Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe,
akimkabidhi nyundo pamoja na vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi mpya ya
Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo
(kushoto), alipokuwa akiizindua Bodi hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Postamasta
Mkuu, Hassan Mwang’ombe akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wizara hiyo (Sekta ya Mawasiliano), Kitolina Kippa akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Waziri Mhandisi Kamwelwe (katikati), akizungumza na wajumbe wa Bodi hiyo, pamoja na Menejimenti ya Shirika wakati uzinduzi huo.
Mwenyekiti
wa Bodi mpya ya Shirika la Posta (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni
Kondo (kulia), akiwa na Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe (wa pili)
pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo, wakipiga makofi wakati wa
uzinduzi huo.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Shirika la Posta wakimsikiliza Waziri alipokuwa akizungumza.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi mpya ya Shirika wakifuatilia shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika uzinduzi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizungumza wakati wa uzinduzi.
Mwenyekiti
wa Bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt.
Haruni Kondo akitoa neno la shukrani mbele ya Waziri Mhandisi Isack
Kamwelwe.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati),
katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi hiyo na Postamasta Mkuu,
Hassan Mwang’ombe (kulia) na mwakilishi wa Katibu Mkuu wizara hiyo (Sekta ya Mawasiliano), Kitolina Kippa (wa pili kulia).
Picha
ya pamoja ya Waziri Mhandisi Isack Kamwelwe na wajumbe wa bodi pamoja
na Menejimenti ya Shirika, mara baada ya kumaliza uzinduzi huo katika
ukumbi wa mikutano uliopo katika Jengo la Makao Makuu ya Bandari.
No comments :
Post a Comment