Saturday, February 1, 2020

WAZIRI JAFO AZUNGUMZIA MIAKA MINNE YA UTEKELEZAJI TAMISEMI


 
WAZIRI wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,akizungumza  wakati akieleza mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijni Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akitoa neno kuhusiana na mambo yaliyofanywa na TAMISEMI katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijni Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala na Serikali za Mitaa, Mwanne Nchemba,akitoa pongezi kwa Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijni Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi.
Sehemu ya washiriki katika hafla ya mafanikio ya TAMISEMI wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,wakati akizungumzia   mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijni Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,wakati akizungumzia   mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijni Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi.
Mbunge wa Rombo (Chadema) Mhe.Joseph Selasini,akitoa pongezi kwa Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,kutokana na   mafanikio ya wizara yake aliyoyapata  katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijni Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi.
WAZIRI wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,akikata utepe kuashiria  mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijni Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi.
WAZIRI wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,akionyesha kitabu kinachoelezea  mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijni Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi.
WAZIRI wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,akimkabidhi kitabu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, kinachoelezea  mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijni Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi.
WAZIRI wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,akimkabidhi kitabu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi , kinachoelezea  mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijni Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi.
WAZIRI wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,akimkabidhi kitabu Mbunge wa Rombo (Chadema) Joseph Selasini , kinachoelezea  mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijni Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi
WAZIRI wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge walioshiriki hafla ya  mafanikio ya wizara ya TAMISEMI  katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijni Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi
WAZIRI wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mara baada ya kuzungumzia  mafanikio ya wizara ya yake katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi
WAZIRI wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara yake mara baada ya kuzungumzia mafanikio ya wizara hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali pamoja na viongozi
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
…………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imesema kuwa tatizo la usafiri kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wanaotumia
mabasi ya mwendokasi itamalizika Julai mwaka huu baada ya mzabuni mpya wa kuendesha mradi kupatikana.
Hata hivyo tatizo lililojitokeza kwa sasa  ni upungufu wa mabasi ambapo yanayofanyakazi ni 140 kati ya mabasi 305 yanayohitajika.
Kaulo hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo, wakati akizungumzia  mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli.
“Katika awamu ya kwanza ya mradi wa mabasi ya mwendokasi, tumejifunza mazuri na mabaya ambayo yametuwezesha kuja na maboresho. Awamu ya pili ya utekelezaji mradi huu, changamoto zote zitabaki kuwa historia,” amesema Jafo
Aidha amesema kuwa  kwa sasa mabasi hayo yanasafirisha abiria 300,000 kwa siku kutoka abiria 70,000 wa awali, huku mabasi yanayotumika ni 140 badala ya 305, hivyo kusababisha changamoto ya usafiri kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Jafo amesema kuwa ifikapo Julai hadi Agosti mwaka huu, changamoto hizo zitamalizika baada ya serikali kumpata mzabuni mpya atakayeendesha mradi huo.
“Awamu ya pili ya ujenzi wa miundombinu ya mradi huo kwenda Mbagala imekwisha aanza, lakini pia itafuatiwa na awamu ya tatu kwa ajili ya mabasi ya mwendokasi kuelekea Gongo la Mboto,” amesisitiza
Hata hivyo amesema kuwa kupitia mradi wa uboreshaji miundombinu Jiji la Dar es Salaam (DMDP) barabara za mitaa zinazojengwa zitakuwa kiungo muhimu na zile za mwendokasi.
Waziri amesema kuwa mradi huo unaogharimu zaidi ya sh. bilioni 600 utalifanya jiji la Dar es S alaam kuwa la kisasa zaidi baada ya uboreshaji wa miundombinu.
“Ifikapo mwaka 2020 watu walioondoka Dar es Salaam, watalazimika kupata wasaidizi kuonyeshwa mitaa kutokana na maboresho yanayoendelea kufanyika,” amesema Jafo.
Akizungumzia mafanikio hayo, Mbunge wa Rombo (Chadema) Joseph Selasini,amesema kuwa  ni mtu pekee asiyekuwa na uono wa mafanikio ndio mwenye uwezo wa kubeza maendeleo yaliyopatikana nchini.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala na Serikali za Mitaa, Mwanne Nchemba, amesema kuwa kamati yake imeridhia mafanikio yaliyopatikana kupitia TAMISEMI.

No comments :

Post a Comment