……………………………………………………………………………………
NA MWAMVUA MWINYI, Chalinze
SERIKALI Kuu imetoa
kiasi cha sh.milioni 240 ,kwa ajili ya kumalizia maabara nane katika za
sekondari kwenye halmashauri ya Chalinze, wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa
Pwani .
Fedha hizo zitatokana
na bajeti ya mwaka wa 2020/2021, zinalenga kujenga vyumba hivyo katika
shule 9 za sekondari, ambapo kila chumba kimoja kitatumia sh.milioni
30.
Kaimu Ofisa Elimu
Sekondari Halmashauri ya Chalinze, Irene Joseph aliiambia Kamati ya
Siasa ya Halmashauri Kuu ya (CCM) Wilayani Bagamoyo, chini ya Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alhaj Abdul Sharifu,
ilipokwenda kujionea ujenzi unavyoendelea katika
shule mpya ya msingi ya Kwamkomba, Kata ya Mioni kuwa ,lengo
kuwawezesha wanafunzi kujipatia fursa ya kujisomea masomo ya sayansi.
“Katika mwaka wa
fedha wa 2020/2021 tunataraji kupokea kiasi cha sh.milioni 240
zitazomalizia chumba kimoja kimoja, katika majengo ya maabara nane kati
ya tisa kwenye shule zetu za Sekondari zilizopo ndani ya Halmashauri
yetu,” alisema Irene.
Wakichangia mada
katika ujenzi wa shule hiyo shikizi, wajumbe Ally Ally, Alhaj Amir
Mkang’ata na Yahya Msonde walimtaka Ofisa Elimu Msingi vifaa na Takwimu
Pilli Kinunga kuwasiliana na Mkurugenzi Mtendaji, ili wanaohusika na
usajili wafike hatimae waipatie usajili shule hiyo kwani inakidhi
vigezo.
“Hii shule ni ya
Serikali inaonekana inakidhi vigezo, hivyo nikushauri Ofisa Elimu
wasiliana na Mkurugenzi ili wanaohusika na usajili wa shule hii
wakamilishe taratibu hatimae ianze kupokea wanafunzi, angalia mabati
yameshaanza kuchakaa,” alisema Ally.
Mwenyekiti wa (CCM)
Wilaya Sharifu aliwataka wataalamu wanaoandaa taarifa za miradi katika
naeneo yao, wasisahau kuandika nguvu zinazotolewa na wananchi, kwani
kutoiweka kwenye taarifa zao ni kuwavunja nguvu.
Awali Mwalimu Mkuu wa
shule ya Msingi ya Kikalo Mdachi Mnyani, anayesimamia ujenzi huo
alielezea, katika majengo mapya ilitakiwa kuongezwa chumba kimoja cha
darasa, lakini yamejenga vitatu.
No comments :
Post a Comment