Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akizungumza na Waandishi wa habari(hawapo pichani)
Ofisini kwake Mjini Bariadi, kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wanawake
Duniani Kitaifa yanayofanyika Mkoani Simiyu pamoja Ziara ya Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
……………………………………………………………………………………………
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa
kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake
Duniani ambayo Kitaifa yatafanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji
wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari ofisini kwake Mjini Bariadi Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka amesema Maadhimisho haya yanaongozwa na kauli Mbiu
“Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na ya baadaye”
ambapo yataanza tarehe 02 Machi 2020 mpaka tarehe 08 Machi 2020.
“Katika
Maadhimisho haya tunawatarajia wageni mbalimbali na shughuli mbalimbali
kufanyika; mathalani kuanzia Tarehe 02 Machi 2020 maonesho ya shughuli
mbalimbali zinazofanywa na Wanawake zitaoneshwa, wajasiriamali kutoka
maeneo yote nchini wamethibitisha kushiriki pia kutakuwa na upimaji kwa
magonjwa mbalimbali ya Wanawake,”
“Siku ya tarehe
06 Machi 2020 kutakuwa na Jioni ya mwanamke ambapo wake za Viongozi
waliopo madarakani na wastaafu na Watendaji mbalimbali wa Taasisi
watashiriki; mpaka sasa Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya nne,
Mama Tunu Pinda, Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania na viongozi
mbalimbali Wanawake wamethibitisha kushiriki, wakiongozwa na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu,”
alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka
ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu kushiriki katika shughuli
zote zitakazofanyika katika Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake
Duniani Kitaifa na kilele chake ambazo zitafanyika katika Uwanja wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Katika hatua
nyingine Mtaka amesema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku tatu
Mkoani Simiyu kuanzia tarehe 06 Machi 2020 hadi 08 Machi 2020.
Amesema tarehe 06
Machi, 2020 Mhe. Makamu wa Rais atafungua Tawi la Benki ya NMB katika
Kata ya Nyashimo makao Makuu ya Wilaya ya Busega na baadaye kuweka Jiwe
la Msingi Ujenzi wa Tawi la Chuo cha Usimamizi (IFM), katika Kata ya
Sapiwi wilayani Bariadi.
Ameongeza kuwa
tarehe 07 Machi, 2020 Mhe. Makamu wa Rais atafungua Ofisi ya Kampuni ya
Simu Tanzania (TTCL) ya Mkoa na siku hiyo hiyo ataweka jiwe la msingi
Ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichopo
Kata ya Somanda.
“Nitumie nafasi
kuwaomba Wananchi wa Mkoa wa Simiyu hususani katika maeneo yote ambayo
Mhe. Makamu wa Rais atapita kujitokeza kwa wingi kumsikiliza kwa kuwa
katika maeneo yote ambayo Mhe. Makamu wa Rais atafungua na kuweka mawe
ya msingi miradi, atazungumza na wananchi, ” alisema Mtaka.
Mhe. Makamu wa
Rais atahitimisha ziara yake Mkoani Simiyu tarehe 08 Machi kwa
kuwaongoza wananchi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake
Duniani Kitaifa.
No comments :
Post a Comment