Wednesday, March 4, 2020

Picha : MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AFUNGUA KONGAMANO KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI...AWATAKA WANAWAKE KUJITOSA UCHAGUZI MKUU 2020

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing linalofanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

****

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi ikiwemo Udiwani na Ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.

Mhe. Samia ametoa wito huo leo Jumatano Machi 4,2020 wakati akifungua Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing linalofanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam.

Alisema Mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi hivyo ni vyema wanawake wakajitokeza kuwania nafasi za uongozi huku akiwataka wanawake kuacha tabia ya kubezana pale mwenzao anapojitokeza kugombea nafasi za uongozi.
“Huu ni mwaka wa uchaguzi,Wanawake tujitokeze katika majimbo,tujitokeze kwa wingi katika nafasi za udiwani na kisha tujaze kwa wingi fomu za viti maalumu. Tuhamasishe wanawake wajitokeze kugombea nafasi za uongozi”,alisema.
“Wanawake ni Jeshi kubwa katika kuleta usawa lakini cha kushangaza Mwanamke ndiyo wa kwanza kumponda mwenzie. Haya tuyaache,Ukiona mwanamke mwenzio kachukua fomu ya kugombea msaidie siyo kumponda.Mimi mwenyewe nimefikia hatua hii baada ya kushikwa mkono”,aliongeza.
Aliwaasa wanawake kushikamana kuiomba jamii kwa kuwashika mkono wanawake wenye sifa za kuwa viongozi ili kuhakikisha idadi ya wanawake katika meza za maamuzi inaongezeka hatimaye kufikia usawa wa kijinsia.
Alisema kuhusu suala la ushiriki wa wanawake katika meza ya maamuzi serikali imechukua hatua kadhaa ili kuondoa vizingiti vinavyowazuia wanawake wasishiriki kikamilifu katika meza ya maamuzi.

“Changamoto iliyopo ni uchache wa wanawake wenye uwezo wa kugombea nafasi mbalimbali iwe kwenye uongozi wa kisiasa,biashara,asasi za kiraia na sekta binafsi. Ni jukumu letu kama watetezi wa haki za wanawake kushawishi wanawake wenye uwezo kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika Nyanja tofauti”,alisema.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) Prof. Ruth Meena Prof. Meena kutoka WFT,alisema licha ya wanawake kuwa nguzo kuu ya Maendeleo katika kukuza uchumi wa nchi bado wanabeba mzigo mkubwa wa kulea na kuendeleza kizazi cha taifa bila nyenzo wezeshi katika kaya na jamii zao hali inayosababisha umaskini na ufukara wa dunia kuendelea kubeba sura ya mwanamke na msichana.
Prof. Meena kutoka WFT inayofanya shughuli za utetezi wa haki za wanawake na ujenzi wa tapo ya wanawake Tanzania,alisema pamoja na ongezeko la wanawake na wasichana katika uongozi na meza za maamuzi lakini bado ushiriki wao katika katika meza hizo za maamuzi haupo sawia katika Nyanja zote za kisiasa,kiuchumi na hata ki – ustawi wa jamii. 
“Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanyika kuleta mabadiliko kwenye sera na sheria za nchi,bado kuna mifumo kandamizi na ya kiubaguzi katika mifumo hi, hivyo kuna umuhimu wa uwajibikaji zaidi kwenye kubomoa mifumo kandamizi hususani mfume dume”,alisema. 
Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing likiongozwa na Kauli mbiu ya ''Uwajibikaji wa uongozi kwenye kujenga kizazi cha usawa wa jinsia'' limeandaliwa na  Mtandao wa Wanawake na katiba, Uchaguzi na Uongozi kwa ufadhili wa Women Fund Tanzania, Global Affairs Canada, Embassy of Ireland, High Commission of Canada na WiLDAF. 

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing linalofanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) linalofanya shughuli za utetezi wa haki za wanawake na ujenzi wa tapo ya wanawake Tanzania, Prof. Ruth Meena akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Mwenyekiti wa Bodi ya WFT, Prof. Ruth Meena akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania, Mary Rusimbi akizungumza wakati wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania, Mary Rusimbi akionesha tuzo ya kutambua mchango wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika harakati za ukombozi wa wanawake nchini Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha tuzo aliyotunukiwa kutokana na harakati zake za ukombozi wa wanawake nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza wakati wa majadiliano kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika la Msichana Initiative Rebeca Gyumi akizungumza wakati wa majadiliano kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Mkurugenzi  Mtendaji wa shirika la Door of Hope Tanzania,Clemence Mwombeki akichangia hoja kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
MwanaMtandao Asseny Muro akichangia hoja kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Meneja Miradi wa shirika la Young Women Leadership (YWL) mkoani Shinyanga Veronica Massawe akichangia hoja kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania, Mary Rusimbi akichangia hoja kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Mkurugenzi  Mtendaji wa shirika la Women Wake Up(WOWAP) ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma Hassan Toufiq akichangia hoja kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wakiwa ukumbini.

Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye kwenye Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing linalofanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam. 

Wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Kuadhimisha na Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na Miaka 25 baada ya Mkutano wa Beijing wakipiga picha ya kumbukumbu.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

No comments :

Post a Comment