Wahandisi kutoka Kanda ya
Magharibi na Ziwa wakiapishwa na Rais wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania
(IET) Mhandisi Menye Maanga wakati wa semina ya siku moja ya utendaji
kitaalamu katika fani ya uhandisi kwa Wahandisi ilifanyika leo mkoani
Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri akitoa leseni ya kazi kwa Mhandisi kutoka RUWASA Mpanda
Maglalena Mkelemi wakati wa semina ya siku moja ya utendaji kitaalamu
katika fani ya uhandisi kwa Wahandisi wa Kanda ya Magharibi na Ziwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi
Mhandisi Profesa Ninatubu Lema akitoa hotuba wakati akifungua semina ya
siku moja ya utendaji kitaalamu katika fani ya uhandisi kwa Wahandisi wa
Kanda ya Magharibi na Ziwa.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri akifungua leo semina ya siku moja ya utendaji kitaalamu katika
fani ya uhandisi kwa Wahandisi wa Kanda ya Magharibi na Ziwa.
Baadhi ya Wahandisi kutoka Kanda
ya Magharibi na Ziwa wakiwa katika semina ya siku moja ya utendaji
kitaalamu katika fani ya uhandisi kwa Wahandisi ilifanyika leo mkoani
Tabora.
********************************
NA, TIGANYA VINCENT, TABORA.
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetoa
miezi miwili kwa Wahandisi kuhakikisha wamesajiliwa na kupata leseni za
uhandisi zinazotolewa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini (ERB) ili
wanapokuwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali waweze kutambulika.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa
Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifungua semina ya siku moja ya
utendaji kitaalamu katika fani ya uhandisi kwa Wahandisi wa Kanda ya
Magharibi na Ziwa.
Alisema kuwa baada ya kipindi hicho kupita hataki kuona Mhandisi asiye na leseni ya ERB ndani ya Mkoa wa Tabora anafanyakazi.
Mwanri alisema utaratibu wa utoaji
wa leseni ni muhimu katika kuhakikisha Wahandisi wanaosimamia miradi
wanatambulika na wako tayari katika kuhakikisha usalama wa mazingira na
maisha ya wananchi.
Alitoa wito Wahandisi wote ambao
hawasijali kuhakikisha watumia nafisi hii ambapo Bodi yao inaendelea
kuhuisha leseni ambazo muda wake umekwisha ili ziwe hai na waweze
kutekeleza majukumu yao kwa uwazi.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa
aliongeza kuwa waandisi wasipozingatia taaluma zao ni hatari sana kwani
majengo yataanguka, madaraja yatabomoka, miundombinu mbalimbali itakuwa
hafifu isiyo na ubora hivyo kuleta maafa na hasara kubwa kwa uchumi wa
taifa.
Alisema serikali inaendelea
kutekeleza miradi mbali mbali ya kimkakati na wasimamizi wa utekelezaji
wake ni waandisi hivyo wanapaswa kuzingatia miiko na maadili ya taaluma
za utendaji kazi zao.
Mapema Msajili wa Bodi ya Usajili
wa Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi alisema hadi kufikia sasa kuna
jumla ya Wahandisi 3,373 waliopisha na kuna 26,918 ambao wamesajiliwa
kufanyakazi nchini.
Alisema kati ya hao 2,700 sawa na
asilimia 11 ni wa kike ambapo lengo la Bodi ni kufikia asilimia 50 kwa
50 ndani ya muda mfupi ujao.
Mhandisi Barozi aliongeza
Wahandisi wa kike wamekuwa waamiifu wakati wa utekelezaji wa miradi
mbalimbali wanayopewa kusimamia na ndio maana Bodi inataka kuongeza
idadi yao hapa nchini.
Katika semina hiyo jumla ya Wahandisi 16 wameapishwa na kupatiwa leseni za Bodi.
No comments :
Post a Comment