…………………………………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema Serikali imesitisha uchumbaji wa madini ya
boxite katika mlima wa Magamba wilayani Lushoto baada ya wananchi
kuulalamikia mradi huo unasababisha uharibifu wa mazingira.
Hivyo, Waziri
Mkuu amewaagiza viongozi wa Serikali wahakikishe wanaimarisha ulinzi
katika eneo hilo mtu yeyote asiendeshe shughuli za uchumbaji wa madini
hata Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) nao wasichimbe eneo hilo.
Waziri Mkuu
ameyasema hayo leo(Alhamisi, Machi 5, 2020) baada ya kutembelea eneo
hilo na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
katika uwanja wa shule ya msingi Mabughai kata ya Magamba wilayani
Lushoto, Tanga.
Amesema alipokea
taarifa kwamba yapo malalamiko kuhusu shughuli za uchimbaji wa madini
zinazoendelea kwenye mgodi huo kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,
Benjamin Mkapa pamoja na mbunge wa Lushoto, Shabn Shekilindi.
“Hatuwezi
kuendelea na shughuli za uchumbaji wa madini kwenye eneo hili wakati
wananchi wanalalamikia uharibifu wa mazingira unaosababisha na shughuli
hii. Serikali yenu ni sikivu hivyo nawaomba muendelee kuiamini na
kushirikiana nayo.”
Kadhalika, Waziri
Mkuu ameagiza watu wote waliopewa leseni za kuchimba madini katika eneo
hilo wazirudishe Serikalini na amemuelekeza Waziri wa Madini, Doto
Biteko asimamie zoezi hilo.
Kwa upande wake,
Mbunge wa Lushoto amesema wananchi hawataki shughuli za uchimbaji wa
madini ya boxite ziendelee kufanyika kwenye mlima Magamba kwa ajili ya
kuzuia uharibifu wa mazingira.
Amesema katika
mlima huo ndiko kwenye chanzo cha maji kinachotegemewa na wananchi pia
mlima huo umezungukwa na miundombinu mbalimbali ya shughuli za kijamii,
hivyo kuendelea kwa uchimbaji wa madini kutasababisha athari kubwa
ikiwemo ukosefu wa maji.
Awali,Waziri wa
Madini, Doto Biteko amesema eneo hilo la Magamba lina leseni 22 za
uchimbani lakini kutokana na mvutano wa wenye leseni na wananchi, wizara
iliamua kusitisha shughuli za uchimbaji hadi watakapokubaliana.
Baada ya
kuzungumza na wananchi, Waziri Mkuu alimtembelea Bi Miriam Shemndolwa
ambaye ni mlemavu mkazi wa Mombo aliyemfahamu kupitia TBC alipohojiwa na
Mtangazaji wa Kipindi cha Wape Nafasi, Tuma Dandi.
Apohojiwa katika
kipindi hicho Bi Miriam aliomba msaada kutoka kwa watu mbalimbali
wakiwemo viongozi ambapo alimtaja Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu
ametoa msaada wa sh. milioni tano ili pamoja na michango mingine
zimuwezesha kujenga nyumba ya kuishi yeye na bibi yake Eonica Hiza
ambaye ndiye anayemlea. Kwa sasa Miriam na mlezi wake wanaishi kwenye
nyumba ya mjomba wake.
No comments :
Post a Comment