Naibu Waziri wa Mali Asili na
Utalii Constantine Kanyasu (mrefu kuliko wote) kulia kwake ni Mkuu wa
Wilaya ya Mpanda mama Lilian Matinga; wakiwa pembezoni mwa bwawa la
Milala
Mmoja wa wanyama aina ya kiboko wanaolalamikiwa na wananchi wa kata ya Misunkumilo kwa uharibifu wa mazao
……………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu, Katavi
Zoezi la kuwahamisha wanyama pori
aina ya viboko wanaoishi katika bwawa la Milala manispaa ya Mpanda
mkoani Katavi limeendelea kukwama kutokana viboko hao kukimbilia
katika
mito midogo baada ya maji kujaa katika bwawa hilo kufuatia mvua
zinazoendelea kunyesha
Akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa
Mali Asili na Utalii aliyefanya ziara mkoani Katavi; Mtafiti wa wanyama
pori kutoka Taasisi ya Wanyama Pori ya TAWIRI Dk. Emmanuel Masenga
amesema zoezi hilo limesitishwa mpaka wakati wa kiangazi
Dk. Masenga ameeleza kuwa kwa sasa
viboko hao wamehamia katika mito midogo midogo inayojaza maji katika
bwawahilo ambapo ni vigumu kuwaondoa
“Kule hakuna barabara, na kama tukitaka kuwatoa huko tutafanya uharibifu mkubwa kwa mazao ya wananchi” alisema Dk. Masenga
Ameendelea
kuelea kuwa kiboko ana uwezo wa kutembea umbali wa kilometa kumi kwa
siku hivyo hata wakiondolewa wana uwezo wa kurudi katika bwawa hilo na
hivyo kupendekeza kujengwa kwa uzio kuzunguka bwawa pamoja na kuweka
askari wanyama pori kwa ajili ya kulinda eneo hilo
Bwana Iddo Richa ni mhandisi
kutoka Mamlaka ya Maji Mpanda, ambao ndio wasimamizi wa bwawa hilo,
amlisema wanahitaji kiasi cha shilingi bilioni moja nukta mbili ili
kujenga uzio kuzunguka bwawa hilo
Hata
hivyo alisema fedha hizo ni nyingi na hawawezi kuzipata kupitia
makusanyo yao hivyo kuomba serikali kuu kuangalia uwezekano wa kusaidia
Kwa upande wake Naibu Waziri wa
Mali Asili na Utalii mheshimiwa Constantine Kanyasu amewatoa wasiwasi
wananchi wanaoishi katika maeneo hayo na kuahidi serikali itatafuta
fedha za kujenga uzio
No comments :
Post a Comment