Wednesday, March 4, 2020

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMUAGIZA DC KILINDI KUWACHUKULIA HATUA KALI WANAOUZA ARDHI KIHOLELA


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa wilaya
ya Kilindi Sauda Mtondoo kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wanaouza ardhi
kiholela bila kibali cha Halmashauri kutokana na kwamba wao ndio

chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji.

Majaliwa aliyasema hayo leo wakati akizungumza na
wananchi Kata ya Kwediboma wilayani Kilindi mkoani Tanga kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake
ya siku sita mkoani hapa ambapo pamoja na mambo mengine alipata fursa ya
kusikiliza kero zinazowakabili wananchi na kuzitoa ufafanuzi.
Kauli ya Waziri Mkuu inatokana na miongoni mwa mabango
yaliyoonyeshwa kwenye mkutano wake na mmoja wa wananchi wa Kata hiyo
akieleza uwepo wa migogoro ya ardhi jambo ambalo lilimlazimu kutoa kauli hiyo
Waziri Mkuu alimtaka Mkuu huyo wa wilaya kuhakikisha
wanazipatia ufumbuzi changamoto za migogoro ya ardhi zilizopo kwenye maeneo yao
kwani zimekuwa zikikwamisha juhudi kubwa maendeleo kutokana na wananchi kutumia
muda mwingi kutafuta  suluhu badala ya
kushiriki kwenye shughuli za uzalishaji. 
“Mkuu wa wilaya hapa Kilindi nimepata malalamiko kwamba
kuna migogoro ya ardhi na hili limekuwa ni tatizo kubwa sana hivyo nikuagize
kwamba wale wote wanaouza ardhi bila kibali cha Halmashauri wachukuliwe hatua
za kisheria”Alisema Waziri Mkuu.
“Kwani wamekuwa wakituingiza kwenye migogoro isiyokuwa
ya muhimu na siku ile madiwani wenzangu nimewaambia msijiingize kwenye mambo ya
kukata mipaka ipo imeshachorwa na ipo na ramani zipo sasa wewe ukisema mpaka
hapo sio sawa”Alisema
Waziri Mkuu alisema kwamba mkoa huo ulikuwa kwenye mkoa
kabla ya kugawanya manyara  na Tanga na
Arusha kulikuwa na ramani ingawa mikoa haibadiliki ramani ni ileile haiwezekani
kubadilishwa mipaka ya kimkoa ipo vile vile.
“Hivyo tunagombania nini hapa sasa…. vongozi tuache
tabia ya kuwaingiza wananchi kwenye migogoro isiyokuwa muhimu niliwambia siku
ile haizuiliki mwananchi wa Kilindi kwenda kulima Kiteto na wa kiteto kufanya
hivyo kilindi lakini zifuatwe taratibu kwa mamlaka husika”Alisema
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo,Naibu Waziri wa
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Anjelina Mabula alisema changamoto kubwa  ya wilaya ya Kilindi ni migogoro mingi ya
ardhi kama alivyosema Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella.
Alisema kwamba wao kama wizara wanalitambua hilo na
walikwishakutana na wapo kwenye hatua nzuri kuhakikisha migogoro yote inakwisha
ili wananchi waweze kuishi kwa amani kwenye maeneo yao.
“Lakini katika jambo hilo suluhu kubwa kuwafanya wana
kilindi kuwa na amani ni kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye maeneo
yao yote kama tulivyofanya kwenye mkoa wa Morogoro kwenye wilaya ya Kilomober,Ulanga
na Malinyi”Alisema
Aidha alisema kwa sababu changamoto iliyopo ni namna ya
matumizi ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji na tatizo kubwa kama alivyoeleza
Mkuu wa mkoa ni viongozi kutokuwa waaminifu na watu kutokutambua mipaka yao
vizuri.
Hata hivyo alieleza Waziri Mkuu kwamba serikali
haijafumbia macho suala hilo na wamelifikisha kwenye hatua nzuri na muda sio
mrefu wanakwenda kulipatia suluhu ya moja kwa moja kuachana na migoigoro hiyo.
Waziri Mkuu bado yupo mkoani Tanga kwa ziara ambapo kesho anatarajiwa kuendelea na ziara yake kwenye wilaya ya Lushoto

No comments :

Post a Comment