Mbunge wa Kibaha Mjini, Slyvestry
Koka Akimkabidhi Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Edwin Shunda (Kushoto) Mizinga Kumi ya Nyuki Yenye
Thamani ya Shilingi Milioni 1.5, Kwa Ajili ya Mradi wa Ufugaji wa
Nyuki, Makabidhiano Hayo Yalifanyika katika Ofisi za CCM Kibaha Mjini,
Jana. Picha na Ofisi ya Mbunge.
…………………………………………………………………..
NA:MWANDISHI WETU,KIBAHA.
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini, Slyvestry Koka, Amekabidhi Mizinga 10 ya Nyuki Yenye
Thamani ya Shilingi Milioni 1.5 kwa Umoja wa
Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini kwa
Ajili ya Mradi wa Ufugaji wa Nyuki.MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini, Slyvestry Koka, Amekabidhi Mizinga 10 ya Nyuki Yenye
Akizungumza Wakati wa Makabidhiano
Hayo, katika Ofisi za CCM Kibaha Mjini, Jana, Mbunge Koka Aliipongeza
Jumuiya Hiyo kwa Kupata Mwenyekiti Mwenye Maono Makubwa ya Kuiendeleza
Jumuiya Hiyo kwa Kuitafutia Miradi Mbalimbali.
“Niwapongeze Jumuiya ya Wazazi
Kibaha Mjini kwa Kupata Mwenyekiti Shunda Ambaye Anajitambua,Mbunifu na
Mckarikaji katika Kutaka Kuacha Alama kwa Muda Aliopo Madarakani katika
Utawala Wake;
“Ninamfahamu Tangia Akiwa
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Forest Lililopo Kata ya Kongowe, Mengi
Nilishirikiana Nae Tulijenga kwa Pamoja Shule ya Msingi naSekondari ya
Mwambisi Lakini Hata Kuifufua Zahanati ya Mwambisi iliyokuwa Haifanyi
Kazi kwa Muda Mlefu” Alisema Mbunge Koka.
Aidha Mbunge Koka, Alisema kwa
Hamasa ya Maendeleo ya Jumuiya ya Wazazi Imempelekea Yeye Kama
Mwakilishi katika Jimbo Hilo la Kibaha Mjini Kutoa Mizinga 10 Kwa Ajili
ya Kuchagiza na Kutunisha Mradi wa Ufugaji wa Nyuki Ambao Baada ya
Uvunaji wa Asali Utaipatia Jumuiya Hiyo Kipato.
Akizungumza Baada ya Kupokea
Mizinga Hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya CCM,
Edwin Shunda, Alimshukuru Mbunge Koka kwa Kuipatia Jumuiya Hiyo Mizinga
10 na Kusema Awali Walikuwa na Mizinga 30 kwa Kuongezewa Mizinga 10 Sasa
Mizinga imefika 40.
“Kwa Niaba ya Jumuiya ya Wazazi
Kibaha Mjini Tunamshukuru Mbunge Koka kwa Kutupatia Mizinga 10 ya Nyuki
Tayari Tuna Mizinga 30 Ambayo Tumeshatundika Kwenye Shamba Letu na Hii
10 Jumla 40” Alisema Mwenyekiti Shunda.
Pia Mwenyekiti Shunda Alitumia
Nafasi Hiyo Kuwashukuru Meneja wa Kanda wa Wakala wa Misitu Tanzania na
Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti wa Miti Dawa Kutoka Muhimbili kwa
Kuipatia Jumuiya Hiyo ya Wazazi Shamba Ekari 5 na Maji kwa Ajili ya
Ufugaji wa Mradi wa Nyuki Utakaozalisha Asali Baada ya Uvunaji na
Kuiletea Fedha Jumuiya Hiyo.
Aidha Katibu wa Jumuiya Hiyo
Kibaha Mjini, Daima Utanga, Alimshukuru Mbunge Koka kwa Kuipatia Jumuiya
Hiyo Mizinga 10 na Ameahidi Atatumia Utashi Wake na Juhudi Kubwa katika
Kuhakikisha Mradi Huo Unafanikiwa.
No comments :
Post a Comment