Kauli
hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizundua mpango wa elimu ya afya kwa
umma kwa siku 20 ambao utaongozwa na vikundi vya kijamii kwa
kushirikiana na Red Cross chini ya Wizara ya Afya.
Waziri
Ummy amesema lengo la kuzindua mpango huo ni kukata mnyororo wa
maambukizi ya ugonjwa wa Corona Kati ya mtu na mtu kwa kutumia vikundi
vya kijamii ambavyo vitaelimisha na kutoa taarifa sahihi kwa Jamii
kuhusu ugonjwa wa Corona.
“Vikundi hivi vya kijamii, vitashirikiana na Wizara ya Afya na Red Cross na UNICEF kutoa elimu ya afya kwa umma.
Magari
18 yatatumika kwa siku 20 na yatakwenda katika maeneo ya masoko, stendi
za mabasi na maeneo mengine yenye mikusanyiko ya watu,” amesema Waziri
Ummy Mwalimu.
Waziri
amefafanua kuwa Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, vikundi vya kijamii
vitakwenda katika maeneo ya nyumba za ibada kwa ajili ya kuongeza nguvu
ya kutoa elimu ya afya kutokana na kuwapo kwa ongezeko la ugonjwa wa
Covid-19.
“Niwatoe
hofu Watanzania, tutashinda hii vita endapo kila mmoja katika Jamii
atazingatia maelekezo ya Wataalamu wa Afya,” amesema Waziri Ummy
Mwalimu.
Waziri
amesema mbali ya Elimu ya afya kutolewa katika Mkoa wa Dar es Salaam,
pia vikundi vya kijamii vitakwenda katika mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza
na Arusha kwa ajili ya kutoa elimu ya afya kwa umma kuhusu kujikinga na
maambukizi ya ugonjwa Corona.
“Serikali
inawashukuru Watanzania kuhusu suala la kunawa mikono kwa maji tiririka
na sabuni, wameelewa, wamepokea hili vizuri sana, hata katika ngazi ya
Kijiji nje ya nyumba wameweka ndoo ya maji na sabuni, kwa hili
tunawashukuru Sana Watanzania na tunawatia moyo wa kuendelea kunawa
mikono kwa maji tiririka na sabuni,” amesema Waziri.
Waziri
amewasisitiza Watanzania kuepuka mikusanyiko na misongamano ili
kukabiliana na ugonjwa huo Kama walivyofanya kwenye hatua ya kunawa
mikono kwa sabuni na maji tiririka.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi wa Elimua ya Afya kwa Umma wa Wizara ya Afya, Dkt.
Ama Kasangala amesema atahakikisha elimu kwa Jamii inatekelezwa ili
kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini.
“Nitashirikiana
na Red Cross na wenzangu wa kitengo cha elimu ya afya kwa umma ili
kuhakikisha Mipango ya utoaji wa elimu kwa wananchi inatekelezeka,”
amesema Dkt. Kasangala.
No comments :
Post a Comment