Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akitoa ufafanuzi juu
ya malalamiko ya wananchi kuhusu kupanda kwa bei ya sukari
nchini, Jijini Dodoma leo tarehe 16 Aprili 2020
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa (Mb) ameyasema hayo
Jijini Dodoma leo tarehe 16 Aprili 2020 wakati akitoa ufafanuzi juu ya
malalamiko ya wananchi kuhusu kupanda kwa bei ya sukari.
Amesema
kuwa kila mwaka serikali imekuwa makini katika kutathmini mahitaji ya
sukari kwa wananchi kadhalika uwezo wa viwanda vya ndani katika
uzalishaji.
Bashungwa
amesema ni kweli bei ya sukari imepanda lakini haisababishwi na
upungufu wa sukari bali imesababishwa na waagizaji kushindwa kuagiza kwa
wakati kutokana na ugonjwa wa homa ya mapafu unayosababishwa na kirusi
cha Corona.
Ili
kukabiliana na kadhia hiyo serikali imetoa vibali vya jumla ya Tani
40,000 kwa kampuni 4 za wazalishaji ambapo kila kampuni imeagiza Tani
10,000
Waziri
Bashungwa amesema kuwa tayari sukari iliyokwisha ingia bandarini
kupitia kampuni ya Kagera Sugar ni Tani 9,990 na imeanza kutolea
bandarini tangu jana jioni.
Kadhalika
tarehe 24, 28 na 30 kampuni ya Mtibwa Sugar itaingiza jumla ya Tani
10,000. Kampuni ya Kilombero Sugar itaingiza jumla Tani 1,624 hivi
karibuni kutoka Malawi na Msumbiji huku Tani 1,800 ikiagizwa kutoka
Afrika Kusini.
Sambamba
na hayo amesema kuwa wiki ya kwanza ya mwezi Mei Kampuni ya Kilombero
Sugar itaingiza Tani 7,276 huku tarehe 15 Mei kampuni ya TPC itaingiza
Tani 5,000 na Tarehe 30 Mei Tani 4,500 zitaingia nchini.
Katika
hatua nyingine Waziri Bashungwa amesema kuwa Wizara inatarajia kuomba
nyongeza ya Tani 58,000 ili kukidhi mahitaji ya sukari kufikia Juni 2020
Hata
hivyo amesema kuwa Asilimia 80% ya sukari ambapo kwa mujibu wa Takwimu
mahitaji ya sukari inayotumiwa majumbani ni kiasi cha Tani 4,700,000
ambapo kati ya hizo Tani 378,000 zinazalishwa nchini.
Bashungwa
amesema kuwa Hiyo ni hatua kubwa kwa nchi na serikali katika mkakati wa
kuimarisha uchumi wa viwanda huku wawekezaji wengi wakiendelea na
mchakato wa uongezaji tija na uwezo wa uzalishaji
Kadhalika
wakulima wamekuwa na mtazamo mkubwa katika kuzalisha miwa kwa wingi
ambayo wataipeleka katika viwanda vya kuchakata sukari na Katika kipindi
cha hivi karibuni serikali itafikia uwezo mkubwa wa uzalishaji hivyo
kuwa na ziada ya skari itakayouzwa nje ya nchi.
No comments :
Post a Comment