaji wa bidhaa na abiria pamoja na kupunguza gharama za uchukuzi. Kadhalika, utachochea ukuaji wa miji na sekta nyingine kama vile kilimo, viwanda, utalii na biashara. Vilevile, mradi huu utakuwa chanzo cha
1 2
ongezeko la mapato ya Serikali
yatakayosaidia katika kuboresha maslahi ya watumishi na huduma za
kijamii kama vile afya, elimu na maji.
- Mheshimiwa Spika, vilevile, ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere ambalo litakapokamilika litazalisha umeme wa Megawati 2,115. Hadi Machi 2020 mradi huo umegharimu Shilingi trilioni 1.28 na umekamilika kwa asilimia 10.74. Kukamilika kwa bwawa hilo kutalihakikishia Taifa letu umeme wa uhakika na wa nafuu zaidi. Aidha, ongezeko hilo la uzalishaji wa umeme litawezesha shughuli za uzalishaji viwandani kuwa za uhakika, tija, ufanisi na gharama nafuu. Vilevile, mradi huu utachangia kwa kiasi kikubwa katika juhudi za kuhifadhi mazingira kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya nishati ya umeme kwa watu wengi.
- Mheshimiwa Spika, Serikali imefanikiwa kutekeleza Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA) ambapo vijiji vilivyounganishiwa umeme nchini vimeongezeka kutoka vijiji 2,118 Mwaka 2015 hadi vijiji 9,001 mwezi Machi
1 3
- Mradi huo pia umezinufaisha Taasisi 11,128 zikiwemo za elimu, afya, dini, mashine za kusukuma maji na huduma za biashara.
- Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha huduma za usafiri wa anga, Serikali inaendelea kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania. Hadi kufikia Machi, 2020 tayari ndege 8 mpya zenye thamani ya Shilingi trilioni 1.27 zimepokelewa na kuanza kazi. Kadhalika, malipo ya awali ya Shilingi bilioni 85.7 kwa ajili ya ununuzi wa ndege nyingine 3 mpya yamefanyika. Ununuzi wa ndege hizi, umeongeza ufanisi katika usafiri wa anga, kuongezeka kwa mapato ya Serikali, kuimarika kwa utalii na kuongezeka kwa fursa za ajira katika sekta ya huduma.
- Mheshimiwa Spika, bajeti ya dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 31 kwa Mwaka 2015 hadi Shilingi bilioni 269 kwa Mwaka 2019. Serikali pia imegharamia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya afya kwa kujenga zahanati 1,198, vituo vya afya 487, hospitali za Halmashauri za Wilaya 69 na hospitali za rufaa za Mikoa
1 4
10 za Njombe, Simiyu, Mara, Geita,
Songwe, Katavi, Sekou Toure, Burigi, Mwananyamala, Mawenzi na Manyara
na hospitali za rufaa za kanda 3 za Mtwara, Mbeya na Burigi-Chato na
Hospitali maalum ya Kibong’oto. Katika kipindi cha Julai 2015 hadi
Januari 2020 jumla ya Shilingi trilioni 3.01 zimetumika kugharamia
huduma za afya. Kuongezeka kwa bajeti ya dawa na uboreshaji wa
miundombinu ya afya, kumeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya kwa
kuimarisha afya za Watanzania.
- Mheshimiwa Spika, nyote mtakubaliana nami kuwa ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya afya, ununuzi wa dawa na vifaa vya kisasa vya tiba ni utekelezaji wa dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha kila Mtanzania anapatiwa haki yake ya kupata matibabu tena katika eneo alipo.
- Mheshimiwa Spika, katika eneo la elimu, Serikali imeongeza mikopo kwa ajili ya elimu ya juu kutoka Shilingi bilioni 365 Mwaka 2015 hadi Shilingi bilioni 450 Mwaka 2019. Elimumsingi bila Ada nayo imetekelezwa kwa mafanikio makubwa na kuhakikisha watoto wote 1 5
wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa na kupatiwa elimu.
- Mheshimiwa Spika, utekelezaji mzuri wa Mpango wa Elimumsingi bila Ada, uliwezesha kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi walioandikishwa darasa la kwanza. Kwa mfano, kabla ya kuanza kwa Mpango huo Mwaka 2015 ni wanafunzi 1,568,378 walioandikishwa. Aidha, baada ya kuanza utekelezaji wa Mpango Elimumsingi Bila Ada wanafunzi 2,120,667 waliandikishwa Mwaka 2016. Katika kipindi cha mwaka 2015 hadi Februari 2020 jumla ya Shilingi trilioni 1.2 zimetumika kugharamia Elimumsingi Bila Ada.
- Mheshimiwa Spika, maboresho yanayofanyika kwa upande wa elimumsingi yanazingatia uhitaji wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia. Kuanzia Mwaka 2015 hadi Februari, 2020 vyumba vya madarasa 166,627, maabara 5,801, nyumba za walimu 57,541, matundu ya vyoo 231,612 yamejengwa na madawati 2,886,459 yamenunuliwa. Aidha, idadi ya shule za msingi zenye madarasa ya
1 6
elimu ya awali imeongezeka kutoka
madarasa 16,889 Mwaka 2015 hadi kufikia madarasa 17,771 Mwaka 2020.
Kadhalika, idadi ya shule za sekondari imeongezeka kutoka shule 4,708
Mwaka 2015 hadi shule 5,330 Mwaka 2020.
- Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mpango wa Elimumsingi Bila Ada unawahakikishia watoto wote wa kitanzania hususan wale wa hali ya chini kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu. Aidha, Mpango huo umewapunguzia wazazi mzigo wa ada na michango isiyokuwa ya lazima na hivyo kujielekeza zaidi katika kutafuta na kuwapatia mahitaji ya msingi vijana wetu kama vile sare za shule na madaftari.
- Mheshimiwa Spika, kama utakavyokumbuka, katika vikao vingi vya Bunge lako Tukufu vilivyotangulia, changamoto ya maji ni suala lililoongoza kuchangiwa Bungeni na Waheshimiwa Wabunge. Katika kipindi cha takribani miaka mitano, Serikali yetu sikivu ya Awamu ya Tano imetekeleza ujenzi na ukarabati wa miradi ya maji 1,423. Kati ya miradi hiyo, 792 imekamilika ikihusisha miradi 710 vijijini na
1 7
miradi 82 mijini. Vilevile,
Serikali ilipokea ombi la Waheshimiwa Wabunge na kuanzisha Mfuko wa
Taifa wa Maji na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira
Vijijini (RUWASA). Lengo la Serikali ni kuhakikisha vyombo hivi vinakuwa
chanzo cha uhakika cha upatikanaji wa fedha za kugharamia miradi ya
maji na kusimamia utoaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira. Juhudi
hizi kwa pamoja zitasaidia kusogeza huduma ya maji kwa kasi zaidi
karibu na wananchi katika maeneo ya mijini na vijijini.
- Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha takriban miaka mitano, Serikali imefanikiwa kulinda na kuendeleza rasilimali na maliasili za Taifa hususan madini na kuhakikisha zinatumika kwa maslahi mapana ya Taifa na watu wake. Mafanikio hayo, yametokana na Serikali kutekeleza kwa ufanisi mkubwa Mkakati wa Utekelezaji wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusu Umiliki wa Utajiri na Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Utajiri na Maliasili za Nchi ya Mwaka 2017.
1 8
- Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mkakati na sheria hiyo umechangia kuongezeka kwa maduhuli ya Serikali yatokanayo na sekta ya madini mwaka hadi mwaka. Maduhuli ya Serikali yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 205.2 Mwaka 2015/2016, hadi Shilingi bilioni 346.6 Mwaka 2018/2019. Aidha, katika Mwaka 2019/2020 Serikali inatarajia kukusanya Shilingi bilioni 471.
- Mheshimiwa Spika, ukusanyaji wa mapato nao umeongezeka kutoka wastani wa Shilingi bilioni 850 kwa mwezi Mwaka 2015 hadi kufikia wastani wa Shilingi trilioni 1.3 Mwaka 2019. Ongezeko hili limechangiwa na hatua za makusudi zilizochukuliwa na Serikali hususan kuimarisha matumizi ya mifumo ya ukusanyaji mapato kwa njia za kielektroniki, kuongeza idadi ya walipa kodi na kuibua vyanzo vipya vya mapato. Aidha, ongezeko hilo limekuwa chachu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo imesaidia kuimarisha utoaji wa huduma pamoja na kusogeza huduma hizo karibu na wananchi.
- Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kuwashukuru wananchi na walipa kodi wote kwa kuendelea kuitikia wito wa Serikali wa kulipa kodi kwani hatua hiyo ni muhimu katika kulifanya Taifa
1 9
letu kujitegemea. Serikali
itaendelea kusimamia matumizi kwa lengo la kuongeza ufanisi na tija kwa
mustakabali wa maendeleo ya Taifa.
- Mheshimiwa Spika, Serikali pia imefanikiwa kudhibiti matumizi ya hovyo ya fedha za Umma kwa kuziba mianya ya ukwepaji kodi sambamba na kuhakikisha kwamba wale wote wanaotakiwa kulipa kodi wanafanya hivyo. Kwa mfano, katika kipindi cha miaka mitano (2015 – 2019), Serikali imeweza kuokoa Shilingi bilioni 19.83 ya mishahara kwa kuwaondoa kwenye mfumo wa malipo watumishi hewa 19,708 na wenye vyeti vya kughushi 15,411. Msingi huu tunaojenga ni muhimu katika kujenga uchumi imara na usio tegemezi.
- Mheshimiwa Spika, katika siku ya Mashujaa iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai 2016, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitangaza na kusisitiza azma ya Serikali kuhamia Dodoma ambapo alisema, nanukuu:
“…….ninazungumza kutoka kwenye
dhamira yangu kabla sijamaliza kipindi changu cha miaka mitano Serikali
yote itakuwa hapa Dodoma…..”
2 0
- Mheshimiwa Spika, ninapenda kuliarifu Bunge lako Tukufu na watanzania kuwa tayari Serikali imehamia Dodoma. Hadi Machi 2020, jumla ya watumishi 15,361 wa Wizara na Taasisi za Serikali wamehamia Makao Makuu ya Serikali Dodoma, ujenzi wa awali wa ofisi za Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba umekamilika, maandalizi ya ujenzi wa majengo ya ofisi za Serikali awamu ya pili na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika mji huo unaendelea. Vilevile, Serikali imekamilisha mapitio ya Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma ambao niliuzindua tarehe 13 Februari 2020 kwa ajili ya kusimamia shughuli za upangaji wa Jiji la Dodoma. Naielekeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kusimamia ipasavyo utekelezaji wa mpango huo ili kuhakikisha Jiji la Dodoma linaendelezwa kwa kuzingatia Mpango huo.
- Mheshimiwa Spika, nyote mtakubaliana nami kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa katika usimamizi madhubuti wa sheria, kanuni na taratibu za uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma. Usimamizi huo, umewezesha viongozi na watendaji wa umma kuwajibika ipasavyo kwa wananchi ambao ndiyo waajiri wao. Sambamba na
2 1
hilo, nidhamu Serikalini
imeongezeka kutokana na Serikali kuwachukulia hatua za kinidhamu
watumishi wazembe, wadanganyifu na wasio waadilifu.
- Mheshimiwa Spika, tunapotaja mafanikio haya tuna kila sababu ya kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani uongozi wake mahiri na wenye uthubutu ndiyo msingi mkuu wa mafanikio yaliyopatikana. Dhana na falsafa aliyojenga ya Hapa Kazi Tu imesaidia kubadili mtazamo wa Watanzania wengi ambapo sasa tunashuhudia uwajibikaji wa kiwango cha juu wa mtu mmoja mmoja, katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na uzalishaji iwe shambani, ofisini, kiwandani, sokoni na kwingineko badala ya tabia ya awali ya baadhi ya wananchi wachache kupoteza muda mwingi katika shughuli zisizokuwa na tija kwa Taifa.
- Mheshimiwa Spika, baada ya kueleza mafanikio hayo, nyote ni mashuhuda kwamba Chama Cha Mapinduzi kiliahidi na kimetekeleza kwa vitendo na ndiyo maana kinaendelea kuwa
2 2
Chama cha mfano na cha kuigwa siyo
tu Nchini, bali hata katika Bara la Afrika. Hata hivyo, mafanikio
mengine yataelezwa kwa kina wakati Mawaziri watakapokuwa wanawasilisha
hotuba za bajeti za Wizara zao. Sasa naomba kutoa taarifa kuhusu
utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2019/2020 na shughuli
zitakazotekelezwa na Serikali katika Mwaka 2020/2021.
MPANGO WA MAENDELEO NA BAJETI YA MWAKA 2020/2021
- Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2020/2021 yamezingatia Sera na Miongozo ikiwa ni pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2020/2021. Mpango huu ni wa mwisho katika mfululizo wa mipango ya kila mwaka wa kutekeleza Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/2017 – 2020/2021) wenye dhima ya Kujenga Uchumi wa Viwanda ili Kuchochea Mageuzi ya Uchumi na Maendeleo ya Watu.
- Mheshimiwa Spika, Mpango wa Maendeleo na Bajeti wa Mwaka 2020/2021 umezingatia yafuatayo: Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka 2025 yenye lengo la kuiwezesha Tanzania kuwa Nchi ya hadhi ya uchumi wa
2 3
kipato cha kati inayoongozwa na
viwanda ifikapo Mwaka 2025; Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa
Miaka Mitano, 2016/2017 – 2020/2021; Sera na Mikakati mbalimbali;
Malengo ya Maendeleo Endelevu na Makubaliano ya Kikanda na Kimataifa
ambayo Serikali imeyaridhia. Aidha, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi ya Mwaka 2015 – 2020 imezingatiwa pamoja na Maelekezo ya
Serikali yaliyoainishwa na Mheshimiwa Rais wakati wa uzinduzi rasmi wa
Bunge la 11 mwezi Novemba 2015. Vilevile, Mpango umezingatia hali halisi
ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2019/2020; changamoto
zilizojitokeza; hali ya uchumi kitaifa, kikanda na kidunia kwa Mwaka
2019 na maoteo ya ukuaji wa uchumi kwa Mwaka 2020.
- Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kueleza kwa kifupi vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2020/2021 ambavyo vimejikita katika masuala makuu manne yafuatayo: Ujenzi wa Msingi wa Uchumi wa Viwanda; Kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu; Uboreshaji wa mazingira wezeshi kwa uendeshaji wa biashara na uwekezaji na Kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo.
2 4
Katika kufikia malengo ya Mpango,
Serikali itaendelea kutoa kipaumbele cha pekee katika kutekeleza miradi
ya kielelezo ya kimkakati ikiwa ni pamoja na: Ujenzi wa Reli ya Kati ya
Kiwango cha Kimataifa; Mradi wa kufua umeme wa Maji wa Julius Nyerere –
MW 2,115; Kuboresha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL); Mradi wa Ujenzi
wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania);
Uanzishwaji wa kanda maalum za Kiuchumi na Kusomesha wataalam wengi
zaidi katika fani za Ujuzi Adimu na Maalum. Hatua hizo, zitasaidia
kufungamanisha ujenzi wa miundombinu wezeshi na sekta nyingine za
kiuchumi ili kuongeza kasi ya maendeleo, ajira na kipato na hatimaye
kuliwezesha Taifa kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.
- Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kutoa rai kwa Wafanyabiashara, Wawekezaji, Wajasiriamali, Wabunge, Viongozi na Watendaji wa Serikali, Taasisi za Dini, Asasi za Kiraia, Washirika wa Maendeleo, na Wananchi wote kwa ujumla, kushirikiana na Serikali bega kwa bega katika kutekeleza Mpango huu ili azma ya kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo Mwaka 2025 iweze kutimia.
2 5
HALI YA UCHUMI
- Mheshimiwa Spika, uchumi wa Taifa umeendelea kuimarika ambapo katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2019, ukuaji halisi wa Pato la Taifa ulifikia asilimia 6.9. Baadhi ya shughuli zilizochangia ukuaji huo kwa viwango vikubwa ni pamoja na ujenzi asilimia 14.8; uchimbaji wa madini na mawe asilimia 12.6; habari na mawasiliano asilimia 11.0; uchukuzi na uhifadhi wa mizigo asilimia 8.8 na huduma za usambazaji maji asilimia 8.5.
- Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Januari 2020, mfumuko wa bei ulikuwa wastani wa asilimia 3.7. Kiwango hiki ni chini ya lengo la Taifa la kipindi cha muda wa kati la asilimia 5.0, na chini ya malengo ya asilimia 7.0 kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na asilimia 8.0 kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hali hii inatokana na utekelezaji madhubuti wa sera za fedha na za bajeti, uhakika wa upatikanaji wa chakula na utulivu wa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu nyingine duniani.
