Kushoto ni Afisa Lishe Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision , Stella Mbuya na Afisa
Jinsia na Utetezi wa Shirika la World Vision kupitia mradi wa ENRICH,
Magreth Mambali wakionesha alama ya Usawa wa Kijinsia.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wanawake
wajawazito wamekumbushwa umuhimu wa kuhudhuria Kliniki angalau mara nne
katika kipindi chote cha ujauzito ili waweze kupata huduma zote za
msingi ili wajifungue salama kupunguza vifo vya uzazi vya mama na
mtoto.
Rai
hiyo imetolewa na Afisa Lishe Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika
la World Vision katika mikoa ya Shinyanga na Singida, Stella Mbuya
wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga
yaliyofanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga.
Mbuya
alisema endapo mama mjamzito atahudhuria kliniki itamsadia kupata
huduma zote za msingi katika kipindi chote cha ujauzito ili aweze
kujifungua salama ili kupunguza vifo vya uzazi na mtoto ambavyo pia
husababishwa na Lishe duni.
“World
Vision kupitia mradi wetu wa ENRICH,tunahamasisha akina mama kula
vyakula kwa kuzingatia mlo kamili unaoundwa na makundi matano ya chakula
ili kuimarisha afya ya uzazi na lishe kwa mama na mtoto aliyepo
tumboni”,alisema Mbuya.
“World
Vision pia tunaendelea kuwahamasisha matumizi ya maziwa ya mbuzi kwa
sababu maziwa ya mbuzi yana uwiano wa virutubishi/viini lishe vilivyopo
kwenye maziwa ya mbuzi yanakaribiana sana na maziwa ya binadamu tofauti
na wanyama wengine ama maziwa ya kopo”,alisema Mbuya.
Mbuya
aliwakumbusha akina mama wajawazito kutumia vidonge vya madini chuma na
Asidi ya Foliki ‘Folic acid sambamba na viazi lishe na mboga za majani
yakiwemo matembele kwa ajili ya kuongeza damu mwilini ili kukabiliana na
vifo vinavyotokana na upungufu wa damu.
Kwa
upande wake,Afisa Jinsia na Utetezi wa Shirika la World Vision kupitia
mradi wa ENRICH unaofadhiliwa na serikali ya Canada, Magreth Mambali
aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi
katika uchaguzi mkuu 2020.
“Tunapoelekea
kwenye uchaguzi Mkuu,World Vision tunasisitiza kumpa mwanamke nafasi
katika nyanja zote ikiwemo kiuchumi na kisiasa.Tunapenda mwanamke
ashiriki katika ngazi za maamuzi kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa
kwa sababu wanawake tunaweza na tumeshuhudia wanawake wengi wanafanya
vizuri katika masuala ya uongozi. Mfano Mzuri ni mama yetu Makamu wa
Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan”,alieleza Mambali.
Mambali
aliitaka jamii kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mimba na ndoa za
utotoni na kutomaliza masomo shuleni akibainisha kuwa mlinzi wa kwanza
wa mtoto wa kike ni jamii inayomzunguka.
Katika
hatua nyingine alifafanua kuwa,World Vision kupitia mradi wa ENRICH
inatekeleza afua zake kwa kuunda vikundi mbalimbali ikiwemo vikundi vya
‘Baba wanaojali’ ambao wamepata mafunzo ya kuwa baba wanaojali familia
zao na kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Alivitaja
vikundi vingine kuwa ni VICOBA kwa wanawake,klabu za afya ya uzazi kwa
vijana katika shule za msingi na sekondari na vikundi vya Sauti ya Umma
na Utendaji ambavyo vinajihusisha na utoaji elimu kwa wanawake juu ya
umuhimu wa kuhudhuria kliniki na kujifungulia katika vituo vya afya.
Kwa
upande Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale
aliwapongeza World Vision kwa kuendelea kushirikiana na serikali
kuhamasisha wanawake kuzingatia lishe ili kupunguza vifo vitokanavyo na
lishe duni.
Naye
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM)
alitoa wito kwa wazazi na walezi kupeleka watoto shule na kutowaozesha
wangali wadogo huku akiwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi
kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu 2020.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Machi 8,2020 ni “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya baadae”.
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (katikati)
akipokea maandamano ya wadau mbalimbali wa haki za wanawake na watoto
wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga
yaliyofanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga.Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga Mhe. Hoja Mahiba. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa
Shinyanga Kaimu ni James Bwana. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Maafisa
kutoka Shirika la World Vision kupitia Mradi wa ENRICH wakiwa wamebeba
bango lenye ujumbe wa ' Mlinde Mtoto wa kike, Mpe Mwanamke Nafasi' na
Kauli Mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka 2020 ' “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya baadae”.
Askari
polisi wanawake wakiwa kwenye maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku
ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya
Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM)
akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa
Shinyanga ambapo alitoa wito kwa wazazi na walezi kupeleka watoto shule
na kutowaozesha wangali wadogo.
Mbunge
wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM)
akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa
Shinyanga na kuwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi
za uongozi katika uchaguzi mkuu 2020.
Afisa
Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akilipongeza
shirika la World Vision kwa kuendelea kushirikiana na serikali
kuhamasisha wanawake kuzingatia lishe ili kupunguza vifo vitokanavyo na
lishe duni.
Maafisa
kutoka Shirika la World Vision kupitia Mradi wa ENRICH wakiwa na
matembele na viazi lishe,wameshikilia vipeperushi kwenye banda lao la
maonesho kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa
Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya
ya Shinyanga.
Maafisa
kutoka Shirika la World Vision kupitia Mradi wa ENRICH wakiwa
wameshikilia vipeperushi kwenye banda lao la maonesho kwenye Maadhimisho
ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata
ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Viazi
Lishe vikiwa kwenye banda la World Vision kwenye Maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya
Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
Afisa
Lishe Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision katika
mikoa ya Shinyanga na Singida, Stella Mbuya akionesha mboga za majani
'matembele' ambayo akina mama wajawazito wanashauriwa kutumia ili
kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu.
Maafisa
kutoka Shirika la World Vision kupitia Mradi wa ENRICH wakiwa na mbuzi
kwenye bando lao la maonesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake
Duniani Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya Iselamagazi
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Maafisa
kutoka Shirika la World Vision kupitia Mradi wa ENRICH wakionesha alama
ya Usawa wa Kijinsia wakati Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri
ya wilaya ya Shinyanga.
Maafisa
kutoka Shirika la World Vision kupitia Mradi wa ENRICH wakionesha alama
ya Usawa wa Kijinsia wakati Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri
ya wilaya ya Shinyanga.
No comments :
Post a Comment