……………………………………………………………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU
TAASISI ya Saratani ya Ocean
Road(ORCI) imeanzisha huduma mpya ya kibingwa ya kutibu ugonjwa wa
saratani kwa miale ya mionzi kwa njia ya kisasa zaidi ijulikanayo kama
Intensity Modulated Radiation Therapy (IMRT), ambapo tiba yake ni ya
mionzi ikiwa inatibu eneo
mahususi yenye tatizo pekee.
Tanzania inakuwa ya kwanza kutumia
huduma hiyo ya IMRT kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki huku kwa Afrika
inaingia kuwa nchi ya tatu baada ya Afrika Kusini na Misri.
Kwa mataifa mengine huduma hiyo inatolewa kwa nchi za Marekani na India pamoja na baadhi ya nchi ya za Ulaya.
Akizungumza na waandishi wa
Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk. Julius Mwaiselage, alisema kwa
sasa wagonjwa waliokuwa wakienda kutibiwa Nchini India watakaporejea
wataweza kutibiwa hapahapa kwa sasa kwani tayari wamenzisha huduma hiyo.
‘Huduma hii awali ilikuwa
inapatikana nje ya nchi haswa nchi zilizoendelea ikiwe, India. Hivyo
hata wagonjwa watakaporejea hapa nchini wataweza kupata tiba hii hapa
hapa na wakaendelea na matibabu.
“Awali tulikuwa tunatoa tiba ya
teknolojia ya 3D ambapo kwa sasa tumeziongezea uwezo yaani kuzimobireti
na kuja na huduma hii mpya kwa kutumia mashine hizi hizi za ‘LINAC
ACCELERATOR.’ Alisema Mwaiselage.
Dk. Mwaiselage amesema mashine
hizo zimenunuliwa kwa fedha za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na
Dk. John Pombe Joseph Magufuli zikiwa mpya kabisa kutoka kiwandani kwa
TSh. bilioni 9.5 zikiwa mbili ya mionzi na ya kupanga tiba, mwaka 2018
na kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan mwaka 2019
ambapo imekuwa na uwezo wa kutoa tiba mbalimbali za mionzi ikiwemo
teknolojia ya 3D na zingine zikiwemo ya tiba ya upasuaji wa mionzi na
zinginezo.
‘Toka zimefka hizi mashine
tulianza na hii ya mionzi kwa teknolojia ya 3D, lakini kwa sasa mashine
hizi tumezi ongezea uwezo ‘upgrade’ na kuanza kutumia tiba hiyo ya
kisasa zaidi ya IRMT ambayo kwa sasa inatumika Duniani kote ikiwemo
Afrika Kusini, Lakini India na Marekani.
Tiba hii ni mahususi kabisa kwa
kutibu maeneo yale ambayo ungeona hauitaji kufikiwa n miale ya mionzi
mikali kwenye eneo ambalo usingetaka iguswe.
Kwa upande wake Daktari bingwa wa
Saratani wa ORCI, Dk.Sekondari Muya alisema kuwa tiba hii mpya ni maalum
ambapo itasaidia kuzuia mionzi mikali kuzuiwa isipenye maeneo mengine
isidhurike.
‘Huduma hii inasaidia kutibu eneo
lenye saratani kwa miale yake ya mionzi kuenda kutibu eneo lile pekee
lenye tatizo. Mfano uvimbe wa saratani ukiwa eneo la kichwa basi tiba
hii mionzi yake itaenda kutibu tu eneo hilo na sehemu za ubongo
hazitaguswa.
Hii ndio faida kuu ya tiba hii na ni ya kipekee sana ambapo inachukua dakika kuanzia 10 hadi 30.’ Alisema Dk. Muya.
No comments :
Post a Comment