Mwenyekiti wa chama cha
wafanyakazi wanawake wa serikali na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani
Catherine Katele kulia akimkabidhi msaada wa magunia ya mahindi Katibu
Tawala wa Wilaya ya Rufiji Maria Katemana kwa ajili ya kuwapatia
wananchi waliopata maafa ya mafuriko kutoka na mvua zilizonyesha hivi
karibuni.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Baadhi ya wanawake wa Chama cha
Tughe Mkoa wa Pwani wakiwa wanatoa msaada wa mahindi kwa Katibu Tawala
wa Wilaya ya Rufiji akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali wa
serikali kwa ajili ya kuwapatia wananchi ambao mazao yao yamesombwa na
maji na wengine nyumba zao kuzingirwa kutoka na mafuriko
yaliyotokea.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Wanawake wa chama cha Tughe Mkoa
wa Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wa
serikali wakiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji mara baada ya
halfa fupi ya kukabidhi magunia ya mahindi lengo ikiwa ni kuwapatia
wananchi ambao wamekumbwa na maafa ya mafuriko na kusababisha mazao yao
kusombwa na maji.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji
Maria Katemana akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa wanawake wa
Tughe Mkoa wa Pwani walipofika ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha
na kutoa msaada wa magunia ya mahindi pamoja na vyakula mbali mbali wa
wananchi ambao wanamahitaji kutokana na kupata mafuriko.(PICHA NA VICTOR
MASANGU.)
Mwenyekiti wa chama cha
wafanyakazi wanawake wa serikali na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani Catheline
Katele akifafanua jambo kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji hayupo
pichani kuhusiana na ujio wao wa kufanya ziara maalumu yenye lengo la
kutoa msaada wa vyakula mbali mbali ikiwemo magunia ya mahindi kwa ajili
ya wahanga wa mafuriko.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji
Maria Katemana akiwa na wanawake wa Tughe Mkoa wa Pwani wakiwa
wanatembea kwa furaha mara baada ya kumalika kwa sherehe ya kutoa msaada
wa vyakula mbali mbali ikiwemo magunia ya mahindi ambayo yametolewa kwa
ajili ya kuwasaidia wananchi waliokumbwa na mafuriko(PICHA NA VICTOR
MASANGU)
Baadhi ya viongozi wa Tughe Mkoa
wa Pwani wakiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji wa kati kati
wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kufurahi mara baada ya kumaliza kutoa
msaada wa magunia ya mahinda kwa waananchi waliokubwa na maafa ya
mafuriko.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Baadhi ya wanawake wa Tughe Mkoa
wa Pwani wakiwa wanaimba nyimbo maalumu mara baada ya kuwasili katika
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rufiji kwa ajili ya halfa ya kukabidhi
mahitaji mbali mbali kwa wananchi ambao walipatwa na mafuriko na mazao
yao kusombwa na maji na wengine nyumba zao kuzingirwa na maji.(PICHA NA
VICTOR MASANGU)
*********************
VICTOR MASANGU, RUFIJI
Baadhi ya wananchi Wilayani Rufiji
Mkoa wa Pwani wamekosa makazi ya kuishi kutokana na
nyumba zao pamoja
na maduka kuzingirwa na maji ikiwemo wengine kukumbwa na changamoto ya
mazao yao mbali mbali zaidi ya hekta 4000 kusombwa na maji kufuatia
mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha maafa hayo ambayo
yamepelekea wananchi kuishi katika mazingira magumu hivyo kupelekea
kuishi katika mazingira magumu.
Hayo yalibainishwa na wananchi
hao wakati wa ziara ambayo imefanywa na Wanawake wa chama cha
wafanyakazi wa serikali na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani yenye lengo la
kutembelea baadhi ya maeneo ambayo yamekumbwa na maafa ya mafuriko kwa
ajili ya kutoa msaada wa vyakula kwa walengwa.
Wananchi hao wakizungumza kwa
nyakati tofauti akiwemo Shamte Ally na Said Salumu walisema walidai
kwamba mvua ambazo zinaendelea kunyesha kwa kipindi hiki zimewaletea
hasara kubwa ya mazao yao, mifugo, pamoja na makazi kuzingirwa na na
maji hivyo wameimba serikali ya awamu ya tano kuwasaidia msaada wa
kupata chakula pamoja na sehemu kwa ajili ya kuishi.
