Monday, March 9, 2020

WAZAZI WENYE WATOTO MAHITAJI MAALUM WAASWA KUWAPELEKA SHULE WATOTO WAO BADALA YA KUKAA NAO NYUMBANI


 Kaimu Mkurugenzi Hadija Mwinuka akishiriki michezo na watoto wenye mahitaji maalum
 Watoto wakipangwa kwa ajili ya michezo mbalimbali
 Kaimu Mkurugenzi Hadija Mwinuka akitoa neno kwa wageni waalikwa
 Walimu pia walishiriki michezo na watoto hao
 Kaimu Mkurugenzi akikabidhi mwanagunzi msumeno utakaomwezesha katika shughuli zao za ufundi
 Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa kwa watoto haoKaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Hadija Mwinuka ametoa wito kwa wazazi wenye watoto wenye ...mahitaji maalum wawapeleke shule badala ya kukaa nao nyumbani na kuwafungia
Ameyasema hayo wakati akitoa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na wanawake viongozi wa Elimu Wilaya ya Tandahimba kwenye shule maalum mjimpya
Mwinuka ameeleza kuwa shule hiyo ni bweni hivyo wanapokea watoto wakike na wakiume  wananchi waache kuwafungia ndani badala yake wawapeleke wakapate elimu mbalimbali katika shule hiyo
"Wananchi tuitumie shule maalum mjimpya kwa kuwapeleka watoto,walimu tunao wenye wito hivyo wanafundisha hadi mtoto  anafika hatua ya kujihudumia yeye mwenyewe,tukiwaacha majumbani wqnaopata tabu ni akina mama,"amesema Mwinuka
Naye mwalimu Mkuu wa shule Mohamed chipuputa  ameeleza kuwa wanafunzi hao wanafundishwa pia stadi za kazi  wanapofikia hatua ya kujielewa hivyo inampa uwezo wa kupata kipato
"Tunawafundisha  waweze kujihudumia wenyewe hapa tunawafundisha kuanzia watoto wa awali na kuendelea sambamba na shughuli za ufundi kama kushona,ufundi selemala,ufugaji na shughuli zingine ambazo hata akiwa nyumbani atasaidia kazi mbalimbali,"amesema Chipuputa

No comments :

Post a Comment