Tuesday, March 31, 2020

TUME YA UMWAGILIAJI NCHINI KUJIKITA KATIKA MIRADI MICHACHE ITAKAYO LETA TIJA KWA WAKULIMA



……………………………………………………………………………………………
Na Bashiri Salum,Wizara ya Kilimo
Morogoro
Tume ya Umwagiliaji nchini imetakiwa kujikita  katika miradi michache itakayo kamilika na
kuleta tija kwa wakulima  kuliko kuwa na miradi mingi isiyokamilika. 
Katika kipindi cha miaka  mitano kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020 mkoa  wa Morogoro imekuwepo miradi saba inayotekelezwa katika wilaya  Zaidi ya 11 ambapo mingi haijakamilika kutokana na changamoto mbalimbali.
Akiongea na wahandisi wa Tume hiyo  katika ofisi ya kanda iliyoko Morogoro Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya ameishauri Tume hiyo kuwa na miradi michache ambayo itakamilika kwa ufanisi mkubwa. 
Amesema Tume ya Umwagiliaji  kwa sasa ina deni kubwa kwa wakulima na wananchi  kwa ujumla ambao wamepoteza Imani na tume hiyo.
“Fanye kila litakalowapendeza mhakikishe mnarudisha Imani kwa wananchi na Raisi wa Jamhuri ya muunganoo wa Tanznania Mhe. Dkt John pombe magufuli” alisema Bw. Kusaya.
Akitolea mfano wa skimu za umwagiliaji za Kilangali, Msola Ujamaa  na Kigugu amesema matatizo ya skimu hizi yametokana na usimamizi usioridhisha na kutochukuwa hatua kwa wakandarasi hivyo kusababisha wakulima kushindwa kufikia malengo yao.
Aidha Katibu Mkuu amewataka wahandisi hao kufanya kazi kwa  ushirikiano na kujiamini wakati wakitambua kuwa Tume inamchango mkubwa katika kubadilisha Maisha ya wakulima na taifa kwa ujumla.
Hata hivyo Bw. Kusaya ameitaka tume kuyatangaza mambo mazuri wanayoyafanya  kupitia vyombo vya Habari ili wadau waweze kuifahamu tumena kwa kuwa mambo mengi yanatokana na kutokuwa na taarifa sahihi.
Awali akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu na viongozi wengine walioambatana nao Kaimu Mhandisi umwagiliaji mkoa wa Morogoro Njanji Mlwale amesema changamoto ya ukosefu wa fedha kulingana na mahitaji umechangia kwa kiasi kikubwa miradi mingi kuto kamilika.
Mhandisi Njanji amebainisha kwamba umekuwepo mgongano wa utekelezaji wa majukumu baina ya Tume na wataalamu walioko chini ya wakurugenzi watendaji wa Halmashauri mabalimbali ambao wanatekeleza shughuli za umwagiliaji kama ilivyo Tume.
Muingiliano huo wa majukumu umekuwa ukisababisha  miradi mingi ya Halmashauri kutokamilika na lwama kurudi kwa Tume ya Taifa ya umwagiliaji alisema Mhandisi.
Hata hivyo Mhandisi Njanji  amebainisha kwamba ukosefu wa maabara ya Tume ambayo ingesaidia katika vipimo mbalimbali imesababisha uchelewashaji wa miradi kwa kuwa  Pamoja na kugharimu fedha nyingi lakini sampuli zimekuwa zikichelewa .

No comments :

Post a Comment