Thursday, April 16, 2020

SIKU TATU ZA KULIOMBEA TAIFA KUANZA LEO IJUMAA


SIKU tatu za kumrudia Mwenyezimungu (kumuomba MUNGU) ili atuepushe na gonjwa hatari la COVID-19 zinaanza leo Ijumaa Aprili 17, 2020 kama ambavyo Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania alivyowaasa Watanzania kupitia ujumbe wake wa Twitter  alioutuma Alhamisi Aprili 16, 2020 kupitia akaunti yake ya @MagufuliJP.
Katika ujumbe huo Rais aliandika Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020 {Ijumaa, Jumamosi na Jumapili} KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia”.Aliandika Rais Magufuli.
Ugonjwa wa COVID-19 ama Virusi vya CORONA ulianzia jimnbo la Wuhan nchini China Desemba mwaka 2019 na kutapakaa dunia nzima ambapo tayari umesababisha maafa makubwa.
Hadi kufikia Alhamisi Aprili 16, 2020, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alisema, tawimu zinaonyesha hadi sasa kuna jumla ya wagonjwa wa CORONA 94 na amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka mara kwa mara, kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

No comments :

Post a Comment