………………………………………………………………………………….
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
linamshikilia JOYCE KEPHAS AKYOO @ MANKA [31] Mfanyabiashara na Mkazi wa
Stereo Jijini Mbeya kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kuhusu
ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu [COVID 19] katika Mtandao wa Kijamii.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe
27.04.2020 majira ya saa 13:30 Mchana baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya kufanya msako huko eneo la Stereo lililopo Kata ya Manga, Tarafa
ya Sisimba, Jijini Mbeya.
Ni kwamba mnamo tarehe 30.03.2020
majira ya saa 14:09 Mchana mtuhumiwa alituma taarifa
za uongo na zenye
lengo la kupotosha kuhusiana na ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu kwenye
kundi “Fans of Mwailubi Car Wash” katika mtandao wa WhatsApp kwa kuweka
picha za marobota ya nguo akieleza kwa maandishi na kwa sauti baada ya
kujirekodi akisema “Mablanket ya Wagonjwa wa Corona ambao wamefariki nchini China na nguo hizo zinaletwa barani Afrika na ugonjwa wa Corona” Mtuhumiwa aliendelea kuongea na kuandika akitahadharisha watu wasikubali msaada huo.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Tangu kuanza kwa Janga la Homa
Kali ya Mapafu [COVID 19] na kutangazwa kama Janga la Dunia, Serikali
kupitia Wizara ya Afya na Viongozi wakuu wa Nchi ndio wamekuwa wakitoa
taarifa kuhusiana na ugonjwa huo pamoja na namna ya kujikinga dhidi ya
maambukizi yake, hata hivyo Serikali imekuwa ikitoa makatazo mbalimbali
kwa wananchi kuacha kutoa taarifa za kupotosha umma na kusubiri kupata
taarifa kutoka vyanzo sahihi.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa
Mbeya linaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mpaka wa
Tanzania na Malawi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, maeneo ya
Karantini na kudhibiti magari ya kubeba abiria kwa kuwataka kupakia
abiria kulingana na siti zilizopo [level seat].
Pia elimu inaendelea kutolewa
kwa Wananchi katika maeneo mbalimbali namna ya kujikinga na ugonjwa wa
Homa Kali ya Mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona [COVID 19] na
kuwataka wananchi kufuata maelekezo yanayotolewa na Viongozi Wakuu wa
Nchi, Wataalamu na Wizara ya Afya ikiwemo kuvaa barakoa, kuepuka
mikusanyiko, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au
kutumia vitakasa mikono [Sanitizer].
No comments :
Post a Comment