Friday, March 6, 2020

Wanawake kata ya Moshono watoa msaada kwa watoto yatima kuadhimisha siku ya wanawake duniani.


Katikati ni Diwani mstaafu wa viti maalumu kata ya Moshono,Veronica Mwilange akikabithi msaada kwa mama mwenye uhitaji anayetokea katika Kaya maskini katika kata ya Moshono mkoani Arusha (Happy Lazaro)
Afisa maendeleo kata ya Moshono Salome Njau akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu kata ya Moshono (Happy Lazaro)
Baadhi ya vitu vilivyotolewa katika kituo cha watoto yatima katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani inayofanyika kesho.(Happy Lazaro).
*******************************
Happy Lazaro ,Arusha
Wakati kilele cha maadhimisho ya siku ya Mwanamke duniani ikitarajiwa kufanyika Machi 8 ya kila mwaka ,wanawake wa kata ya Moshono katika halmashaurinya jiji la Arusha,wameyatumia maadhimisho hayo kutoa misaada Mbalimbali kwa watoto yatima katika kituo cha Bethlehem kilichopo katika kata hiyo.
Akiongea mara baada ya kukabidhi msaada huo uliotolewa na wanawake wa kata hiyo ikiwemo vyakula,sabuni na Nguo ,mwenyekiti wa UWT ,CCM wilaya ya Arusha,Mary Kisaka amewapongeza wanawake hao kwa kutumia maadhimisho hayo kuwakumbuka watoto yatima.
Aidha amewataka wanawake kuondoa woga na kujiamini ili waweze kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi nchini kuweza kufikia adhimio la Beijing la kufikia hamsini kwa hamsini.
Baadhi ya washiriki katika hafla hiyo,akiwemo diwani wa viti maalumu aliyejihudhulu ,Veronica Mwelange ,alisema lengo la kutoa Msaada huo katika kituo cha watoto yatima ni kuonyesha upendo kwa watoto hao na wao kama wazazi wameonelea umuhimu wa kuwatembea watoto hao na kula hao chakula cha mchana kama sehemu ya maadgimisho ya siku ya mwanamke.
Wengine walioshiriki  maadhimisho hayo ni pamoja na  afisa maendeleo ya jamii kata ya Moshono ,Salome Njau ambaye amesema akina mama kutoka mitaa tisa katika kata ya Moshono waliweza kuchangishana na kufanikiwa kupata kilo 100 za mchele,sabuni ,Unga wa ngano na vinywaji mbalimbali na kutoa msaada katika kituo hicho cha watoto yatima.
Kilele cha aadhimisho ya siku ya mwanamke duniani kinatarajia kuadhimishwa Siku ya jumapili Machi 8 ya kila mwaka ambapo kauli mbiu ni kizazi cha usawa kwa maendeleo ya Tanzania ya sasa na baadae huku ikielezwa kwamba kiwango cha wanawake kushika nyadhifa mbalimbali hapa nchini kikipanda.

No comments :

Post a Comment