Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg
Milton Milos Lupa akitoa maelezo kuhusu utendaji wa NFRA wakati wa ziara
ya kikazi ya katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akisisitiaz jambo wakati wa
kikao kazi na Watendaji wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).
Mwingine pichani ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi
ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Milos Lupa.

Sehemu
ya watendaji wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA)
wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya
wakati wa kikao kazi kilichofanyika NFRA Makao Makuu Jijini Dodoma.
Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg
Milton Milos Lupa amemuhakikishia katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ya
Kilimo Ndg Jerald Kusaya wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja
NFRA Makao makuu Jijini Dodoma kuwa tayari wataalamu wapo mikoani kwa
ajili ya kazi hiyo.
Lupa
amesema kuwa msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 NFRA itanunua mazao
makuu matatu ambayo ni zao kuu la chakula Mahindi, Mpunga na Mtama.
Amesema
kuwa lengo la serikali kuamua kununua mazao hayo matatu ni kujiimarisha
vyema katika uhifadhi wa chakula ili inapotokea dharula ya chakula
nchini kuwe na hifadhi ya mazao tofauti tofauti.
Akizungumzia
lengo la Wakala kuanza kujipanga ili kununua nafaka mapema, amesema
kuwa lengo la kufanya hivyo ni kupata mazao bora kwa ajili ya kuhifadhi
kadhalika kupata mazao mengi.
No comments :
Post a Comment