
******************************
Na Mwandishi Wetu,Monduli
Wajasiriamali wilayani Monduli
mkoani Arusha wametakiwa kuboresha vifungashio pamoja na ubora wa
bidhaa zao ili ziweze kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika Maonyesho
ya Ubunifu,Ujasiriamali na viwanda vidogo yaliyoandaliwa
na shirika
lisilokua la kiserikali la Okoa New Generation ,Afisa Mipango wa Wilaya
ya Monduli Colex Mwakyelu alisema kuwa wajasiriamali wakiboresha bidhaa
zao wanaweza kupata masoko ya nje na kuepuka utegemezi wa masoko ya
ndani.
Aliwataka wajasiriamali
kuboresha vifungashio na kuzitangaza bidhaa zao katika maonyesho makubwa
yanayofanyika ili kupata fursa za masoko na kunufaika kiuchumi.
Mkurugenzi wa shirika
lisilokua la kiserikali la Okoa new Generation ,Neema Robert amesema
kuwa maonyesho hayo yanalenga kuwapatia fursa za kimasoko pamoja na
mafunzo ya wajasiriamali ambayo wamekua wakiyatoa katika majukwaa ya
vijana yaliyoko katika wilaya hiyo.
Neema aliwataka vijana kutumia
fursa zinazowazunguka kubadilisha maisha yao kwa kuwa wathubutu na
wabunifu ili waweze kufanikiwa kiuchumi .
“Vijana wanapaswa kujitoa
kufanya shughuli za kujitolea na uzalishaji Mali badala ya kusubiri
ajira wakati wanaweza kutengeneza fursa kwa kuamua kujitolea
kwanza” Alisema Neema
Kwa upande wake Mmoja wa
washiriki wa maonyesho hayo Neema Saidi alisema kuwa kupitia maonyesho
hayo yamekua fursa ya kupata wateja na kujifunza kupitia wafanyabiashara
wengine juu ya ubunifu na uboreshaji wa bidhaa.
No comments :
Post a Comment