Waziri wa Nishati Dkt Medadi
Kalemani akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kikao na kamati ya
Bunge ya Bajeti Mokoani Morogoro Leo March 6,2020.
………………………………………………………………………………………………………….
Na Farida Said, Morogoro
Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepewa wasilisho juu ya
maendeleo ya utekelezaji mradi Julius Nyerere (Mw 2115).
Wasilisho hilo limetolewa Mkoani
Morogoro kwenye ukumbi wa bwalo la JKT Umwema na
kuhudhuriwa na Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi
Zena Saidi, Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO.
Akizungumza baada ya wasilisho
hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Mashauri
Ndaki alisema malengo ya kukutana leo na Wizara pamoja na TANESCO
yalikuwa matatu.
Aliyataja malengo hayo kuwa ni
kupata maelezo kutoka kwa Mhe. Waziri wa Nishati juu ya utekelezaji wa
mradi wa Julius Nyerere tangu umeanza na hatua iliyofikia pamoja na
kutembelea na kuona utkelezaji wa mradi.
“Tumejifunza kwamba mradi
unaendelea vizuri na kwa kasi, kwa kazi zilizokuwa zimepangwa mpaka
wakati huu zimefanyika kama zilivyopangwa na tunatarajia mradi
utakamilika ndani ya muda uliopangwa Juni, 2022 “, alisema Mhe. Ndaki.
Aliongeza kazi ya kuchimba mtaro wa kuchepusha maji umekamilika na hatua mbalimbali zimefikiwa za ujenzi wa Bwawa.
Kwa upande wake Waziri wa Nishati
Dkt. Medard Kalemani amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa kuhakikisha fedha
zinalipwa lwa Mkandarasi kwa wakati.
Alisema Serikali ilitakiwa kulipa malipo ya awali kwa Mkandarasi aslimia 15 ambazo imeshazilipa kwa wakati.
Aliongeza Mkandarasi kila mpango kazi ambao upo kwenye mkataba wake amefikia takribani asilimia 85 za utekelezaji.
“Kazi ambazo zimekamilika Serikali
imeshalipa fedha, na kwa ujumla wake kwa sasa Serikali imeshatoa fedha
zaidi ya trilioni 1.19 na jumla ya fedha za utekelezaji ni trilioni 6.5
hadi kukamilika kwa mradi ambazo ni ufadhili wa Serikali kwa asilimia
mia moja”, alisema Dkt. Kalemani.
Aliongeza utekelezaji wa mradi
unakwenda vizuri ukiziangalia kazi kuu nne kama ujenzi wa “Power
House”ambao ulitakiwa kuanza mwaka jana mwezi wa kumi, ulianza mwezi
mmoja kabla.
Aidha kupitia utekelezaji wa mradi wa Julius Nyerere hadi sasa takribani Watanzania 3,642 wameajiriwa.
Kukamilika kwa mradi wa Julius Nyerere kutaifanya nchi kuwa na umeme mwingi, unaotabirika, imara na wa gharama nafuu.
No comments :
Post a Comment