Thursday, March 5, 2020

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AKABIDHI VITI VYA MWENDO (WHEELCHAIRS) KWA WABUNGE KWA AJILI YA WATOTO WENYE ULEMAVU



Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea shukurani za bila kushikana mikono na Mbunge wa Kilombero (kupitia tiketi ya CHADEMA) Mhe. Peter Ambrose Paciens Lijualikali baada ya kumkabidhi viti mwendo (Wheelchairs) 10 kwa ajili ya watoto wenye Ulemavu wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2020. Wanaoshuhudia ni Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Mke wa Balozi wa Tanzania nchini Israel Mama Joan Masima.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa ameketi na  Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu (watu wenye ulemavu) Mhe. Stella Alex Ikupa, Mke wa Balozi wa Tanzania nchini Israel Mama Joan Masima na mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sofia Mjema katika picha ya pamoja na wabunge na wawakilishi wa wabunge baada ya kuwakabidhi viti mwendo (Wheelchairs)
210 kwa  ajili ya watoto wenye Ulemavu wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2020. Wanaoshuhudia ni
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na  Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, baada ya kuwakabidhi wabunge viti mwendo (Wheelchairs) 210 kwa ajili ya watoto wenye Ulemavu wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2020.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na  Mama Ulega, mke wa Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe, Abdallah Ulega baada ya kuwakabidhi wabunge viti mwendo (Wheelchairs) 210 kwa ajili ya watoto wenye Ulemavu wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2020. (kushoto ni Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (watu wenye ulemavu) Mhe. Stella Alex Ikupa
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (watu wenye ulemavu) Mhe. Stella Alex Ikupa  baada ya kuwakabidhi wabunge viti mwendo (Wheelchairs) 210 kwa ajili ya watoto wenye Ulemavu wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2020. (katikakati) ni Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na 
PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………….
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia
Ackson amemshukuru Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa
kuendelea
kuwasaidia wananchi wenye Uhitaji, wakiwemo watoto wenye ulemavu na
Wazee akitaja kitendo hicho kuwa ni cha kizalendo na chenye kutia
moyo.
Mhe. Tulia ametasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya Mama Magufuli
kukabidhi viti mwendo (Wheelchairs) vipatavyo 210 kwa baadhi
Waheshimiwa Wabunge kwa ajili
ya kuwagawia watoto wenye uhitaji majimboni kwao iliyofanyika Ikulu
jijini Dar es salaam.
Naibu Spika  amesema kwamba katika  kuwasaidia wazee na watoto wenye
ulemavu  Mama Magufuli  amekuwa mfano wa kuigwa kwa wanawake kwa
kuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii ya watu wenye mahitaji.
Mama Magufuli, ambaye ametoa msaada wa viti mwendo kwa watoto wenye
ulemavu siku chache kabla ya Siku ya Wanawake Duniani,
amewashukuru Waheshimiwa Wabunge walioitikia mwito wake kupokea msaada huo.
“Kama mjuavyo kila tarehe 08/03 ya Kila mwaka ni Siku ya Wanawake
Duniani. hivyo basi nikiwa miongoni mwa wanawake nimeguswa na
kuamua kusherehekea siku hii muhimu kwetu kwa kutoa zawadi ndogo ya
viti mwendo kwa waheshimiwa wabunge ili wawafikishie
wanangu wenye uhitaji kwenye majimbo yao kwa urahisi zaidi, kwani wao
ndio wawakilishi wa wananchi”, alisema Mama Magufuli.

No comments :

Post a Comment