Aidha waliongeza kuwa kwa sasa
kutokana na kuwepo kwa hali hiyo baadhi ya bidhaa ya vyakula katika
maeneo mengine zimepanda bei hivyo wengine kutokana na kipato chao kuwa
cha chini wanashindwa kumudu gharama kwa ajili ya kununua vyakula hivyo
wameomba wadau mbali mbali kwa kushirikiana na serikali kuliangalia
suala hilo kwa jicho la tatu katika kuwasaidia kuondokana na hali hiyo.
“Kwa kweli ndugu waandishi kwanza
tunashukuru sana hawa wakinamama wa Tughe Mkoa wa Pwani kwa kuweza kuja
mpaka uku katika maeneo ya Rufiji, kwani kwa sasa tupo katika hali ngumu
sana kutokana na mazao mbali mbali ya chakula ambayo ndio tulikuwa
tunayategemea sisi pamoja na watoto wetu yote wamesombwa na maji, lakini
pia tunashukuru kupatiwa msaada huu lakini bado tunahitaji zaidi ili
tuweze kujikimu,” walisema wananchi hao.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa
Wilaya ya Rufiji Maria Katemana alikiri kuwepo kwa maafa hayo na
kubainishwa kwamba hadi sasa zaidi ya hekta 4000 za mazao ya aina mbali
mbali ikiwemo mahindi mpunga, yamesombwa na maji ambapo pia kuna
baadhi ya shule nne za msingi zimefungwa kwa muda kutokana na kuwepo
kwa hali hiyo ya mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
“Kwanza kabisa napenda kutoa
shukrani zangu kwa niaba ya serikali ya Wilaya ya Rufiji kwa msaada huu
wa chakula cha mahindi ambao umetolewa na Wanawake wa Tughe Mkoa wa
Pwani kwa lengo la kuwasaidia baaadhi ya wananachi amabao wamekumbwa na
mafuriko hayo ambayo kwa kweli yamesabisha hekta zaidi ya 4000 za mazao
kusombwa na maji na kuna maeneo mengine ya shule bado maji yapo, hivyo
tunaendelea kujitahidi kwa hali na mali ili wanafunzi waweze kuendelea
na masomo yao, alisema Maria.
Kufuatia kutokea kwa maafa hayo
ya mafuriko Wanawake kutoka chama cha wafanyakazi wa serikali na afya
(TUGHE) Mkoa wa Pwani wameguswa na tukio hilo na kuamua kwenda kutoa
msaada wa vyakula mbali mbali ikiwemo mahindi kwa wananchi ambao
wamekubwa na maafa ya mafuriko hayo kwa lengo la kuwasaidia kuweza
kupata chakula ikiwemo kupata mbegu kwa ajili ya kupanda tena kutokana
na mazao yao yaliyosombwa na maji.
Mwenyekiti wa chama cha
wafanyakazi wanawake wa serikali na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani
Catherine Katele alisema kwamba waliamua kwenda kutembelea baadhi ya
maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko na kutoa msaada wa vyakula kama
mahindi ambayo yatawasaidia wananchi kuweza kupata chakula na mengine
kuyatumia kwa ajili ya kupanda mazao mengine ambayo yamekwenda na maji.
“Sisi kama wanawake wa tughe
Katika Mkoa wa Pwani kwa kweli tumegiswa sana na jambo hili la wenzetu
wa Rufiji kupata maafa ya mafurikio, hivyo ktukaona ni vema tufunge
safari ya kuja mpaka huku na kweli tumjionea jinsi ya nyumba mbali mbali
ambanzo zimezingirwa na maji na mazao ambayo yamesombwa na maji kwa
hiyo kwa hiki kidogo tulichokitoa cha msaada wa mahindi kitaweza
kuwasaidia kwa namna moja hama nyingine na pia tutazidi kuendelea kutoa
misaada mbali mbali kwa watu wenye mahitaji, “alisema Katele.
Wilaya ya Rufiji iliyopo Mkoa wa
Pwani ambayo ina jumla ya kata zipatazo 13 imekuwa ikikabiliwa na
changamoto ya maafa ya mafuriko hasa katika kipindi cha mvua
zinaponyesha kutokana na baaadhi ya maeneo kuwepo pembezoni mwa mto
Rufiji hivyo kupelekea baadhi ya mazao kusombwa na maji na nyumba
nyingine kuzingirwa na maji na kusababisha wananchi kuishi katika
mazingira magumu
No comments :
Post a Comment