Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw.Gerald Kusaya akikagua ofisi mpya za Bodi ya Mkonge jijini Tanga
baada ya kutekelezwa kwa agizo la Waziri Mkuu.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw.Gerald Kusaya (aliyevaa tai) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Mazao Bw.Nyasebwa Enock kuhusu bodi ya Mkonge kuweka bango
la ofisi eneo hilo.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Bodi hiyo Bw.Saad
Kambona
Picha ya pamoja kati ya Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( aliyevaa tai) na Menejimenti ya
Bodi ya Mkonge mara baada ya kukagua jengo la ofisi kufuatia agizo la
Waziri Mkuu la kuitaka bodi ihamie hapo toka ofisi za zamani uwanja wa
gofu jijini Tanga. Jengo hilo awali lilifahamika kama Medicare Hospital
Tanga.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw.Gerald Kusaya akiongoza mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
kuhusu mkakati wa kuinua zao la mkonge mkoa wa Tanga.Mazungumzo
yalifanyika jana ofisini kwa Mkuu wa Mkoa
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw.Gerald Kusaya (aliyevaa suti ya kaki) akiangalia bango litakalowekwa
katika jengo jipya la makao makuu ya bodi ya mkonge jijini Tanga ambalo
zamani lillifahamika kama Medicare Hospital Tanga.
Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Mhe.Martin Shigela akiongea na watumishi wa Bodi ya Mkonge
wakati alipotembelea makao makuu ya bodi hiyo jijini Tanga jana.
(Habari na picha na Wizara ya Kilimo)
…………………………………………………………………………………….
Na.Bashiri Salum,Wizara ya Kilimo,Tanga
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Gerald Kusaya ameipongeza Menejimenti ya Bodi ya
Mkonge na watumishi kwa
kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kuhamia katika ofisi iliyotwaliwa na
serikali hivi karibuni kutoka kwa wamiliki binafsi.
Kusaya ametoa pongezi hizo jana
(tarehe 27.O4.2020) Jijini Tanga wakati alipokwenda kufanya ufuatiliaji
wa utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu mwezi Machi mwaka
huu kufuatia ripoti ya kamati ya uchunguzi kuhusu mali za bodi ya mkonge
kumilikishwa kwa watu binasfi kinyume cha utaratibu.
“Nawapongeza menejimenti mpya ya
Bodi ya Mkonge kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa la kuhamia katika jengo hili na kuendelea na kazi za kusimamia
zao la mkonge”alisema Kusaya
Waziri Mkuu aliagiza kuwa jengo
lililokuwa linamilikiwa visivyo halali na Willian Kimweli Madundo na
kulitumia kama Medicare hospital Tanga litumike kuwa makao makuu ya bodi
kwani miaka ya nyuma ndipo palikuwa makao makuu ya Mamlaka ya Mkonge
Tanzania .
Aidha,Katibu Mkuu huyo aliigiza
bodi ya mkonge kuhakikisha inafuatilia mali zake ikiwemo nyumba 32
ambazo zilirejeshwa serikalini “ nataka waliokuwa wamiliki wapewe notisi
na kuondoka au wapewe mikataba ya upangaji haraka” alisisitiza
“Bado kuna nyumba mbili nchini
Uingereza,nataka zirejeshwe serikalini na zile nyumba mbili jirani na
Mkonge hotel hapa Tanga zifuatiliwe kujua uhalali wa umiliki wake “
alisema Katibu Mkuu huyo
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Bodi ya Mkonge Saad Kambona alimweleza Katibu Mkuu kuwa tayari
wameanza kufanya kazi kwenye jengo jipya la ofisi kama walivyoagizwa na
wamefanya ukarabati mdogo kuwezesha jengo hilo kutumika kama ofisi
badala ya ofisi za zamani uwanja wa gofu Tanga .
Kambona alisema kwa sasa wanaiomba
serikali kuendelea kuiwezesha bodi ili iweze kuhudumia zao la mkonge
wakati ikijipanga kuanza kujitegemea kimapato.
‘Tuna lengo baada ya kuimarisha usimamizi wa zao la mkonge nchini,bodi iweze kutoa gawio kwa serikali “alisema Kambona.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa
wa Tanga Martin Shigela aliipongeza Wizara ya Kilimo kwa jitihada zake
za kufufua zao la mkonge kwani ndio uti wa mgongo wawananchi wa Tanga.
Shigela alisema ni wakati sasa
wizara ya kilimo ikaongeza msukumo katika kuhakikisha mbegu za mkonge
zinapatikana kwa wingi na wakulima wanazipata kwa gharama nafuu. Mwisho
Imetolewa na ;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
TANGA
28.04.2020
No comments :
Post a Comment