************************************
Tanzania Red Cross Society leo
imepokea hundi ya sh. Milioni 230 kutoka katika kampuni ya Cocacola
Tanzania ikiwa ni mchango wa kuunga mkono shughuli zinazofanywa na
Tanzania Red Cross katika kukabiliana na Virusi vya CORONA.
Katika makabidhiano hayo
yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Tanzania Red Cross Mikocheni, jijini
Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Cocacola Tanzania
Ndg Halid Mzee Ali amesema kuwa Cocacola imeamua kuunga mkono Tanzania
Red Cross Society kwakua Red Cross ni ya wote na imepewa mamlaka na
serikali kushughulia janga hili nchini.
Nae Katibu Mkuu wa Tanzania Red
Cross Society Ndg Julius Kejo ameishukuru kampuni ya Cocacola Tanzania
na wadau wengine kwa kutambua na kuunga mkono kazi zinazofanywa na
Tanzania Red Cross katika kukabiliana na Virusi vya Corona.
Aidha, Balozi wa Kampuni ya
Cocacola na Tanzania Red cross Society Mrisho Mpoto amehamasisha
wananchi katika ngazi zote kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na
maambukizi ya Ugonjwa wa Covid-19 na kutoa kauli mbiu yake kwa
watanzania inayosema “Nguvu yetu ni maji na sabuni”.
No comments :
Post a Comment