2 6
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaendelea kuimarisha sekta za uzalishaji na utoaji huduma ili kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato Halisi la Taifa. Vilevile, Serikali itaendelea kutekeleza mikakati na sera za uchumi jumla ili kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuwa na mwenendo tulivu wa uchumi. Serikali pia, itaendelea kuimarisha Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato (GePG) kwa kuharakisha ufungaji wa mfumo huo katika wizara na taasisi za Serikali.
HALI YA SIASA
- Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imeendelea kusimamia utekelezaji wa sheria na maadili ya vyama vya siasa ili kuhakikisha demokrasia ya vyama vingi inaimarika pamoja na kudumisha amani, utulivu na mshikamano uliopo katika nchi yetu.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa itaendelea kusimamia utekelezaji na utoaji elimu kuhusu Sheria ya Vyama vya Siasa, Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, pamoja na Sheria ya
2 7
Gharama za Uchaguzi katika
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020. Vilevile, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya
Siasa itaendelea kufuatilia uhai wa Vyama vya Siasa vyenye usajili wa
kudumu kwa lengo la kuwawezesha wananchi kushiriki na kutoa michango yao
ya mawazo na fikra kupitia vyama hivyo ili kuimarisha demokrasia na
maendeleo nchini.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
- Mheshimiwa Spika, Serikali imeratibu na kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 24 Novemba 2019. Uchaguzi huo ulihusisha Mitaa 4,263, Vijiji 12,319 na Vitongoji 64,384. Katika uchaguzi huo, Chama Cha Mapinduzi kilipata ushindi wa kishindo wa asilimia 99.9 kwa nafasi zote zilizogombewa. Matokeo hayo yameendelea kudhihirisha imani kubwa waliyonayo wananchi kwa Chama Cha Mapinduzi. Hivyo, basi natoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na viongozi waliochaguliwa ili kutimiza azma ya kuwaletea maendeleo.
2 8
Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu
- Mheshimiwa Spika, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2020. Pamoja na mambo mengine, maandalizi hayo yanahusisha Zoezi la Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililofanyika nchi nzima. Awamu ya kwanza ilizinduliwa tarehe 18 Julai, 2019 Mkoani Kilimanjaro na kukamilika tarehe 23 Februari, 2020 katika Mkoa wa Dar es Salaam.
- Mheshimiwa Spika, uboreshaji wa daftari hili ulihusisha: Uandikishaji wa Wapiga Kura wapya ambao wametimiza umri wa miaka 18 au watatimiza umri huo ifikapo siku ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020; urekebishaji wa taarifa za Wapiga Kura walioandikishwa katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 pamoja na ufutaji wa taarifa za Wapiga Kura waliopoteza sifa za kuwemo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
- Mheshimiwa Spika, katika zoezi hilo, jumla ya Wapiga Kura 10,285,732 wameandikishwa na kati yao, Wapiga Kura wapya ni 7,043,247, Wapiga Kura walioboreshewa
2 9
taarifa zao ni 3,225,778 na Wapiga
Kura waliofutwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutokana na
kupoteza sifa ni 16,707. Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura kwa Awamu ya Pili linatarajiwa kuanza tarehe 5 Aprili 2020
na kukamilika tarehe 26 Juni 2020. Zoezi hili litaenda sambamba na
uhakiki wa taarifa za wapiga kura katika daftari hilo. Natoa wito kwa
Wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao
katika daftari hilo, ili waweze kutumia haki yao ya Kikatiba ya kuchagua
viongozi wanaowataka.
- Mheshimiwa Spika, niwasihi Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi Mkuu ujao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu za Nchi. Viongozi wa Vyama vya Siasa waoneshe mfano wa kuendesha siasa za kistaarabu zenye lengo la kuwaunganisha watanzania na siyo kuwatenganisha. Hakuna kiongozi aliyewahi kupata sifa nzuri kwa kuwa chanzo cha mifarakano. Hivyo basi, tudumishe utulivu, amani, mshikamano pamoja na ustaarabu wetu wa kitanzania katika kipindi chote cha kampeni na Uchaguzi Mkuu ili kulifanya Taifa letu
3 0
kuendelea kuwa kisiwa cha amani na mfano wa kuigwa barani Afrika na duniani kwa ujumla.
BUNGE
- Mheshimiwa Spika, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea kutimiza wajibu wake wa kikatiba na kikanuni kwa kufanya mikutano mitatu na huu ukiwa ni wa nne kwa mwaka 2019/2020. Ofisi ya Bunge kwa sasa inatekeleza shughuli za Bunge kwa kutumia TEHAMA kupitia mfumo wa Bunge Mtandao (e-Parliament) uliotengenezwa na kusimamiwa na wataalam wa ndani wa Ofisi ya Bunge. Hivi sasa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali zinawasilisha taarifa na nyaraka mbalimbali Bungeni kwa kutumia nakala tete badala ya nakala ngumu. Hatua hii imeweza kupunguza gharama za uendeshaji hivyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha cha takribani Shilingi bilioni 2 kilichokuwa kinatumika kila mwaka katika uandaaji na uhifadhi wa nyaraka mbalimbali zinazoandaliwa kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Bunge.
- Mshimiwa Spika, Ofisi ya Bunge imeweza kuzindua ‘Bunge Mobile Application’ ambayo imewezesha Waheshimiwa Wabunge
3 1
pamoja na wadau mbalimbali kupata kwa urahisi taarifa mbalimbali kama vile orodha ya shughuli za Bunge (Order Paper), Hansard pamoja
na sheria na miswada. Ni matumaini yangu kwamba Bunge lako Tukufu
litaendelea kuisimamia Serikali ili itekeleze majukumu yake ipasavyo.
MAHAKAMA
- Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati na kwa gharama nafuu, Mahakama imeendelea kuimarisha huduma kwa kuweka mifumo na taratibu mbalimbali za kuwafikia wananchi katika maeneo yote nchini ili kupunguza mlundikano wa mashauri. Mojawapo ya utaratibu unaotumika ni kuwatumia Mahakimu wenye Mamlaka ya Ziada (Extended Jurisdiction) kusikiliza mashauri ya Mahakama Kuu ambapo Mahakimu 195 walipewa Mamlaka hiyo ya ziada. Katika kipindi cha Mwaka 2019 mashauri 1,132 yalisikilizwa na kumalizwa kwa utaratibu huo.
- Mheshimiwa Spika, Mahakama imeendelea kuboresha miundombinu katika ngazi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa majengo. Katika kutekeleza hilo,
3 2
ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu
katika Mikoa ya Kigoma na Mara, Mahakama ya Hakimu Mkazi katika Mikoa ya
Simiyu, Manyara, Geita, Njombe, Mahakama za Wilaya 14, pamoja na
Mahakama za Mwanzo za Mlowo, Magoma, Uyole, Mtowisa, Msanzi na Mkunya
umekamilika.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaendelea kulinda, kuheshimu na kuzingatia haki za binadamu na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa sheria na utoaji Haki kwa kutumia TEHAMA. Vilevile, Serikali itaendelea kufanya maboresho katika mfumo wa Haki Jinai ili kuwezesha shughuli za uchunguzi, upelelezi, uendeshaji wa mashauri na usikilizaji wa mashauri kufanyika kwa ufanisi.
UWEKEZAJI
- Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuratibu na kusimamia shughuli za kuhamasisha na kufanikisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuvutia mitaji, teknolojia na ujuzi ambao ni chachu ya maendeleo katika sekta mbalimbali. Serikali imeendelea kuhakikisha mazingira ya uwekezaji na biashara yanakuwa rafiki.
3 3
- Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutumia vyema uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji na kuwepo kwenye eneo la kimkakati la kijiografia kwa kuhudumia nchi zipatazo 6 ambazo hazipo kwenye mwambao wa bahari. Hali hii inaifanya nchi yetu kuwa lango la biashara ya kimataifa hususani katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati pamoja na Kusini mwa Afrika. Aidha, Serikali inaendelea kuboresha mazingiza ya uwekezaji na biashara ikiwemo kufanya tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996 ili kubaini changamoto za kisera, kisheria na kiutendaji zitakazopelekea kuhuisha Sera ya Uwekezaji ya Mwaka 1996 na Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka 1997.
