Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo
Ijumaa Aprili 10, 2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari
kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama
kilichofanyika katika Hoteli ya Travellers mjini Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog.
Jeshi
la polisi Mkoa wa Shinyanga limeahidi kuendelea kushirikiana na Vyombo
vya Habari kuhakikisha vitendo vya uhalifu ikiwemo mauaji,ajali za
barabarani na ukatili wa kijinsia hususani mimba na ndoa za utotoni
vinatokomezwa mkoani humo.
Hayo
yamesemwa leo Ijumaa Aprili 10,2020 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Shinyanga ACP Debora Magiligimba katika kikao kazi chake na waandishi wa
habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama
kilichofanyika katika Hoteli ya Travellers mjini Shinyanga.
Kamanda
Magiligimba amesema suala la ulinzi na usalama ni jukumu la kila mtu
katika jamii huku akibainisha kuwa Waandishi wa habari wanayo nafasi
kubwa zaidi kuielimisha jamii kuachana na vitendo viovu ndiyo maana
Jeshi la polisi limekuwa likishirikiana bega kwa bega na waandishi wa
habari kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa.
“Naomba
waandishi wa habari tuendelee kushirikiana katika kuufanya mkoa wetu
unakuwa mahali salama pa kuishi kwa kuhakikisha tunapunguza ajali za
usalama barabarani,mauaji kuepuka vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake
na watoto”,amesema Kamanda Magiligimba.
Katika
hatua nyingine ameitaka jamii kuachana na tabia ya kupeleka watoto wa
kike/wasichana wadogo kwa waganga wa kienyeji kwenda kuoshwa dawa za
mvuto/nyota maarufu ‘Samba’ ili wapendwe na wanaume kwani inachangia kuwepo kwa matukio ya mimba na ndoa za utotoni.
"Mkoa
wa Shinyanga ulikuwa unakabiliwa na matatizo ya mauaji ya wazee na watu
wenye ualbino lakini sasa yamepungua kwa asilimia kubwa na kubaki
tatizo la mimba na ndoa za utotoni ambalo linasababishwa na mila na
desturi za kuogesha watoto wao wa kike dawa za mvuto wa mapenzi hasa katika wilaya ya Kishapu",amesema Magiligimba.
Amewaomba
waandishi wa habari kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kuandika habari
ambazo zitatoa elimu kwa wazazi na walezi kuachana na mila potofu za
kuogesha watoto wao wa kike dawa za mvuto wa mapenzi ili kutokomeza
mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga.
Kamanda
Magiligimba ametumia fursa hiyo kuwasihi wakazi wa Shinyanga kuzingatia
maagizo ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto
kuhusu Ugonjwa wa Corona ikiwemo kuepuka, Mikusanyiko isiyo ya lazima,
kuepuka kukumbatiana , kunawa mikono kwa maji na sabuni mara kwa mara na
kutumia Vitaka Mikono 'Sanitizer'.
Kwa
upande wake,Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi
amewashukuru wadau mbalimbali wa masuala ya ulinzi na usalama kwa
kushirikiana na jeshi la polisi kupunguza matukio ya mauaji ambapo
katika Kipindi mwezi Januari hadi Machi 2020 kuna matukio 6 yametokea
ukilinganisha na matukio 23 yaliyotokea Mwezi Septemba hadi Desemba
2019.
Naye
Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga ASP Africanus
Sulle amesema katika Kipindi hiki ambapo kuna Ugonjwa wa Corona Jeshi la
polisi limeendelea kutoa elimu kwa waendeshaji wa vyombo kuhakikisha
hawajazi abiria kupita kiasi ili kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa
Corona.
“Tunaendelea
kukabiliana na ujazaji abiria kwenye magari yanayoingia mjini na
yanayokwenda vijijini ili kukabiliana na ugonjwa wa Corona. Kwa upande
wa magari madogo mfano Hiace tunaondoa viti vya nyuma ya dereva ili
abiria wasiangaliane”,ameeleza Sulle.
Hata
hivyo amesema jeshi la polisi halitasita kuwachukulia hatua za kisheria
madereva bodaboda wanaoendesha kwa mwendo kasi Mjini Shinyanga huku
akibainisha kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa waendesha bodaboda kupitia
kwenye vituo vyao kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuhakikisha
wananawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na kutumia Sanitizer.
“Barabara
kuwa salama ni lazima,nami nitahakikisha nasimamia Sheria na kanuni za
usalama barabarani ili kuhakikisha tunapunguza ajali za barabarani
ambazo zinasababisha vifo,ulemavu na uharibifu wa mali”,ameongeza Sulle.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo
Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari
kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama
kilichofanyika katika Hoteli ya Travellers mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo
Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari
kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo
Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari
kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza leo
Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na waandishi wa habari
kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.
Kikao cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba na waandishi wa habari kikiendelea.
Katikati
ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba
akizungumza leo Ijumaa Aprili 10,2020 katika kikao kazi chake na
waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi
na usalama. Kulia ni Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa
Shinyanga ASP Africanus Sulle , Kushoto ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa
Shinyanga SP Davis Msangi.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Shinyanga SP Davis Msangi akizungumza katika
kikao cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba na
waandishi wa habari kilicholenga kujadili masuala mbalimbali ya ulinzi
na usalama.
Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga ASP Africanus
Sulle akizungumza katika kikao cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga
ACP Debora Magiligimba na waandishi wa habari kilicholenga kujadili
masuala mbalimbali ya ulinzi na usalama.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments :
Post a Comment