Wizara
ya afya nchini Urusi imesema leo kuwa ndege ya nchi hiyo iliyobeba
vifaa vya tiba imeondoka nchini humo kuelekea Marekani, huku ikulu ya
Kremlini ikitanua ushawishi wake wakati huu wa janga la virusi vya
corona.
Video iliyotolewa na wizara hiyo, ilionyesha ndege hiyo ya mizigo iliyobeba masanduku ikijiandaa kuondoka katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Moscow mapema leo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa la AFP, wizara hiyo ilikataa kutoa habari zaidi kuhusu hatua hiyo inayokuja baada ya rais wa Urusi Vladmir Putin kuzungumza na mwenzake wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatatu.
Awali Urusi ilituma vifaa vya matibabu na watalaamu wa virusi vya corona katika taifa la Italia lililoathirika pakubwa kutokana na virusi hivyo kama sehemu ya juhudi zake za kibinadamu ambazo wachambuzi wanasema zimebeba ushawishi mkubwa wa kijiografia na kisiasa.
-DW

No comments :
Post a Comment