Wednesday, April 1, 2020

BODABODA NA BAJAJI RUKSA KUINGIA KATIKATI YA JIJI LA DAR



……………………………………………………………………………….
Na Magreth Mbinga
Madereva wa bodaboda na bajaji wameruhusiwa kuingia katikati ya jiji ili kisaidia kubeba abiria ambao wanamudu kutumia usafiri binafsi kutokana na uhaba wa usafiri uliotokana na
serikali kuagiza abiria wasisimame ndani ya daladala.
Amezungumza hayo leo Mh Paul Makonda katika kituo cha mabasi ya makumbusho wakati akiwataka wananchi wachukue tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa kukaa umbali wa mita mbili kati ya mtu na mtu.
Pia Makonda amewaomba wamiliki wa nyumba,majengo ya ofisi na godauni kupunguza kodi hadi asilimia hamsini ili pesa ambayo itabaki wanunue chakula waweke ndani.
Vilevile amewataka wazazi kutulia nyumbani kama hawana safari za lazima ili kuepusha kusababisha maambukizi ya Corona kuleta nyumbani na kuathiri familia.
“Abiria tuwe walinzi wenyewe ili kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa corona wasijifiche kwaajili ya kuwakwepa askari wakati wanahatarisha maisha yao”amesema Makonda.
Sanjari na hayo Mussa Ndila abiria katika kituo cha mawasiliano amesema agizo la abiria kutokusimama kwenye daladala ni mwarobaini wa kujikinga na ugonjwa huo lakini ameziomba taasisi na mashirika ya umma kuwa na usafiri kwaajili ya kusafirisha wafanyakazi wao.
Hatahivyo Happy Sebastian ambae ni abiria amesema usafiri umekuwa mgumu sana amefika toka asubuhi saa mbili lakini mpaka saa nne hajafanikiwa kupata usafiri.
Mahammedi Said ambae ni kondakta katika kituo hiko amesema ni janga ambalo hawajalitegemea pia abiria wanapata tabu hatakama gari likiwa limejaa wanalazimisha kupanda gari wakati serikali imeshakataza.

No comments :

Post a Comment