- Mheshimiwa Spika, vilevile, Serikali imeendelea kuratibu utekelezaji wa Mpangokazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (Roadmap) pamoja na Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara (Blueprint) ambapo kupitia Mpango huo Serikali imefuta tozo mbalimbali 54 katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 pamoja na kuondoa mwingiliano wa majukumu kati ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)
3 4
ili kurahisisha shughuli za
uwekezaji na biashara ambapo kwa sasa usimamizi wa chakula na vipodozi
unafanywa na TBS na usimamizi wa dawa na vifaa tiba unafanywa na TMDA.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2019/2020 Serikali pia imeratibu mikutano ya mashauriano kati yake na wawekezaji na wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. Katika kipindi hicho, Mikutano 11 ya mashauriano kati ya Serikali na Wafanyabiashara na Wawekezaji katika ngazi ya Mikoa imefanyika katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Morogoro. Katika mikutano hiyo hoja nyingi na changamoto zilipatiwa ufumbuzi na nyingine kutolewa ufafanuzi ambapo pia wafanyabiashara na wawekezaji walikumbushwa wajibu wao katika uendeshaji biashara na uwekezaji wao.
- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliendesha mikutano kati ya Serikali na wawekezaji kutoka China, Uingereza
3 5
na Marekani waliowekeza hapa
nchini. Mikutano hiyo ilipata mafanikio makubwa na Serikali itaendelea
kukutana na wawekezaji wa nchi nyingine waliopo nchini kwa nia ya
kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili na kupata maoni na
ushauri zaidi.
- Mheshimiwa Spika, katika kuongeza njia za kushughulikia malalamiko ya wawekezaji, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imeandaa mfumo wa kielektroniki wa kupokea malalamiko na kupata mrejesho wa wawekezaji (Online Complaints and Feedback Platform) ambao utaanza kutumika katika Mwaka 2020/2021. Mfumo huo unategemewa kurahisisha utatuzi wa changamoto za wawekezaji na kupokea maoni na ushauri kwa njia ya haraka na kuleta ufanisi katika kuwahudumia.
- Mheshimiwa Spika, kutokana na hatua hizo nilizozitaja na nyinginezo, mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini yameendelea kuimarika. Taarifa ya Benki ya Dunia ya Wepesi wa Kufanya Biashara (Ease of Doing Business Report) ya Mwaka 2020 iliyotolewa Oktoba 2019
3 6
inaonesha kuwa Tanzania imepanda
kwa nafasi tatu (3) kutoka nafasi ya 144 hadi kufikia nafasi ya 141.
Lengo letu ni kufikia nafasi ya tarakimu 2 kufikia Mwaka 2025. Naziagiza
Wizara na Taasisi zote za Serikali zinazohusika katika utekelezaji wa
Mpangokazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (Roadmap) pamoja na Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara (Blueprint) kuongeza
kasi ya utekelezaji wa maboresho ili kuweka mazingira mazuri zaidi na
rafiki ya biashara na uwekezaji na hatimaye kuzidi kuboresha nafasi ya
Tanzania katika Ripoti hiyo.
- Mheshimiwa Spika, kwa upande wa kukuza uwekezaji, Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeendelea kuhamasisha Mikoa yote nchini kuandaa Makongamano ya Uwekezaji sambamba na kuzindua Miongozo ya Uwekezaji ya Mikoa inayobainisha fursa za uwekezaji za Mikoa pamoja na maeneo ya uwekezaji yaliyotengwa ili kuhamasisha na kuvutia uwekezaji zaidi katika Mikoa hiyo. Hadi sasa, Mikoa 14 ya Ruvuma, Songwe, Pwani, Lindi, Kagera, Mtwara, Geita, Kilimanjaro, Simiyu, Manyara, Dodoma, Mwanza, Kigoma na
3 7
Morogoro imezindua miongozo hiyo.
Narejea tena maelekezo ambayo nimekuwa nikiyatoa katika makongamano hayo
ya uwekezaji kwamba Mikoa yote ambayo haijakamilisha kuandaa miongozo
hiyo ifanye hivyo kabla ya Septemba 2020.
- Mheshimiwa Spika, Serikali pia imeendelea kufanya tafiti za kisekta (investment sectoral profiles) ili kubaini hali halisi ya ukuaji, mnyororo wa thamani, fursa zilizopo na changamoto za kisekta kwa lengo la kutoa mapendekezo ya maboresho katika sekta husika. Hadi sasa tafiti hizo zimefanyika katika maeneo ya mbolea na kemikali, mifugo na mazao yake, pamba, uchakataji wa mazao ya kilimo kama vile korosho, michikichi na parachichi, nafaka na mbegu za mafuta. Matokeo ya tafiti hizo yameendelea kutumika katika kunadi fursa mbalimbali za uwekezaji ndani na nje ya nchi na kuishauri Serikali kuhusu mikakati na maboresho yanayohitajika katika kuvutia uwekezaji kwenye sekta husika.
- Mheshimiwa Spika, kama njia mojawapo ya kunadi fursa za uwekezaji zilizopo nchini Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu
3 8
imeratibu na kushiriki katika
makongamano ya uwekezaji yaliyofanyika hapa nchini kama vile Kongamano
la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uganda, Kongamano la
uwekezaji kati ya Tanzania na Afrika Kusini; Kongamano la Pili la
Biashara na Uwekezaji la Afrika Mashariki na Sweden na Makongamano
mengine yaliyofanyika nje ya Nchi kama vile Kongamano la Biashara na
Uwekezaji kati ya Tanzania na Burundi; Kongamano la Nne la Uwekezaji
lijulikanalo kama “Investment for Africa” lililofanyika nchini Misri;
Kongamano la Pili la Uwekezaji la Afrika lililoandaliwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) lililofanyika Afrika Kusini; na Kongamano la
Kwanza la Biashara na Uwekezaji kati ya Pakistani na Afrika
lililofanyika nchini Kenya.
- Mheshimiwa Spika, sambamba na Makongamano hayo, tumeendelea kupokea jumbe za wawekezaji wanaofika nchini kwa ajili ya kutafuta fursa za uwekezaji kutoka Nchi za Iran, China, Czech, Uturuki, Indonesia, Italia, Singapore, Ujerumani, Marekani, Omani, Japani, Ghana, Nigeria, Uganda, Misri, Ufaransa, Malaysia, Namibia, Belarus, Sweden, Uingereza, India na Mauritius.
3 9
- Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje ambapo inahakikisha maeneo ya uwekezaji yanatengwa na kuendelezwa kwa kuwekewa miundombinu ya msingi ya maji, umeme, mawasiliano na barabara. Hadi Februari 2020, jumla ya hekta 854,821.61 zimetengwa kwa ajili ya uwekezaji katika Halmashauri zote nchini. Naendelea kuzihimiza Halmashauri zote nchini kuendelea kutenga maeneo ya uwekezaji na kwa maeneo ambayo tayari yameshatengwa zihakikishe zinaendelea kuweka miundombinu muhimu na ya msingi ili kuvutia zaidi wawekezaji.
- Mheshimiwa Spika, kupitia kitengo cha Huduma za Mahala Pamoja (One Stop Facilitation Centre) kilichopo Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) chenye watendaji kutoka Taasisi 10 za Serikali, katika kipindi cha kati ya Julai 2019 na Februari 2020 jumla ya vibali na leseni mbalimbali zilitolewa kwa wawekezaji wapatao 5,505. Aidha, kupitia Kituo hicho hadi kufikia Februari 2020, jumla ya miradi 146 yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 1,514.57 inayotegemewa kutoa ajira za moja kwa moja zipatazo 26,384 ilisajiliwa
4 0
ambapo miradi 52 sawa na asilimia
36 inamilikiwa na wageni, miradi 50 sawa na asilimia 34 inamilikiwa na
Watanzania na miradi 44 sawa na asilimia 30 inamilikiwa kwa ubia kati ya
wageni na Watanzania. Katika miradi iliyosajiliwa katika Mwaka huu wa
Fedha miradi 95 sawa na asilimia 65 ya miradi yote inahusisha sekta ya
uzalishaji viwandani.
SEKTA ZA UZALISHAJI
Viwanda
- Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa viwanda Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuwezesha sekta hii kukua kwa haraka na kutoa mchango mkubwa zaidi katika Pato la Taifa pamoja na kupunguza umaskini. Katika kutekeleza dhana hii kwa vitendo katika mwaka 2019/2020, Serikali iliimarisha kiwanda cha Ngozi na Bidhaa za Ngozi cha Karanga (Moshi) na kuimarisha Shirika la Nyumbu (Pwani) ili kuongeza uzalishaji ikiwemo wa magari ya zimamoto. Vilevile, ada na tozo 54 zilifutwa ili kuondoa kero na urasimu kwa wafanyabiashara na wawekezaji katika sekta hii.
