JESHI LA UHAMIAJI LAIMARISHA UKAGUZI KWENYE VIZUIZI NJOMBE
……………………………………………………………………………
Joctan Agustino,NJOMBE
Jeshi la uhamiaji mkoa wa Njombe limeimarisha ulinzi wa masaa 24 na
kuendesha operesheni ya ukaguzi mkali wa magari ya mizigo na abiria
katika vizuizi vya barabara kuu za mkoa huo kikiwemo cha Mjini Makambako
kinachopitiwa na barabara ya TANZAMU(Tanzania na Zambia) na kubaini
idadi kubwa ya madereva hawazingatii miongozo ya wizara ya afya katika
kujikinga na mlipuko wa ugonjwa tishio wa CORONA.
Ukaguzi huo ambao umefanyika usiku wa kuamkia april 15 ukiambatana na
utoajiwa wa elimu kwa watumia barabara hususani watembea kwa
miguu,abiria na madereva umekuwa na mapokeo chanya kwa wananchi ambao
wamekuwa hawana elimu ya kina kuhusu namna bora ya kujikinga na ugonjwa
huo.
Awali Kamanda wa uhamiaji mkoa wa Njombe John Yindi na Sajenti
Godfrey Mchwekezi wakitoa elimu kwa abiria na madereva mara baada ya
kufanya ukaguzi wametaka watumiaji wa vyombo vya moto kuhakikisha
wanadai vitu vya kujikinga kabla ya kuingia kwenye chombo cha usafiri
na kisha kuweka bayana kwamba zoezi hilo kutokuwa na kikomo.
Operesheni hiyo inapata mapokeo chanya kwa madereva akiwemo Nikson
Salingo ambao wanasema itasaidia kudhibiti maambukizi mapya na kueleza
jitihada wanazochukua kujikinga pamoja na athari wanazokutana nazo
katika kipindi hiki cha mlipuko.
Mbali na kutoa elimu ya corona jeshi hilo pia limekagua vitamburisho
vya urai yanayotoka nje ya nchi katika barabara ya TANZAMU
inayounganisha nchi ya Tanzana na Zambia ambayo imekuwa na mikasa mingi
ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu wanaoingia nchini kinyemela.
No comments :
Post a Comment