Thursday, March 5, 2020

BENKI KUU YA TANZANIA YAJIVUNIA MAFANIKIO WALIYOFIKIA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU WALIOSOMA KWA UFADHILI WA MIFUKO YA UDHAMINI INAYOSIMAMIWA NA BENKI HIYO



 Afisa Uendeshaji wa Mifuko hiyo, Bi. Kashinje Sekule Felician, akiwasilisha mada kuhusu Mifuko hiyo Machi 5, 2020.
 Afisa Uendeshaji wa Mifuko hiyo, Bi. Kashinje Sekule Felician, akiwasilisha mada kuhusu Mifuko hiyo Machi 5, 2020.
  Kutoka kushoto kwenda kulia, Bi. Vicky Msina, Meneja Msaidizi Uhusiano na Itifaki (BoT), Bi.Kashinje Sekule Felician, Afisa Uendeshaji wa Mifuko ya Udhamini ya BoT, Bi. Zalia Mbeo, Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, Bw. Ganga Ben Mlipao, Meneja Msaidizi, Dawati la Kutatua Malalamiko ya wateja wa mabenki na taasisi za fedha, BoT na Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki, BoT Bw. Augustino Hotey, wakiwa kwenye semina hiyo.
 Bi. Zalia Mbeo, Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, akizungumza na wanasemina kuelezea malengo ya BoT kutoa elimu ya masuala ya Uchumi na Fedha kwa wanahabari
 Bi. Vicky Msina, Meneja Msaidizi Uhusiano na Itifaki BoT, akielezea uzoefu wake kwa washiriki jinsi alivyokuwa akifanya kazi za uandishi wa habari.
 Bi. Zalia Mbeo, Meneja Uhusiano na Itifaki BoT, akizungumza na wanasemina kuelezea malengo ya BoT kutoa elimu ya masuala ya Uchumi na Fedha kwa wanahabari
 Baadhi ya washiriki wa semina wakiwa kwenye semina hiyo.
  Baadhi ya washiriki wa semina wakiwa kwenye semina hiyo.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Arusha
BENKI Kuu wa Tanzania BoT imeridhishwa na mafanikio waliyofikia wananfunzi wa elimu ya juu waliosoma na wanaoendelea kusoma kupitia Mifuko ya udhamini inayosimamiwa na benki hiyo.
 Benki Kuu ya Tanzania ilianzisha Mifuko ya Gilman Rutihinda Trust Fund na Mwalimu Nyerere Memorial Trust Fund ili kutoa hamasa ya ufaulu kwa wanafunzi katika masomo ya Hidsabati na Sayansi hususan wanafunzi wa kike kwa kutoa ufadhili huo (Scholarships) ,  Afisa Uendeshaji wa Mifuko hiyo, Bi. Kashinje Sekule Felician amewaambia waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya kuwajengea uwezo wa kuandika kwa usahihi habari Uchumi na Fedha kwenye ukumbi wa BoT jijini Arusha leo Machi 5, 2020.
Amesema katika kutekeleza sera ya kuwajibika kwa jamii (Corporate Social Responsibility-CSR), Benki Kuu ya Tanzania ilianzisha mifuko hiyo ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wa Kitanzania kufanya vizuri kwenye masomo ya Hisabati na Sayansi, hususan wanafunzi wa kike.
Akiwasilisha mada kuhusu Mifuko ya udhamini inayosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania, (BoT)  Bi.Kashinje alisema, wamekuwa wakiwafuatilia wanafunzi hao na kubaini kuwa wamekuwa wakifanya vizuri kwenye masomo yao kila mwaka na wengi wao tayari wamehitimu na kuajiriwa kwenye taasisi mbalimbali ikiwemo Benki Kuu.
"Wengi wamefaulu kwenye daraja la kwanza na wachache sana daraja la pili na tayari baadhi yao wanalitumikia taifa kwenye Nyanja mbalimbali, wengine wamebaki kwenye vyuo hivyo walikosoma na kuajiriwa kama wahadhiri wasaidizi na kwa jambo hili tinafarijika sana. “ Alisema Bi. Kashinje
Akitoa historia ya mifuko hiyo na lengo la kuanzishwa kwake, Bi Kashinje alisema Mfuko wa Gilman Rutihinda Trust Fund ulianzishwa mwaka 1994 kama kumbukumbu ya aliyewahi kuwa Gavana wa BoT, Marehemu Gilman Rutihinda na Mfuko mwingine ni wa Mwalimu Nyerere Memorial Trust Fund ambao ni kumbukumbu ya Hayati Babab wa Taifa.
"Mfuko wa Gliman Rutihinda ulianza kutoa ufadhili mwaka 1995 na  unatoa ufadhili kwa wanafunzi wa Kitanzania wa Chuo Kikuu waliofaulu kwa daraja la juu kabisa kwenye masomo ya Uchumi na Fedha na wana umri usiozidi miaka 35 na wanahitaji kuchukua Shahada ya Pili.
“Njia tunayotumia kuwapata walengwa ni pamoja na matangazo kwenye radio, magazeti, televisheni na tovuti ya BoT.
Aidha Mfuko wa Mwalimu Nyerere unatoa ufaulu kwa wanafunzi waliohitimu mkidato cha sita na kupata alama za juu kabisa katika masomo ya Hisabati na Sayansi.
Alisema  mwaka 1995 Mfuko ulianza kufadhili wanafunzi wawili lakini idadi imezidi kukua na sasa kuna jumla ya wanafuzni 37 na kati ya hao 33 wamekwisha kamilisha kozi zao na wengine tayari wameajiriwa.
Aidha Mfuko wa Mwalimu Nyerere ulianza mnamo mwaka 2009 na ulianza kutoa ufadhili mwaka 2013 ambapo nia ni kuongeza hamasa na ufaulu kwa wanafunzi wa kike katika masomo ya Sayansi na Hisabati.
Aidha Shahada ya kwanza asilimia 50 ya ufadhili unaende kwa wanafunzi wa kike ambaye ni raia wa Tanzania na awe na ufaulu wa juu Daraja la Kwanza katika masomo ya Hisabati na Sayansi na awe amepata udahili kwenye vyuo vikuu vya hapa nchini.
“Utaratibu wa kuwapata wanafunzi hawa huwa tunawailiana na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) ambapo hutuchagulia wananfunzi wenye vigezo hivyo.” Alifafanua.
Ufadhili unahusisha fedha za ada, kujikimu, mafunzo kwa vitendo na computer mpakato
Hadi sasa watanzania 46 wamenufaika na kati ya hao 32 ni wanawake na 12 ni wanaume. Alisema Bi.Kashinje.

No comments :

Post a Comment