4 1
- Mheshimiwa Spika, uzalishaji katika baadhi ya viwanda ulianza ikiwa ni pamoja na Pipe Industries Co. Limited (Dar es Salaam), Kiwanda cha Chai cha Kabambe (Njombe), kiwanda cha Yalin Cashewnut Co. Limited (Mtwara), kiwanda cha 21st Century Food and Packaging (Dar es Salaam), kiwanda cha kusaga mahindi (MeTL, Dar es Salaam), kiwanda cha bidhaa za plastiki cha Plasco Pipelines Co. Ltd (Dar es Salaam), kiwanda cha kupakia na kuhifadhi parachichi, Rungwe Avocado na kiwanda cha kuchakata parachichi kwa ajili ya kutengeneza mafuta (KUZA Afrika).
- Mheshimiwa Spika, kutokana na jitihada kubwa zinazoendelea kufanywa na Serikali za kujenga uchumi wa viwanda, jumla ya viwanda vipya zaidi ya 4,000 vimejengwa katika mikoa mbalimbali. Viwanda vilivyojengwa vinazalisha bidhaa za ujenzi; pamoja na viwanda vya kusindika mazao ya kilimo ikiwemo nafaka, matunda, mafuta ya kupikia na bidhaa za ngozi. Ujenzi wa viwanda vipya nchini, katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano, umechangia kupatikana kwa ajira mpya 482,601 nchi nzima.
4 2
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/2021, Serikali itaendelea kuondoa kero zinazokwamisha ufanisi na ukuaji wa sekta ya viwanda. Aidha, Serikali itaimarisha ushindani katika soko kwa kuzingatia sheria na kanuni za ushindani sawa hususan wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kama vile nondo, mabomba ya plastiki, nguo na mavazi, bidhaa za ngozi na marumaru. Lengo ni kuimarisha msingi wa ukuaji wa sekta ya viwanda nchini pamoja na kuvutia sekta binafsi kuwekeza au kushirikiana na Serikali kuwekeza kwenye viwanda.
Kilimo
- Mheshimiwa Spika, sekta ya kilimo ni muhimu katika kuhakikisha usalama wa chakula, kupambana na umaskini, kuongeza ajira pamoja na kuleta maendeleo ya Nchi kwa ujumla. Kwa kulitambua hilo, Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kutoa kipaumbele kikubwa kwenye sekta hiyo kwa lengo la kuwawezesha wakulima kupata pembejeo na zana za kisasa ili kuongeza tija katika kilimo na hivyo kuleta mageuzi ya kiuchumi.
4 3
Hali ya Upatikanaji wa Chakula 80. Mheshimiwa Spika, pamoja
na mambo mengine hususan kuimarika kwa hali ya hewa, mageuzi
yanayofanywa katika sekta ya kilimo, yamechangia kuimarika kwa hali ya
upatikanaji wa chakula nchini na upatikanaji wa malighafi za viwanda,
sambamba na kuongeza tija kwa wakulima. Katika msimu wa kilimo wa Mwaka
2018/2019, uzalishaji wa mazao ya chakula kitaifa ulikuwa tani milioni
16.3 ikilinganishwa na mahitaji halisi ya tani milioni 13.6. Uzalishaji
huo umeihakikishia Nchi utoshelevu wa chakula kwa asilimia 118 kwa msimu
wa kilimo wa Mwaka 2019/2020.
Upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo 81. Mheshimiwa Spika, Serikali
imeendelea kuhamasisha matumizi ya pembejeo na mbinu bora za kilimo na
teknolojia kwa lengo la kukifanya kilimo chetu kuwa cha kisasa zaidi na
chenye tija. Hadi kufikia Februari 2020, upatikanaji wa mbegu bora za
mazao umefikia tani 71,207 ikilinganishwa na tani 57,023 za msimu wa
Mwaka 2018/2019. Kati ya mbegu hizo, tani 66,031 zimezalishwa nchini
ambayo ni sawa na asilimia 93 na tani 5,175 sawa na asilimia 7
zimeingizwa kutoka nje ya nchi.
4 4
- Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa mbolea nchini kwa kutumia Mfumo wa Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja ambao umesaidia kupunguza bei ya mbolea kwa wakulima. Kutokana na mfumo huo, upatikanaji wa mbolea hadi Februari 2020 umefikia tani 516,813 sawa na asilimia 89 ya lengo la tani 586,604. Kwa kuwa mbolea hizo hutumika kulingana na hatua mbalimbali za ukuaji wa mazao, Serikali inaendelea kuhakikisha asilimia 11 iliyobaki inapatikana na kusambazwa kwa wakulima kwa wakati. Aidha, Serikali imeendelea kuratibu upatikanaji wa viuatilifu ambapo hadi Januari 2020, jumla ya tani 8,719 za viuatilifu zimeingizwa nchini ili kudhibiti visumbufu vya mimea na mazao.
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) 83. Mheshimiwa Spika, katika
kipindi cha Julai 2019 hadi Februari 2020, Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB), imetoa mikopo ya Shilingi bilioni 34 kwa miradi ya
kilimo 38 na kufanya jumla ya mikopo iliyotolewa kufikia Shilingi
bilioni 160.6 toka Benki ilipoanza utoaji wa mikopo. Mikopo iliyotolewa
imewanufaisha wakulima wadogo, wa kati na wakubwa wapatao
4 5
milioni 2.1 wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na viwanda vidogo vya uchakataji wa mazao.
- Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho TADB imetoa mikopo ya ziada ya Shilingi bilioni 31.77 kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo. Mikopo hiyo imewanufaisha wakulima wapatao 5,080, biashara ndogo na za kati za kilimo zipatazo 30, Vyama vya Msingi (AMCOS) 20 katika mikoa mbalimbali nchini pamoja na kufanikisha ununuzi wa matrekta 19 katika mikoa hiyo.
Uzalishaji wa Zao la Chikichi 85. Mheshimiwa Spika, Serikali
imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini kwa
kuendeleza zao la chikichi sambamba na mazao mengine yanayozalisha
mafuta. Uendelezaji wa zao la chikichi unahusisha kupanda kwa wingi
miche mipya yenye uzalishaji wenye tija. Serikali kupitia Taasisi ya
Utafiti wa Kilimo nchini (TARI) imeanza uzalishaji wa mbegu bora za
chikichi aina ya TENERA inayotoa mafuta mengi. Lengo ni kuzalisha mbegu
bora na za kutosha zitakazowezesha wakulima kuongeza uzalishaji na hivyo
kujiongezea kipato 4 6
na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.
- Mheshimiwa Spika, hadi tarehe 15 Februari 2020, mbegu 1,525,017 zimezalishwa ambazo zitatosha kupanda eneo la ekari 30,500. Tayari mbegu 1,026,111 zimesambazwa kwa ajili ya kuziotesha ili miche bora iweze kusambazwa kwa wakulima. Usambazaji kwa ajili ya uoteshaji umefanyika katika halmashauri za mkoa wa Kigoma na taasisi nyingine ikiwemo Magereza ya Kwitanga na Ilagala na JKT Bulombora.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaendelea kuimarisha huduma za ugani, kilimo cha umwagiliaji, ushirika na upatikanaji wa pembejeo ikiwa ni pamoja na mbegu bora za mazao. Aidha, itajenga na kukarabati miundombinu ya kuhifadhi mazao ya kilimo na masoko.
