Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
Meneja
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga Specioza Owure akiwa
kwenye picha ya pamoja na watumishi wa mamlaka hiyo wakati wa
maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
NA MWANDISHI WETU,TANGA
NA MWANDISHI WETU,TANGA
WANAWAKE Mkoani Tanga wametakiwa
kuchangimkia fursa ya kauli mbiu ya awamu ya
tano kuelekea uchumi wa
viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo na vikubwa ili kuweza
kujikwamua kiuchumi wao na jamii zinazowazunguka.
Hayo yalisemwa leo na Meneja wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Tanga Specioza Owure wakati wa
maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye
viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga.
Alisema wakina mama wasilaze damu
kwa kuhakikisha wanachangamkia fursa ikiwemo kujiunga kwenye vikundi na
kuanzisha viwanda ambavyo vitakuwa chachu kubwa ya kufikia mafanikio na
kuweza kuwainua kiuchumi.
“Wakina mama tunaweza kufanya
hivyo kwani tuna vikundi vidogo vidogo tunavyoweza kujipatia fedha
ikiwemo vikoba tutumie fursa hiyo kwa kuunganisha nguvu za pamoja
kufikia malengo yetu”Alisema Meneja huyo.
“Lakini pia tuhakikishe wanawake
tunalipa kodi kwa hiari kwani ndio jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi
yetu pia tujikite kwenye ujasiriamali ambao utakuwa chachu kubwa
“Alisema
Aidha alisema kwamba pia
wakinamama wajikite kufungua viwanda kikubwa na vidogo ili kuweza
kuwasaidia na kutoa ajira na hivyo kuepukana na kuwa tegemezi kwa
wanaume ili uchumi wa viwanda usiwapite.
“Leo ni siku ya wanawake duniani
wanawake ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya Taifa lolote lile sisi TRA
tumeungana na wanawake wenzetu lakini pia niwahimize mlipe kodi kwa
maendeleo ya Taifa letu”Alisema
Hata hivyo alisema katika jamii
watu wanaoingaika na mambo ya kiuchumi ni wanawake kuanzia ngazi ya
familia mpaka maofisini hivyo wakina mama wanamcvhango mkubwa kwa
maendeleo.
“Kwenye familia mwanamke ndio
Waziri wa fedha na mipango, mama kama nguzo ya familia kutengewa siku
yake ni jambo muhimu sana anayefahamu vizuri umuhimu wa mama ni yule
ambayo mama yake ameshamtoka”Alisema
Meneja huyo alisema jamii nzima
inatambua juhudi kubwa ambazo wakina mama wanafanya na sapoti
wanazofanya wakina mama ambao unaweza kuwafananisha na majembe. “Pia
wakina mama wanahainagika, wakina mama ni walipa kodi wazuri
wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa,wakina mama wajikite kwenye
shughuli za kujenga uchumi wa nchi kwa kulipa kodi kwa hiari na wakati.
No comments :
Post a Comment