…………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Bunge limetaka wizara ya maji kuweka usawa katika ugawaji wa miradi ya maji nchini ili kutoleta upendeleo katika maeneo mengine.
Hayo
yamebainishwa na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai wakati wa
mjadala wa
bajeti ya wizara ya maji kwa mwaka 2020/2021.
Akizungumza Mhe. Ndugai amesema kuwa hakuna usawa katika ugawaji wa miradi ya maji kwani kuna maeneo yamependelewa.
“Haiwezekani maeneo mengine vijiji viwe vichache huku maeneo mengine wakipatiwa mamilioni ya fedha” amesema Mhe. Ndugai
“ Profesa
tunakupitishia bajeti ya wizara yako ,lakini mambo hovyo, hakuna usawa
wengine Kijiji kimoja wengine wanapata mamilioni hapana hili linatakiwa
kuangaliwa kwa kina” ameeleza Mhe. Ndugai
Mhe. Ngugai amebainisha kuwa hilo ni tatizo kubwa unaweza ukaona wewe unapata ugali unashiba lakini hili ni tatizo kubwa .
No comments :
Post a Comment