Mifugo
- Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuimarisha sekta ya mifugo nchini ili iweze kutoa mchango mkubwa zaidi katika Pato la Taifa na kutoa fursa za ajira. Ili kufikia lengo hili, Serikali
4 7
imehamasisha wafugaji kuendelea
kuimarisha ufugaji wa kisasa, kuchakata bidhaa za mifugo kwa ajili ya
mahitaji ya ndani, ikiwemo lishe bora na kuuza nje pamoja na kuhamasisha
uwekezaji wa sekta binafsi. Aidha, katika Mwaka 2019/2020, Serikali
imekarabati majosho 292, inaendelea na ukarabati wa majosho 207 na
kuendelea na ujenzi wa majosho mapya 84 katika halmashauri mbalimbali
nchini. Hatua hii imewezesha kuongezeka kwa majosho yanayofanya kazi
kutoka 1,486 Mwaka 2018/2019 hadi majosho 1,738 Mwaka 2019/2020. Aidha,
Serikali imenunua lita 12,549 za dawa za kuogesha mifugo.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021 Serikali itaendelea kuhimiza ufugaji wa kisasa pamoja na kuimarisha afya ya mifugo kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za chanjo na tiba kwa kuimarisha vituo vya utengenezaji wa chanjo za mifugo. Aidha, Serikali itaendelea kuhakikisha upatikanaji wa malisho kwa kutambua, kutenga, kumilikisha, kusimamia na kuendeleza maeneo ya malisho. Vilevile, huduma za ugani zitaboreshwa na mafunzo kwa wafugaji na maafisa ugani yatatolewa ili kuwapatia maarifa na teknolojia mbalimbali kwa lengo la kuongeza tija.
4 8
Uvuvi 90. Mheshimiwa Spika, Serikali
imeendelea kuboresha Sekta ndogo ya Uvuvi ili iweze kuchangia
kikamilifu katika Pato la Taifa na ajira kwa ujumla. Hatua
zilizochukuliwa ni pamoja na kuondolewa kwa kodi katika zana na
malighafi za uvuvi, kupambana na uvuvi haramu, kuboreshwa kwa mialo ya
kupokelea samaki na kuwa ya kisasa, kuhamasisha uwekezaji katika ukuzaji
wa viumbe maji pamoja na kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika
viwanda vya kuchakata samaki.
- Mheshimwia Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaimarisha sekta ya uvuvi ili kuongeza mchango wa sekta hiyo katika pato la Taifa na kuwaongezea wavuvi kipato. Hatua zitakazochukuliwa zitahusisha, utekelezaji wa Mkakati wa kujenga na kuboresha miundombinu ya uvuvi, mkakati wa kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania, kuweka mazingira bora katika uvuvi wa bahari kuu kwa kuweka vivutio kwa wawekezaji, kuendelea kupambana na wavuvi haramu na kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi, uhifadhi na uchakataji wa samaki ili kuimarisha mnyororo wa thamani.
4 9
Utalii 92. Mheshimiwa Spika, sekta
ya utalii nchini imeendelea kuimarika ikichagizwa pamoja na mambo
mengine na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika miundombinu ya usafiri na
usafirishaji na utoaji huduma. Katika Mwaka 2019, idadi ya watalii
walioingia nchini ilifikia 1,510,151 ikilinganishwa na 1,505,702 Mwaka
2018. Ongezeko la idadi ya watalii nchini limeongeza mapato ya Serikali
yatokanayo na utalii kutoka Dola za Marekani bilioni 2.4 Mwaka 2018 hadi
Dola za Marekani bilioni 2.6 Mwaka 2019.
- Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine ya kuimarisha shughuli za utalii nchini, Serikali imepandisha hadhi Mapori ya Akiba 6 ambayo ni Burigi (Chato), Ibanda (Kyerwa), Rumanyika (Karagwe), Nyerere, Mto Ugalla na Kigosi kuwa Hifadhi za Taifa. Lengo ni kuimarisha Sekta ya Utalii kwa kuwa na maeneo mengi ya hifadhi na vivutio vya watalii yatakayosaidia kuongeza wigo wa utalii na mapato yatokanayo na sekta hiyo.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaendelea kuvitangaza vituo vya utalii ndani na nje ya nchi hususan kwenye 5 0
masoko ya kimkakati, kuimarisha
hifadhi mpya 6 za Taifa, kukuza wigo wa mazao ya utalii na kuweka
mazingira wezeshi ili sekta binafsi ishiriki kikamilifu katika uwekezaji
kwenye utalii. Kadhalika, maeneo mengine yatakayopewa kipaumbele ni
utalii wa meli, mikutano, fukwe, utamaduni, malikale, ikolojia na
jiolojia.
Madini
- Mheshimiwa Spika, usimamizi mzuri wa mikakati na sheria za ulinzi wa rasilimali na maliasili zetu umekuwa chachu ya kukua na kuimarika kwa sekta ya Madini nchini. Usimamizi huo umeifanya sekta hiyo kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa Pato la Taifa. Mathalan, katika kipindi cha nusu ya kwanza ya Mwaka 2019/2020 mchango wa Sekta ya madini ulikuwa asilimia 13.7. Katika kipindi hicho, sekta ya madini ilishika nafasi ya pili katika kuchangia Pato la Taifa baada ya sekta ya ujenzi iliyochangia asilimia 16.5.
- Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Januari 2020, maduhuli ya Serikali yaliyokusanywa kupitia Sekta ya Madini ni Shilingi bilioni 284.4. Kiwango hicho ni sawa na asilimia 60.4 ya lengo la mwaka la kukusanya Shilingi bilioni 470.89. Mafanikio hayo, ni ishara tosha ya kuendelea kuimarika kwa sekta hii kufuatia usimamizi thabiti unaowekwa na Serikali.
5 1
- Mheshimiwa Spika, Serikali imeanzisha masoko ya madini nchini kwa lengo la kupata takwimu sahihi za mauzo ya madini, kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata soko la uhakika, kupata bei stahiki kwa bidhaa za madini na kuondoa tatizo la utoroshaji na biashara haramu ya madini. Hatua hiyo imewezesha kuongezeka kwa mapato ya Serikali kupitia tozo za mrabaha na ada ya ukaguzi wa mauzo ya madini kwenye masoko.
- Mheshimiwa Spika, hadi Januari 2020, jumla ya masoko ya madini 28 na vituo vidogo vya ununuzi wa madini 28 vimeanzishwa nchini. Kupitia masoko na vituo hivyo, katika kipindi cha Machi 2019 hadi Januari 2020, jumla ya kilogramu 9,237.34 za dhahabu; karati 12,973.14 za madini ya almasi; kilogramu 20,099.17 za madini ya bati na kilogramu 514,683.28 za madini ya vito mbalimbali ziliuzwa na kuipatia Serikali mapato ya Shilingi bilioni 66.57 ambazo zimetokana na mrabaha, ada ya ukaguzi na ushuru wa Halmashauri. 5 2
- Mheshimiwa Spika, masoko ya madini yamekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha upatikanaji wa takwimu sahihi za madini tofauti na ilivyokuwa awali kabla ya kuanzishwa kwake. Masoko hayo, yana ulinzi na usalama wa kutosha na sifa zote za kimataifa zinazohitajika katika kuendesha biashara ya madini. Hivyo, natoa rai kwa wadau wa ndani na nje ya nchi kutumia masoko na vituo hivyo ambavyo vinaendeshwa kwa misingi ya kisheria kwa kuzingatia ushindani na uwazi wa kibiashara.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaendelea kuimarisha uchimbaji mdogo na wa kati wa madini nchini; ukusanyaji wa mapato yatokanayo na madini; kuhamasisha uwekezaji katika Sekta ya Madini; kuimarisha shughuli za ugani na utafiti, uongezaji thamani madini na masoko.
Nishati
- Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa umeme nchini imeendelea kuimarika na kuchangia katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa Taifa kwa ujumla. Uwezo wa mitambo ya kufua
5 3
umeme nchini ni Megawati 1,602.32
ambapo kati ya hizo Megawati 1,565.72 zipo katika Mfumo wa Gridi ya
Taifa na Megawati 36.6 zipo nje ya Mfumo wa Gridi ya Taifa. Aidha, hali
ya maji katika mabwawa ya Mtera, Kidatu, Kihansi, Nyumba ya Mungu na New Pangani Falls imeendelea kuwa nzuri na hivyo kutuhakikishia kuwa na umeme wa uhakika.
- Mheshimiwa Spika, pamoja na kuelezea juu ya mafanikio tuliyoyapata katika utekelezaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere hapo awali, Serikali vilevile inatekeleza Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Rusumo utakaozalisha Megawati 80. Kukamilika kwa miradi hii na mingine itaimarisha upatikanaji wa umeme nafuu na wa uhakika na hivyo kuchangia katika maendeleo ya ukuaji wa viwanda na uchumi.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa na ya kielelezo ya uzalishaji wa umeme hususan Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (MW 2,115), upanuzi wa Mradi
5 4
wa Kinyerezi I (MW 185) pamoja na
kuimarisha mifumo ya usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini. Aidha,
Serikali itaendelea kutekeleza Awamu ya Tatu ya Mradi wa Kupeleka Umeme
Vijijini ili kuhakikisha vijiji vilivyobaki vinapatiwa umeme.
