Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na Balozi wa China
nchini Tanzania Wang Ke wakitia sahihi makubaliano ya kupokea msaada wa
vifaa kinga vya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
********************************
Na.WAMJW-Dar es Salaam
Ubalozi wa China nchini Tanzania
umeipatia Serikali msaada wa vifaa kinga kwa ajili ya
kuendelea
kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 (Corona), na kuahidi
kuendelea kushirikian na Serikali ya Tanzania kukabiliana na ugonjwa
huo, hadi hapo utakapomalizika.
Akipokea vifaa hivyo Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema
msaada huo utaenda kwa watumishi wa afya kote nchini kwani serikali
imetoa kipaumbele cha kwanza kwao ili kuweza kuwakinga na maambukizi ya
Covid-19.
“kwa niaba ya serikali
tunaishukuru sana Serikali ya China kwa mchango huu, na niendelee
kuwathibitishia wale wote mnaoisaidia Serikali ya Tanzania,msaada huu
tutaupeleka kwa watumishi wa afya,kipaumbele ni kuwakinga watumishi wa
afya wasipate maambukizi”
Ummy Mwalimu amesema msaada huo
uliotolewa na ubalozi wa China nchini Tanzania ni pamoja na mavazi (PPE)
1,000 ya kujikinga wakati wa kuhudumia watu waliothibitika kuwa na
ugonjwa wa corona, Barakoa (Mask) 100,000 pamoja na Vipima joto vya
mkono(thermal scanner) 150.
Kwa upande wake balozi wa China
nchini Tanzania Mhe. Wang Ke amesema nchi yake na Tanzania ni marafiki
kwa muda mrefu na ugonjwa huo ulipoikumba Nchi yao kwa mara ya kwanza,
Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono katika mapamabana dhidi
ya ugonjwa huo, hivyo na wenyewe wamejitoa kuisaidia kukabiliana nao.
Mhe.Wang Ke amesema Serikali ya
China kwa sasa imechukua hatua na kujitoa rasmi kuwa nchi itakayoisaidia
Tanzania katika misaada ya dharura ya vifaa kinga ambayo itasaidia
kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Corona.
Katika mwendelezo wa kuisadia
vifaa kinga Serikali ya Tanzania, kwa mara nyingine tena inatarajia
kupokea msaada wa vifaa tiba vya kusaidia wagonjwa kupumua (Ventilator)
500 kutoka kwa mfanyabiashara raia wa China Jack Ma.
No comments :
Post a Comment