Tuesday, March 31, 2020

KATIBU MKUU CHAMA CHA CUF AFARIKI DUNIA


Kwa masikitiko na huzuni kubwa nawatangazia wanachama wote wa CUF-Chama Cha Wananchi na Umma wa Watanzania kifo Cha Katibu Mkuu wa Chama Mhe. Khalifa Suleyman Khalifa kilichotokea usiku huu.
Marehemu Khalifa amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya Aga Khan alipokuwa akipatiwa
matibabu kutokana na Matatizo ya ini.
Kwa hakika Chama kimepata pigo kubwa na kwa yakini marehemu ameacha pengo ambalo haliwezi kuzibika kirahisi.
CUF-Chama Cha Wananchi kinatoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu na jamaa wote walioguswa na Msiba huu mzito na tunamuomba Allah awape Subira na Uvumilivu katika wakati huu mgumu. Allah aiweke Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi. Aamiyn.
Tutafahamishana rasmi juu ya ratiba ya maziko kadri tutakavyopata taarifa kutoka kwa familia ya marehemu.
Hakika sisi ni wa Allah na kwa Hakika Sote kwake tunarejea!
Prof. Ibrahim H. Lipumba
Mwenyekiti Taifa
CUF- Chama Cha Wananchi

No comments :

Post a Comment