Thursday, February 13, 2020

Wabunge wafurahishwa na ufanisi wa kazi Ofisi ya Msajili wa Hazina

Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka akiongoza timu ya
Menejimenti ya Ofisi ya Msajili wa Hazina kuwapokea Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika Ofisi za Msajili wa Hazina, walipotembelea kuona utendaji kazi wa Ofisi hiyo Mirambo jijini Dar es Salaam, leo Februari 13, 2020.
Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti walipotembelea kuona utendaji kazi wa Ofisi hiyo Mirambo jijini Dar es Salaam, leo Februari 13, 2020.
Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka akitoa ufafanuzi wa
baadhi ya hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati wa Ziara ya Kibunge ya kutembelea na kupata taarifa  ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, leo Februari 13,2020 Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Jimbo la Muheza , Adadi Rajabu akifafanua jambo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Menejimenti ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti, kilichofanyika leo Februari 13,2020 jijini
Dar es Salaam.
Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Menejimenti ya Ofisi ya Msajili wa Hazina pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, walipotembelea kuona utendaji kazi wa Ofisi hiyo Mirambo jijini Dar es Salaam, leo
Februari 13, 2020.
(Picha na Ofisi ya TR)
**************************
Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wameelezea kufurahishwa na ufanisi wa
utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, baada ya kutembelea na kukutana na  Menejimenti ya ofisi
hiyo yenye jukumu la kusimamia Taasisi, Mashirika ya Umma na Kampuni ambazo Serikali inamiliki hisa.
Katika mkutano kazi huo, Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka alitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi yake inayosimamia Mashirika na Taasisi 266.

No comments :

Post a Comment