Monday, March 9, 2020

WAFANYAKAZI WANAWAKE TCRA KANDA YA KASKAZINI WATEMBELEA SHULE YA WERUWERU NA KUTOA ELIMU.

Wafanyakazi na wake wa wafanyakazi wa TCRA katika picha ya pamoja walipokwenda kutoa elimu ya matumizi bora ya mtandao Weruweru
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Weruweru wakiwa katika picha za pamoja  
Eng. Emelda wakati akiwasilisha mada ya matumizi bora ya mitandao kwa wanafunzi wa Sekondari Weruweru
Eng. Emelda Salum akiongea na wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya weruweru iliyopo mkoa wa Kilimanjaro
Na Vero Ignatus, Arusha
Katika kusheherekea siku ya wanawake duniani 8/3/2020 wanawake wanaofanyakazi ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Kanda ya Kaskazini wameamua kutumia maadhimisho hayo kutoa elimu ya matumizi bora ya mitandao ya kijamii kwa wanafunzi wa shule ya wasichana Weruweru iliyopo mkoani Kilimanjaro.
 Akizungumza na wasichana hao wa kidato cha tano na sita mkuu wa kanda wa Taasisi hiyo Eng. Emelda Salum alisema lengo la kutoa elimu hiyo ni kuwaelimisha wasichana ambao wako mbioni kumaliza masomo na watakapo anza kutumia mitandao ya kijamii kwamba watumie kwa ufasaha kwani wao ndio waathirika wakubwa wa madhila ya mitandaoni.
 "Tumeona tuwape wasichana zawadi itakayo wasaidia kwenye maisha yao ya kesho watakapoanza kutumia mitandao kwa kuwafundisha juu ya sheria ya makosa ya mitandao na matendo yatakayo washushia hadhi au hata kushindwa kuajirika" alisema Eng. Emelda. 
 Aliongeza kuwa kampuni nyingi hivi sasa mbali na kuangalia ufaulu wa kwenye vyeti ili wakuajiri wanaenda mbali zaidi kuangalia hata kwenye account za mitandao ya kijamii namna mhusika anavyo itumia na kwamba kwa wanafunzi hao ambao mbioni wanakwenda kumaliza shule ni vyema wasiingie kwenye mkumbo huo. 
 Anzirani Ibrahim mwanafunzi wa kidati cha tano (EGM), mara baada ya kupata somo hilo alisema kuna vijana wanaoathirika na madhila ya mitandaoni kwa kutokujua hivyo kwa upanda wao wanaona ni nafasi ya kipekee kupata elimu hiyo.
 Naye dada mkuu wa shule hiyo Irene Siami kidato cha sita (PCB) maarufu kama President aliahidi kutokuwa wachoyo wa kuelimisha wengine juu ya matumizi bora ya mitandano.
 Mkuu wa shule hiyo Mwl. Rosalia Frimin aliwapongeza TCRA kwa kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi wapatao 750 wa kidato cha tano na sita, mbali na Computer 10 pamoja na mtambo wa Internet waliopewa hivi karibuni.

No comments :

Post a Comment