Kaimu Meneja wa Kampuni ya Ranchi
zaTaifa Bw.Masele Shilagi akiwa ofisi ya meneja wa ranchi ya
Kongwa,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa zoezi la
uchanjaji mifugo katika ranchi za NARCO zote zinazonguka ranchi ya
Kongwa,jijini Dodoma.
Afisa Mifugo Msaidizi Mwandamizi
Idara ya uzalishaji na Masoko kutoka wizara ya mifugo na Uvuvi
Bw.Charles Lugamara,akizungumzia mikakati ya wizara hiyo katika
uzalishaji wa mifuko.
Kaimu Meneja wa Kampuni ya Ranchi
zaTaifa Bw.Masele Shilagi mwenye tai akizungumza na Mwenyekiti wa Umoja
wa wafugaji waliokodishwa vitalu 28 vya Ranchi ya Kongwa Bw.Ngonyani
Uledi,alipowasili kwenye eneo la liliandaliwa kuchanja mifugo ya
wafugaji katika kijiji cha Maucha wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma.
Baadhi ya wafugaji wakiwa kwenye
eneo la liliandaliwa kwa ajili ya kuchanja mifugoi katika kijiji cha
Maucha wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma.
Kaimu Meneja wa Kampuni ya Ranchi
za Taifa Bw.Masele Shilagi akichanja ng’ombe wa Umoja wa wafugaji
waliokodishwa vitalu vya ranchi katika kijiji cha Maucha,kilichopo
wilaya ya Kongwa ,jijini Dodoma kama ishara ya uzinduzi wa zoezi la
uchanjaji mifugo katika Ranchi zote nchini.
Baadhi ya ng’ombe walioletwa na
wafugaji kwa ajili ya kupata chanjo kijiji cha Maucha waliokodishwa
vitalu 28 katika ranchi ya Kongwa.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
………………………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Jumla ya ng’ombe
24,999 katika vitalu vya Ranchi ya Kongwa mkoani Dodoma wamepatiwa
chanjo kwa ajili ya kukabiliana na
homa ya mapafu na mapele ngozi.
Hayo yameelezwa
jana na Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi ya Taifa(NARCO), Masele
Mipawa, katika zoezi la utoaji chanjo ya mifugo kwa wafugaji
wanaozunguka Ranchi hiyo.
Amesema Ranchi ya
Kongwa ina ukubwa wa hekta 38,000 ambapo hekta 12076.6 limetengwa
vitalu kwa ajili ya wafugaji wanaozunguka ranchi hiyo.
Amesema katika
kutekeleza mpango wa uthibiti wa magonjwa na kuwa eneo huru, Ranchi hiyo
ilianza kuchanja mifugo ya wananchi kulingana na kalenda ya chanjo.
“Tumeanza zoezi
hili Februari 21, mwaka huu kwa ng’ombe ambapo wanapatiwa chanjo ya homa
ya mapele ngozi, mapafu na magonjwa mengine tupo hatua za mwisho
kukamilisha zoezi, na mwitikio ni mzuri,”amesema.
Kwa upande
wake, Ofisa Mifugo Msaidizi Mwandamizi wa Idara ya Uzalishaji na Masoko
kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Charles Lugamara, amesema ulaji wa
mazao ya mifugo kwa watanzania ni hafifu ambapo kwasasa mtu mzima
anakula nyama kilo 15 kwa mwaka.
Amesema Kwa mujibu wa kiwango kilichowekwa na Shirika la Chakula Duniani, mtu mmoja anatakiwa kula kilo 50 za nyama kwa mwaka.
Amebainisha ulaji wa nyama bado upo chini licha ya Tanzania kuwa na mifugo mingi zaidi ya Milioni 32.
“Licha ya kuwa na
mifugo mingi, tija ya mazao ya mifugo bado ni ndogo, ndio maana wizara
ina mikakati mingi ya kuboresha sekta ya mifugo ili mazao yanayozalishwa
yawe ni bora,”amesema.
Ametaja miongoni
mwa mikakati ambayo ipo mbioni kutekelezwa ni uzalishaji nyama kwa ajili
ya soko la nje ambao unalenga kutatua kero zinazowakabili wazalishaji
ili kuzalisha nyama bora kukidhi mahitaji ya ndani na nje.
Ofisa huyo
amesema kupitia NARCO, wizara imejipanga wafugaji waliopewa vitalu
watazingatia misingi ya uzalishaji kwa kuzalisha nyama itakayokidhi
ubora na uchanjaji mifugo.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa
wafugaji waliokodishwa vitalu 28 vya Ranchi ya Kongwa Bw.Ngonyani
Uledi,amesema kuwa wanatarajia kuchanja mifugo yote iliyopo ndani ya
ranchi hiyo na ile ambayo iko jirani lengo kubwa ni kudhibiti magonjwa
hatari ya mifugo.
Bw.Masele ametoa rai kwa wananchi
waliokodishwa vitalu vya kufugia kuhakikisha wanachanja mifugo yao na
wafugaji watakao kaidi watachukuliwa hatua kali za kisheria.
No comments :
Post a Comment