HUDUMA ZA KIUCHUMI
Ardhi
- Mheshimiwa Spika, ardhi ni rasilimali namba moja katika kuifikia ndoto ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda. Kwa msingi huo, Serikali imeendelea kusimamia upimaji wa ardhi, mipango ya matumizi ya ardhi kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa na umilikishaji ardhi kwa wananchi. Sambamba na kuimarisha utoaji huduma kwa njia ya kielektroniki, Serikali inatekeleza mpango wa kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi. Hadi sasa ofisi za ardhi za mikoa 26 zimeanzishwa pamoja na kuendelea kuziimarisha ofisi zote za ardhi za Halmashauri kwa kuwapatia mafunzo wataalam wa sekta ya ardhi na kununua vifaa.5 5
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2019/2020, Serikali imekamilisha awamu ya kwanza ya usimikaji wa Mfumo Unganishi wa Kuhifadhi Kumbukumbu za Ardhi katika Ofisi za Ardhi Kanda ya Dar es Salaam na Halmashauri za Manispaa ya Kinondoni na Ubungo. Lengo ni kuharakisha upimaji na utoaji hatimiliki za ardhi ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kumiliki ardhi kisheria na kutumia hati hizo kupata mikopo katika taasisi za fedha itakayowezesha kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za ujasiriamali.
Mipango ya Matumizi ya Ardhi 106. Mheshimiwa Spika, Serikali
imeendelea kusimamia upangaji na utekelezaji wa mipango ya matumizi ya
ardhi katika ngazi ya Kanda, Wilaya na Vijiji. Lengo la Serikali ni
kuharakisha upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya makazi na shughuli
mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji, biashara na uwekezaji. Katika
kipindi cha Julai 2019 hadi Februari 2020, mipango ya matumizi ya ardhi
ya vijiji 132 imeandaliwa katika Wilaya 27.
5 6
- Mheshimiwa Spika, sambamba na uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Serikali imeendelea kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi katika maeneo mbalimbali. Katika Mwaka 2019/2020 Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ametoa kibali kwa vijiji 920 kati ya vijiji 975 vilivyokuwemo ndani ya hifadhi na mapori ya akiba kuhalalishwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na kijamii. Hatua hiyo itapunguza migogoro iliyokuwa ikiendelea katika maeneo mbalimbali nchini na hivyo kuwawezesha wananchi kutumia muda mwingi katika shughuli za uzalishaji.
Miundombinu ya Usafiri na Usafirishaji
- Mheshimiwa Spika, sekta ya miundombinu hususan ya usafiri na usafirishaji ndio kiunganishi cha sekta za uchumi wa nchi ili kuwezesha shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma katika jamii. Kuimarika kwa sekta hii, ni kichocheo muhimu katika kukua kwa uchumi na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.
- Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa sekta hii Serikali ya Awamu ya Tano ilichukua hatua za makusudi kuanza
5 7
ujenzi mkubwa wa barabara,
madaraja, vivuko, ufufuaji na ujenzi wa reli mpya, uimarishaji wa
usafiri wa majini, na uboreshaji wa usafiri wa anga ili kuchochea ukuaji
wa uchumi kwa kurahisisha huduma za uchukuzi na usafirishaji wa watu na
bidhaa.
Barabara na Madaraja 110. Mheshimiwa Spika, katika
Mwaka 2019/2020, Serikali imepata mafanikio makubwa katika kujenga
mtandao wa barabara za kiwango cha lami nchini. Serikali imeendelea
kuhakikisha mikoa yote inaunganishwa na mtandao wa barabara za lami ili
kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa.
- Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho jumla ya kilomita 399.07 za barabara kuu na barabara za mikoa zilijengwa kwa kiwango cha lami. Aidha, kilomita 56 za barabara kuu zilifanyiwa ukarabati kwa kiwango cha lami na kilomita 84 za barabara za mikoa zilifanyiwa ukarabati kwa kiwango cha changarawe. Hadi kufikia Februari 2020, jumla ya kilomita 6,960 zimefanyiwa matengenezo ya kawaida, kilomita 1,444 zimefanyiwa matengenezo maalum na madaraja 416 yamefanyiwa matengenezo.
5 8
- Mheshimiwa Spika, katika kuondoa msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam, Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya njia 8 kutoka Kimara hadi Kibaha yenye urefu wa Kilomita 19 ambapo ujenzi umefikia asilimia 63. Mradi mwingine ni ujenzi wa Ubungo Interchange ambao umefikia asilimia 65.
- Mheshimiwa Spika, miradi mingine inayotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa Daraja la Tanzanite (Salender) lenye urefu wa Kilomita 6.2 uliofikia asilimia 25 na kuanza maandalizi ya ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 na upana wa mita 28.45. Aidha, kati ya Julai 2019 hadi Januari 2020 Serikali imetoa Shilingi bilioni 703.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya barabara na madaraja nchini.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaendelea na utekelezaji wa miradi mikubwa niliyoitaja pamoja na mingine inayoendelea. Vilevile, Serikali itaanza ujenzi wa barabara na madaraja mapya ili kuwahakikishia wananchi, wawekezaji na wafanyabiashara huduma bora na za uhakika za usafirishaji katika kipindi chote cha mwaka. 5 9
Reli 115. Mheshimiwa Spika, kama
nilivyoeleza hapo awali, moja ya mafanikio makubwa tuliyoyapata katika
eneo la reli ni kuendelea na ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha
Kimataifa. Nikiri pia kuwa, katika kipindi hiki, Serikali inajivunia
kurejesha huduma ya reli kati ya Dar es Salaam na Moshi ambayo ilisimama
kwa zaidi ya miaka 20 na kufufuliwa kwa huduma ya reli kati ya Tanga na
Moshi iliyosimama kwa takribani miaka 12 ambapo hadi Machi 2020 jumla
ya abiria 33,459 na mizigo tani 5,080 imesafirishwa kupitia reli hizo.
Aidha, ukarabati wa reli ya kati kutoka Dar es Salaam hadi Isaka nao
unaendelea kwa kuondoa reli zote nyepesi na kuweka reli mpya nzito.
Ukarabati huo umewezesha kurejea kwa huduma za usafiri wa abiria na
mizigo na hivyo kurahisisha usafirishaji, kupunguza kero ya usafiri na
ajali za barabarani.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itakamilisha ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro na kuendelea na ujenzi wa kipande cha Morogoro – Makutupora
6 0
sambamba na kukarabati miundombinu mingine ya reli.Bandari
- Mheshimiwa Spika, katika eneo la bandari, Serikali imeendelea kuboresha na kuimarisha miundombinu ya bandari zilizopo katika mwambao wa pwani na maziwa kwa lengo la kuendeleza huduma ya usafiri wa majini ndani ya nchi na nchi jirani. Katika Mwaka 2019/2020, Serikali imekamilisha ujenzi wa gati namba 1, 2, 3 na gati la kupakia na kupakua magari (RoRo Berth) katika Bandari ya Dar es Salaam. Kazi ya ukarabati wa gati namba 5 hadi 7 inaendelea.
- Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Bandari ya Mtwara, ujenzi wa Gati lenye urefu wa mita 300 umefikia asilimia 60 wakati ukarabati wa Gati namba 2 na uongezaji wa kina cha Bandari ya Tanga unaendelea na umefikia asilimia 60. Ujenzi na ukarabati wa bandari zetu utaifanya nchi yetu kuendelea kuwa lango muhimu la uagizaji na uingizaji bidhaa kuelekea nchi jirani.
6 1
Ujenzi wa Meli 119. Mheshimiwa Spika, Serikali
inafanyia kazi changamoto ya utoaji wa huduma za usafiri katika Maziwa
Makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa. Kwa upande wa ziwa Nyasa, tayari
ujenzi wa Meli ya MV Mbeya yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200
za mizigo umekamilika. Vilevile, tarehe 8 Desemba 2019, Mheshimiwa Rais
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa
chelezo, meli mpya ya MV Mwanza na ukarabati wa Meli za MV Victoria na
MV Butiama.
- Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Februari 2020, ujenzi wa meli ya MV Mwanza itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo ulikuwa umefikia asilimia 52. Aidha, ujenzi wa chelezo umefikia asilimia 80, ukarabati wa meli za MV Victoria asilimia 75 na MV Butiama asilimia 70. Katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaendelea kuboresha huduma za usafiri kwa njia ya maji ikiwa ni pamoja na kukamilisha miradi inayoendelea, kukarabati vyombo vilivyopo na kununua vyombo vipya.
