Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza
na viongozi pamoja na maafisa wa mkoa wa Arusha wakati wa kuanzisha
rasmi ofisi ya ardhi ya mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha
Kamishna Mstaafu Zelothe Stephen.
Viongozi na maafisa wa mkoa wa
Arusha wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Lukuvi wakati wa kuanzisha rasmi ofisi ya ardhi ya ka nda ya
mkoa wa Arusha.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsikiliza Mzee Mashauri
Rajabu mkazi wa Arusha mwenye mgogoro wa ardhi ambapo waziri Lukuvi
alimueleza afikishe mgogoro wake katika ofisi mpya ya Kamishna wa ardhi
mkoa wa Arusha.
*************************
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi William Lukuvi amaliza rasmi
ulaji uliokuwa unafanywa na baadhi ya maafisa ardhi wa jiji la Arusha.
Waziri
Lukuvi amesema hayo mkoani Arusha tarehe 8/3/2020 wakati wa ziara yake
ya kuanzisha rasmi ofisi za ardhi za mikoa na kuvunja ofisi za kanda
ambazo zilikuwa zinahudumia zaidi ya mkoa mmoja, hali iliyokuwa
inawasababishia wananchi usumbufu.
Akizungumza
na viongozi wa mkoa huo wakati akianzisha rasmi ofisi mpya ya kanda ya
mkoa wa Arusha amesema kuanzia sasa ulaji uliokuwa unafanyika na baadhi
ya maafisa aridhi wa jiji kwa kudai posho za kwenda kufuatilia hati mkoa
wa kilimanjaro ameaumaliza rasmi.
Ameongeza
kuwa Huduma zote za utoaji hati, uandaaji wa michoro ya mipango miji,
pamoja na huduma za Msajili wa Hati zitatolewa Katika Jiji la Arusha na
sio katika makao makuu ya kanda Moshi kama ilivyokuwa hapo awali.
Hadi
sasa Waziri Lukuvi ameishafungua ofisi za ardhi ngazi ya mkoa katika
mikoa ya Singida, Tabora, Geita, Mara na Arusha na kazi inaendelea
katika mikoa mingine yote nchini ambapo huduma zote za uandaaji na
utoaji hati kuanzia sasa zinafanyika mkoani.
Hatua
hii ya kuanzisha ofisi za ardhi ngazi ya mkoa imekuja ili kupunguza
kero za wananchi kufuata huduma hiyo Wizarani au katika Makao makuu ya
Ofisi za Kanda za mikoa mitatumitatu.
No comments :
Post a Comment