Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC) wametangaza kupitia tovuti yao na mitandao ya kijamii kuzindua
Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania 2019.
Ripoti imepangwa kuzinduliwa Jumatano, Aprili 29, 2020 kupitia mtandao wa YouTube (Haki TV), mtandao wa Zoom na mitandao ya Twitter, Facebook na Instagram.
Kwa mujibu wa LHRC, hii ni mara ya kwanza kwa shirika hilo la utetezi wa haki za binadamu hapa nchini kuzindua ripoti kwa njia ya kidigitali tangu walipoanza kuchapisha ripoti hiyo mwaka 2002.
Kwa mujibu wa LHRC, hii ni mara ya kwanza kwa shirika hilo la utetezi wa haki za binadamu hapa nchini kuzindua ripoti kwa njia ya kidigitali tangu walipoanza kuchapisha ripoti hiyo mwaka 2002.
LHRC imetaja sababu kubwa ya kulazimika
kufanya hivyo ni kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona ambao
umewalazimisha kufanya kazi kutoka nyumbani na kuepuka mikusanyiko ili
kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo hatari.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ripoti hiyo
itaangazia hali ya haki za binadamu kwa mwaka 2019 sambamba na kufanya
ulinganisho wa hali ilivyokuwa mwaka 2018. Ripoti ya Haki za Binadamu
Tanzania inayoandaliwa na LHRC huangazia haki zote za binadamu ikiwemo
haki za kiraia na kisiasa, haki za kiuchumi, haki za maendeleo na haki
za makundi maalumu.
Ripoti hiyo pia huchambua ufanisi wa mamlaka za usimamizi wa haki na kutoa mapendekezo kwa lengo la maboresho.
No comments :
Post a Comment