6 2
Usafiri wa Anga na Viwanja vya Ndege 121. Mheshimiwa Spika, pamoja
na mafanikio niliyoyaeleza hapo awali kuhusu kufufua Shirika la Ndege
Tanzania, katika Mwaka 2019/2020 Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa
anga la Tanzania ni salama ili kuimarisha utoaji wa huduma za usafiri wa
anga. Aidha, Serikali inakamilisha usimikaji wa mfumo wa rada 4 za
kuongozea ndege za kiraia katika viwanja vya ndege vya Julius Nyerere,
Kilimanjaro, Mwanza na Songwe.
- Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuboresha viwanja vya ndege mbalimbali vilivyopo nchini. Hadi kufikia Februari, 2020 Serikali imekamilisha ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Kukamilika kwa jengo hilo kunawezesha kuwahudumia abiria milioni 6 kwa mwaka na hivyo kuongeza mapato. Serikali pia, imekamilisha upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza na inaendelea na ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja huo. Jengo hilo ambalo litagharimu Shilingi bilioni 13.26 litahudumia
6 3
abiria 400,000 kwa mwaka.
Vilevile, Serikali inaendelea na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya
ndege vya Mtwara, Songea, Geita, Nachingwea, Iringa na Musoma.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaendelea kuboresha usafiri wa anga nchini ili kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa kitovu cha usafiri wa anga kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Katika kufanikisha azma hiyo, Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa usalama na miundombinu ya viwanja vya ndege inaboreshwa.
Mawasiliano
- Mheshimiwa Spika, katika eneo la mawasiliano Serikali imeendelea na zoezi la usajili wa laini za simu kwa njia ya biometria Nchi nzima. Hadi mwisho wa mwezi Februari, 2020 jumla ya laini milioni 31.4 kati ya laini milioni 43.9 zilikuwa zimesajiliwa. Idadi hii ni sawa na asilimia 71 ya zoezi zima la usajili. Nitoe wito kwa wananchi waliopata namba za vitambulisho vya Taifa kukamilisha usajili wa laini zao kwa njia ya biometria ili waendelee kupata huduma
6 4
za mawasiliano. Zoezi hili lina
umuhimu kwa Taifa kwani linasaidia kuimarisha usalama wa watumiaji wa
huduma za mawasiliano nchini na Taifa kwa ujumla.
- Mheshimiwa Spika, Serikali pia, imeendelea kusimamia mtambo wa Telecommunications Traffic Monitoring System (TTMS) ili kuhakikisha kuwa tunapata mapato stahiki kutokana na huduma za mawasiliano. Mfumo huu umeongeza ufanisi katika kusimamia huduma ya mawasiliano ya simu nchini. Katika kipindi cha Julai, 2019 hadi Februari, 2020 jumla ya miamala bilioni 2 yenye thamani ya Shilingi trilioni 12.2 imefanyika ambapo Serikali imepata mapato ya Shilingi bilioni 7.3.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaendelea kushirikiana na makampuni ya simu kuboresha huduma za mawasiliano hususan maeneo ya pembezoni ili kuongeza kasi ya mawasiliano ya kimtandao kwa wananchi wa maeneo hayo. Aidha, Serikali itaendelea na ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kufikisha huduma katika Makao
6 5
Makuu ya Wilaya zote nchini pamoja na kuanza ujenzi wa Kituo cha Data Dodoma.
HUDUMA ZA JAMII
Elimu
- Mheshimiwa Spika, elimu ya kisasa na hasa yenye mwelekeo wa sayansi na teknolojia ina nafasi ya pekee katika kufanikisha ujenzi wa msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea. Kwa kutambua umuhimu huo na kama nilivyoeleza awali Serikali ilianzisha na kutekeleza Mpango wa Elimumsingi Bila Ada ili kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anaandikishwa. Naendelea kuwasihi wazazi na walezi wote nchini kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa shule katika umri muafaka kama inavyoelekezwa katika Sera ya Taifa ya Elimu.
- Mheshimiwa Spika, kwa upande wa elimu ya juu, Serikali imeongeza wigo wa upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kutoa kipaumbele kwa watu wenye
6 6
mahitaji maalum. Katika Mwaka
2019/2020, Serikali imeongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya juu kwa
kutoa mikopo kwa wanafunzi 130,883 ikilinganishwa na wanafunzi 122,754
kwa Mwaka 2018/2019. Aidha, Shilingi bilioni 450 zilitumika katika
kipindi hicho ikilinganishwa na Shilingi bilioni 424.8 kwa Mwaka
2018/2019.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Elimumsingi Bila Ada, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kuhimiza uwekezaji kwa kushirikiana na sekta binafsi hususan katika kuboresha miundombinu, vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kuendeleza rasilimali watu ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu.
MajiUpatikanaji wa Maji Vijijini 130. Mheshimiwa Spika, Serikali
kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeendelea kutekeleza Programu
ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa
6 7
huduma ya maji safi na salama kwa
wananchi wote hususan wale wanaoishi maeneo ya vijijini. Katika Mwaka
2019/2020, jumla ya miradi 94 ya maji yenye vituo vya kuchotea maji
2,495 katika maeneo mbalimbali vijijini imekamilika. Aidha, miradi 558
ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
- Mheshimiwa Spika, kutokana na juhudi kubwa za Serikali katika utekelezaji wa miradi hiyo, hadi Desemba 2019, upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo ya vijijini umefikia asilimia 64.8. Vilevile, ili kuboresha utoaji wa huduma ya maji vijijini, Serikali imeanzisha Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wenye jukumu la kutekeleza miradi na kusimamia utoaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira vijijini.
Upatikanaji wa Maji Mijini
- Mheshimiwa Spika, kwa upande wa maji mijini, Serikali imetekeleza miradi mipya ya maji katika Jiji la Dodoma na Dar es Salaam pamoja na maeneo ya Kibaha, Bagamoyo na Kisarawe. Aidha, Serikali pia imeboresha 6 8
miundombinu ya upatikanaji wa
huduma ya maji katika miji mikuu ya mikoa, wilaya, miji midogo na maeneo
yanayohudumiwa na miradi ya maji ya kitaifa ya Chalinze, Mugango –
Kiabakari, Maswa, Wanging’ombe, Masasi – Nachingwea na Kahama –
Shinyanga. Utekelezaji wa miradi hiyo umewezesha upatikanaji wa maji
katika miji ya mikoa kufikia asilimia 85.
- Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2020/2021, Serikali itaifanyia mapitio Sera ya Taifa ya Maji ya Mwaka 2002 ili kuzingatia masuala mapya ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, kutilia mkazo suala la usafi wa mazingira na matumizi ya vyanzo vya maji chini ya ardhi. Serikali pia, itakamilisha miradi inayoendelea, kuanza miradi mipya ya maji na kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka Singida hadi Dodoma.
Afya Ujenzi na Ukarabati wa Hospitali 134. Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na miradi ya ujenzi wa hospitali za Rufaa za
6 9
Mikoa, ikiwemo ujenzi wa hospitali
za Mikoa mipya ya Geita, Simiyu, Songwe, Katavi, Njombe (Mgondechi).
Vilevile, Serikali inaendelea na ujenzi wa hospitali za Mikoa ya Mara,
Singida na Shinyanga pama Halmashauri 69 nchini. Vilevile, Serikali
inajenga Hospitali ya Uhuru wilayani Chamwino, Dodoma na Hospitali za
Rufaa za Kanda za Mtwara Mbeya na Burigi-Chato.
Huduma za Afya za Kibingwa 135. Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuimarisha huduma za kibingwa bobezi (super specialist) katika
Hospitali za Rufaa za Kanda, Hospitali Maalum na Hospitali ya Taifa.
Utoaji wa huduma hizo umewezesha wananchi wengi kupata huduma ambazo
awali zilikuwa zinapatikana nje ya Nchi. Katika kipindi cha Julai hadi
Machi 2020, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya Rufaa ya
Benjamini Mkapa, MOI na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete zimetoa huduma
mbalimbali za kibingwa kwa wagonjwa wa ndani na nje ya Nchi.
- Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2019 hadi Machi 2020, idadi ya wagonjwa waliopata huduma za kibingwa bobezi
7 0
No comments :
Post a Comment