Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na
wanawake wajasiriamali mkoani Simiyu wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya
Wanawake Wajasiriamali kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.
……………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu Simiyu
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amezindua
maonesho ya wajasiriamali na huduma na kuwataka wakazi wa Simiyu
kujitokeza kuchangamkia fursa hasa wanawake ili kujikwamua kiuchumi.
Ameyasema hayo leo
wakati akifungua maonesho ya wanawake wajasiriamali na kuupokea msafara
wa kijinsia ukizunguka katika katika mikoa tisa kutoa elimu ya kupambana
na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Waziri Ummy amefungua
maonyesho hayo ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya
Siku ya Wanawake Duniani yatakayohitimishwa tarehe 8 Machi, 2020.
Aidha amempongeza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya
Maendeleo ya Jamii, John Jingu kwa kufanikisha maadhimisho hayo
zikiwemo
Taasisi mbalimbali.
Akizungumzia
uboreshaji wa bidhaa lishe amesema Wizara ya Kilimo na Wizara ya Afya,
zinaweza kushirikiana kuboresha chakula lishe kwa watoto na kukabiliana
na udumavu kwa watoto.
“Tukishirikiana kuwawezesha wanawake hawa kutumia teknolojia rahisi kukabiliana na udumavu kwa watoto” Alisema Waziri Ummy.
Amepongeza huduma na
elimu kupitia misafara ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoratibiwa na
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali.
“Misafara hii imewafikia watu wengi na hivyo kupata elimu itakayowasaidia kuondokana na vitendo vya ukatili” alisema.
Ameongeza kuwa anazo
taarifa za wanaume wanaopata vipigo kutoka kwa wenza wao hivyo, wasione
aibu kutoa taarifa kwenye madawati ya jinsia kwa ajili ya kupata
msaada.
“Ingawa unyanyasaji wa vipigo uko kwa wanawake lakini wanaume msiogope kuripoti pale mnaponyanyaswa ili mpate msaada” alisema
Kwa upande wake
Katibu Mkuu- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu amesema
Wizara kwa kushirikiana na wadau imejidhatiti katika kuhakikisha inatoa
elimu kwa jamii ili kuweza kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia
Amesema kupitia
makongamano na msafara wa kijinsia, Wizara imewafikia wadau wengi na
lengo lilikuwa ni kuwafikia watanzania katika ngazi mbalimbali.
Akitoa salamu za
Wizara ya ya kilimo, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Hussein Bashe amesema
wizara yake inatambua mchango wa wanawake katika sekta hiyo.
“Kila penye wakulima
wanne, watatu ni wanawake hivyo mchango wa wanawake katika kilimo ni
mkubwa sana tunautambua sana mchango wenu wanawake” alisema
Maadhimisho ya Siku
ya Wanawake duniani 2020 yanaongozwa na Kaulimbiu ya isemayo Kizazi cha
Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa na baadaye.
No comments :
Post a Comment