WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameonya tabia ya baadhi ya wenyeviti wa vijiji
wanaofanya biashara ya ardhi waache na badala yake amewataka... wajihusishe
katika kutekeleza majukumu yao ya msingi.
Ameyasema
leo(Jumatano, Machi 4, 2020) wakati akizungumza na wananchi kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Bokwa
wilayani Kilindi akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani Tanga.
Waziri
Mkuu amesema tabia ya baadhi ya wenyeviti wa vijiji kujihusisha na
biashara ya uuzaji wa ardhi inachangia kuwepo kwa migogoro, hivyo
amewataka wasijihusishe na masuala hayo.
“…Wanaouza
ardhi za vijiji bila ya kuwa na vibali vya halmashauri wachukuliwe
hatua kwa sababu ndio wanaosababisha migogoro ya ardhi. Viongozi acheni
tabia ya kuwaingiza wananchi kwenye migogoro.”
Pia,
Waziri Mkuu ameonya tabia ya wafugaji kuingiza mifugo kwenye mashamba
ya wakulima.“Haikubaliki na haiingii akilini katika hali ya kawaida mtu
amelima shamba lale la chakula alafu mwingine anaenda kuingiza mifugo
haikubaliki.”
Waziri
Mkuu ameongeza kuwa “kama unadhani mahindi ndio chakula bora cha
ng’ombe wako lima ulishe mifugo. Hakuna Mtanzania aliyeko juu ya sheria
kama kuna mtu ameua kwa kulinda ng’ombe wake, Mkuu wa Wilaya fanya
uchunguzi wa jambo hilo na hatua zichukuliwe.”
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi
waliodai kuwa kuna mkulima ameuawa na mfugaji kutokana na mgogoro
uliotokea wakati mfugaji alipoingiza mifugo kwenye shamba la mkulima.
Akizungumzia
kuhusu mgogoro wa mpaka kati ya wilaya ya Kilindi (Tanga) na Kiteto
(Manyara) amesema suala hilo iachiwe Serikali kwani tayari imeshaanza
kulishughulikia.
Wakati
huo huo, Waziri Mkuu amesema wilaya ya Kilindi itajengewa hospitali ya
wilaya ili kuwapunguzia wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za
afya.
Pia,
Waziri Mkuu aliwataka wananchi waendelee kuiamini Serikali yao na
kwamba changamoto mbalimbali zinazowakabili zikiwemo za upatikanaji wa
huduma za maji, umeme na miundombinu ya barabara zitafanyiwa kazi.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amezindua mradi wa maji wa Bokwa na amesema kwamba Serikali
ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la
upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini
ikiwemo na wilaya ya Kilindi.
Waziri
Mkuu amesemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya
kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote
nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao.
Awali,
Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa kituo cha
afya cha Mswelo kilichopo kwenye kata ya Kwediboma, ambapo amesema awali
Serikali ilitoa sh. milioni 300 kwa ajili ya ujenzi huo na itaongeza
sh. milioni 200 ili kituo hicho kikamilike.
(mwisho)
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
No comments :
Post a Comment