Afisa Mkuu wa Wateja Bianfsi,
Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati – Filbert Mponzi akiteta jambo na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Mhandisi
Elius Mwakalinga kwenye hafla hiyo.
Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa
na Biashara ya Serikali – Aziz Chacha akiongea kwenye Hafla
iliyowakutanisha Benki ya NMB na Wakandarasi wa Kanda ya Ziwa jijini
Mwanza. Pembeni yake ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi, Wafanyabiashara
Wadogo na wa Kati – Filbert Mponzi.

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Mhandisi Elius
Mwakalinga akitoa maelezo ya Serikali kwenye mdahalo kati ya NMB na
Wakandarasi kutoka Kanda ya Ziwa.
………………………………………………………………………………………………..
BENKI
ya NMB mwaka jana imetoa zaidi ya dhamana 500 kwa wakandarasi
wazawa ili kuwawezesha kugharimia miradi mbalimbali ya ujenzi
nchini. Mkakati huo ulifikiwa kufuatia kilio cha muda mrefu cha
wakandarasi kushindwa kushiriki katika ujenzi wa
miradi
mbalimbali kutokana na ukata wa fedha na ushindani toka kwa
makampuni ya nje.
Akiongea
wakati wa kongamano lililohudhuriwa na zaidi ya wanadarasi 300
kutoka Kanda ya Ziwa mwishoni mwa wiki, Afisa Mkuu wa Wateja
Binafsi, Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati wa NMB Filibert Mponzi
alisema zoezi hilo litakua endelevu.
Alisema
mbali na kusaidia kuwanyanyua wakandarasi wadogo kimtaji, pia
Benki hiyo imeitikia wito wa Rais John Magufuli alioutoa juu ya
taasisi mbalimbali za kibenki kuwakopesha wakandarasi kwa
masharti nafuu. “Kama benki ya biashara na kama mbia wa
serikali tumeshiriki kikamilifu kuwasaidia wakandarasi kimtaji na
pia kuitikia wito wa Rais Magufuli kuhakikisha kada hiyo
inashiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi,” alisema Mponzi.
Mkakati
wa kutoa dhamana kwa wakandarasi umesaidia sana kuwawezesha
kupata kazi za uhakika za ujenzi na kwa mujibu wa Mponzi
benki inatoa dhamana ya asilimia 50 ya thamani ya mradi husika.
Mbali na kutoa dhamana ya mikopo NMB pia itaanza kutoa
huduma ya bima kwa waka ndarasi hao kuwawezesha kushiriki kwa
ufanisi zaidi kwenye miradi mbalimbali kwa riba nafuu.
Hata
hivyo, alisema wakati benki ikibuni njia mbalimbali za
kuwasaidia wakandarasi wadogo na wazawa kuna umuhimu mkubwa kwao
kuwa waaminifu katika urejeshaji wa mi kopo na kuheshimu
masharti ya dhamana ili kuepuka kulipa riba kubwa kama adhabu
baada ya mikataba kukiukwa.
Katika
kongamano hilo lililohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eliud Mwakalinga wakandarasi
walijadili chan gamoto mbalimbali na kushauri mikakati mbalimbali
ya kupambana nazo.
Akizungumza
nao, Katibu Mkuu Mwakalinga mbali na kuishukuru NMB kwa
ubunifu na huduma za mikopo na dhamana kwa wakandarasi wazawa
alisema kazi za ujenzi zinahitaji uaminifu mkubwa na kuzi ngatia
ubora. Alisema tafiti mbalimbali zinaonesha wakandarasi wazawa
hasa wadogo wamekuwa wakishindwa kupewa kazi kubwa kwa zababu
kadhaa zikiwamo wengi kushindwa kuajiri wahandisi waliobobea na
wenye weledi usiotiliwa shaka.
“Tumefanya
utafiti na kugundu a kuna shida kubwa kwa wakandarasi wengi
wadogo kushindwa kukaa na wahandisi waliobobea kwa kukwepa
kuwalipa mishahara wanayostahili na kuishia kuajiri wahandisi
wanafunzi na hata mafundi mchundo tu,” alisema.
Mhandisi
Mwakalinga alidokeza mbinu kadhaa za kuwawezesha wakandarasi
wadogo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanashindana katika
kujenga miradi mikubwa inayoshikiriwa na makampuni mengi ya nje.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wakandarasi Mkoani Mwanza
Mhandisi Oscar Munishi aliwataka wakandarasi wazawa kujitathmini
juu ya uadilifu wao kazini na kwamba kuna mapungufu kadhaa
yanayohitaji kufanyiwa kazi miongoni mwao. Aliyashukuru mabenki
yaliyojitokeza kuwadhamini kwa mikopo ya riba nafuu na
akaishukuru NMB kwa kukutana nao na kujadili nao namna ya
kuboresha utendaji kazi na kushindana kikamilifu sokoni.
#NMBKaribuYako
No comments :
Post a Comment