Monday, March 9, 2020

AMBO YAMCHANGIA SHILINGI 500,000/= KUONGEZA MTAJI MWANAMKE SHUJAA MWENYE ULEMAVU


Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ ya mkoani Shinyanga imemsaidia mtaji wa shilingi 500,000/= Mwanamke mwenye ulemavu Happiness Kwigema anayejishughulisha na biashara ya pipi na sabuni za kufulia Mjini Shinyanga.
 

Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga ,Tedson Ngwale akimtambulisha Bi. Happiness Kwigema (kulia), Mwanamke mwenye ulemavu Shujaa anayejituma katika kazi ambaye amekabidhiwa shilingi 500,000/= na Kampuni ya Vinywaji Jambo Food Products Ltd kwa ajili ya kuongeza mtaji wake wa kuuza pipi na sabuni za kufulia. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (katikati) akizungumza wakati wa Kukabidhi shilingi 500,000/= za mtaji zilizotolewa na Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ kwa Mwanamke mwenye ulemavu Happiness Kwigema anayejishughulisha na biashara ya pipi na sabuni za kufulia Mjini Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha shilingi 500,000/= zilizotolewa na zilizotolewa na Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ kwa ajili ya  Mwanamke mwenye ulemavu Bi.Happiness Kwigema anayejishughulisha na biashara ya pipi na sabuni za kufulia Mjini Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum.
Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum akinyoosha mkono wakati Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha shilingi 500,000/= zilizotolewa na zilizotolewa na Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ kwa ajili ya  Mwanamke mwenye ulemavu Bi.Happiness Kwigema.
Bi.Happiness Kwigema akishukuru baada ya kukabidhiwa shilingi 500,000/= zilizotolewa na Kampuni ya Jambo Food Products Limited’ ili zimsaidie kuongeza mtaji wa biashara anazofanya.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM)  pamoja na viongozi mbalimbali wakipiga picha na Bi. Happiness Kwigema.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM)  pamoja na viongozi mbalimbali wakipiga picha na Bi. Happiness Kwigema.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM)  pamoja na viongozi mbalimbali wakipiga picha na Bi. Happiness Kwigema.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM)  pamoja na viongozi mbalimbali wakipiga picha na Bi. Happiness Kwigema.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Fedha hizo Taslimu zimekabidhiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwenye Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo katika mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika katika kijiji cha Iselamagazi kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum amesema Jambo imeguswa na kujituma kwa mwanamke huyo ‘Mama Shujaa Happiness na kuamua kumpatia shilingi Laki 5 ili aongeze mtaji katika biashara anazozifanya.
 
“Happiness Kwigema ni mwanamke mwenye ulemavu lakini anajituma katika kazi,anajishughulisha na biashara ndogo ndogo ili kujipatia kipato.Kwetu tunamuona ni Mama Shujaa,tumeamua kumchangia shilingi 500,000/=”,alisema Salum.
 
Alisema katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Jambo mbali na kumchangia Bi. Happiness Kwigema pia wameshiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kuchangia katoni 20 za maji,Shilingi milioni 1 kwa ajili ya Taulo za kike kwa wanafunzi wa kike wanaotarajia kufanya mtihani wa Darasa la saba mwaka 2020.
Soma pia : MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI TAULO ZA KIKE ‘PEDI’ ZA MIL 7.8 KWA WANAFUNZI WA KIKE DARASA LA SABA 2020

“Katika kushiriki kikamilifu katika kumuenzi Mwanamke na kutambua mchango wake katika ajira, katika Kiwanda cha Jambo Food Products Ltd tunazingatia sana usawa wa kijinsia kwani mpaka sasa wastani wa ajira zetu Kiwandani ni 45% wanawake na 55% wanaume, lakini lengo letu likiwa ni kufikia 50%  kwa 50%”,alisema Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo.


 “Kwa mara ya kwanza kwa sasa kiwandani tumeajiri Machine Operators wanawake, Mafundi umeme na Mafundi magari, lakini pia kwa kuwa tuna mpango wa kufungua viwanda vingine vipya vya asali, biscuits, pipi na ice cream tutaajiri pia Engiiners wanawake. Ikumbukwe kwa miaka mingi baadhi ya kazi zilionekana kufanywa na wanaume tu kutokana na Mila na Desturi gandamizi. Ni imani yetu sura hii itatoa hamasa kubwa kwa Jamii”,aliongeza Salum.
 
Kwa Upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoa wa Shinyanga, amempongeza Bi. Happiness Kwigema kwa kujituma kufanya shughuli za kumwingizia kipato na kuwashauri wanawake wengine kuiga mfano wa Happiness kwa kufanya kazi za kuwaingizia kipato.
 
Mhe. Azza pia ameipongeza Kampuni ya Jambo kwa michango inayoendelea kuitoa katika jamii akibainisha kuwa Jambo wamekuwa wadau wazuri wa maendeleo mkoani Shinyanga.

No comments :

Post a Comment