Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto Dkt. Riziki
Kisongo akisema jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kuu.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga
kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi akisema jambo kwa wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na
Kifua Kikuu (hawapo kwenye picha) mara baada ya kufanya ziara katika
Hospitali ya Rufaa ya Magonjwa Ambukizi (Kibong’oto)
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Mhe.
Oscar Mukasa akisema jambo kwa wajumbe wa kamati na wataalam katika
kikao mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Magonjwa Ambukizi
ya Kibkng’oto. Aliye upande wa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo
Buselu.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Dkt.
Mwigulu Nchemba (MB) akichangia hoja katika kikao na wataalam mara baada
ya kufanya ziara katika Hospitali ya Magonjwa Ambukizi ya Kibong’oto.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi (Kibong’oto) Dkt.
Riziki Kisongo akiwaelekeza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu namna ya kuvaa
barakoa (mask) kabla ya kuelekea kwenye wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu
sugu hospitalini hapo. Aliye upande wa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Siha,
Onesmo Buselu
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu na wataalam
wakiwa wamevalia barakoa (mask) kujilinda na maambukizi ya Kifua Kikuu
sugu kabla ya kuelekea kwenye wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu
katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ambukizi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu (kushoto)
akizungumza na watoto wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu wanaopata matibabu
katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto,
Kilimanjaro.
Mkurugenzi,wa Huduma za Kinga
kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Leonard Subi (kushoto) akiwa pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya, na Kifua Kikuu
wakizungumza na wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu katika Hospitali ya Rufaa
ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi – Kibong’oto.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu
Dkt. Jasmine Tisekwa (kulia) akizungumza na mtoto Kidawa Baraza mwenye
umri wa miaka 10 (kushoto) anayepata matibabu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu
Sugu katika Hospitali ya Kibong’oto
……………………………………………………………………………………………………
Na Englibert Kayombo WAMJW – Kilimanjaro.
Tafiti za
magonjwa ambuzuki kutoka Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa
Ambukizi (Kibong’oto) zimesaidia Shirika la Afya Duniani (W.H.O)
kubadilisha miongozo ya kutibu na
kugundua vimelea vya ugonjwa wa Kifua
Kikuu.
Kauli hiyo
imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Riziki
Kisongo wakati akiwasilisha taarifa ya Hospitali hiyo kwa wajumbe wa
Kamati ya kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya masuala
ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifuaa Kikuu.
Tuna machapisho
ya kisayansi 50 ambayo tumeyayachapisha kwenye majarida ya kimataifa,
kati ya machapisho hayo; mawili yamechangia kwenye kubadilisha miongozo
ya kutibu na kugundua vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu” amesema Dkt.
Riziki
“Mwaka 2009
ilikuwa inachukua siku 392 ili mtu kugundulika kuwa ana ugonjwa wa Kifua
Kikuu toka aende hospitali’ anasema Dkt. Riziki na kusema kuwa kupitia
watafiti waliweza kutengeneza miongozo ambayo ilitoa dira ya kuwa na
haja ya kuwa na vipimo vipya ambavyo vingepunguza muda wa kugundua
mgonjwa wa Kifua Kikuu.
“Miongozo imesaidia kuja kwa vipimo vya kisasa vya ugonjwa wa Kifua Kikuu “GeneXpert Mashines” ambazo zinachukua masaa mawili na nusu kepee kufanya vipimo vya ugonjwa wa Kifua Kikuu” Amesema Dkt. Riziki.
Andiko
lingine lililobadili tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu amesema kuwa kupitia
machapisho hayo, tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu imebadilika na sasa
wagonjwa wanatibiwa kupitia dawa na sii sindano kama ilivyokuwa awali.
“Tiba ya ugonjwa
wa Kifua Kikuu ilikuwa ni kwa njia ya sindano kwa muda wa miezi nane,
utafiti ulivyofanyika hapa ilionekana asilimia 47 ya wagonjwa walikuwa
wanapata matatizo ya usikivu” anasema Dkt. Riziki na kuendelea kusema
kuwa kwa kuchapisha maandiko hayo yalisaidia kubadili tiba ya ugonjwa
huo ambapo hadi hivi sasa tiba inatolewa kwa vidonge.
Naye Mkurugenzi
wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amesema kuwa Tanzania ni mojawapo ya
nchi inayofanya vizuri kwenye matibabu ya TB ambapo hadi hivi sasa ina
vituo 145 vya matibabu ya Kifua Kikuu sugu nchi nzima, tofauti na awali
ambapo ilikuwa na Hospitali ya Kibong’oto pekee.
“Lengo la kuwa na
Hospitali ya Kibong’oto sio kwa ajili ya kutoa tiba pekee bali
wanatakiwa kubobea kwenye tafiti, tiba na matokeo chanya kwa Taifa na
Dunia kwa ujumla” amesema Dkt. Subi na kuendelea kusema kuwa Wizara ya
Afya imeongezewa uwezo Hospitali hiyo wa kushughulikia magonjwa yote
ambukizi, tafiti na ufuatiliaji.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na
Kifua Kikuu Mhe. Oscar Mukasa amefurahi kusikia Hospitali hiyo inatoa
mchango wa mabadiliko ya sera za matibabu ya magonjwa kutokea Tanzania
na kuwasihi waongeze juhudi zaidi na kuja na tafiti nyingi zaidi
zitakazo saidia katika kupata tiba ya ugonjwa huo ambao bado ni tatizo
kubwa kwa Watanzania.
No comments :
Post a Comment