Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mzee Maarufu jijini Dodoma, Mohammed Makbel baada ya
kuzindua Mpango Kabambe wa jiji la Dodoma kwenye ukumbi wa Hazina jijini
Dodoma, Februari 13, 2020. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista
Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akionyesha Mpango Kabambe wa Jiji la Dodoma baada ya kuuzindua kwenye
ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Februari 13, 2020. Wengine pichani
kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi,
Angelina Mabula, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Spika wa Bunge
Job Ndugai na kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tixon Nzunda
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza wakati alipozindua Mpango Kabambe wa jiji la Dodoma kwenye
ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Februari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikata utepe wakati alipozindua Mpango Kabambe wa jiji la Dodoma kwenye
ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Februari 13, 2020. Kulia ni Spika wa
Bunge, Job Ndugai na kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimkabidhi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama Mpango Kabambe wa jiji
la Dodoma baada ya kuuzindua kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma,
Februari 13, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
***********************************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ameiagiza Ofisi ya Rais–TAMISEMI ishirikiane na mamlaka nyingine,
zihakikishe zinakamilisha mchakato wa muundo wa Halmashauri ya Jiji la
Dodoma.
Pia, Waziri Mkuu ameitaka
Halmashauri ya Jiji la Dodoma iongeze kasi ya upimaji wa
viwanja pamoja
na kusimamia kikamilifu udhibiti wa uendelezaji holela wa makazi.
“Hatuhitaji kuona Jiji la Dodoma likiwa na makazi yasiyopimwa na
holela.”
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo
leo (Alhamisi, Februari 13, 2020) wakati akizindua mpango kabambe wa
jiji la Dodoma katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema Serikali
haitaki kuona jiji la Dodoma likiwa na makazi yasiyopimwa na holela
kwani kasi ndogo ya upimaji wa viwanja kwa halmashauri ya jiji ndiyo
itakayosababisha wananchi kujenga makazi holela yasiyopimwa.
Amesema wananchi hawawezi
kuisubiri halmashauri bali halmashauri ndiyo inapaswa kuendana na kasi
ya mahitaji ya wananchi. “Tayari katika baadhi ya maeneo wananchi
wameanza na wanaendelea kujenga bila kufuata taratibu zinazotawala
masuala ya ujenzi mijini.”
Waziri Mkuu ameongeza kuwa upimaji
wa maeneo uende sambamba na uendelezaji wa miundombinu na huduma muhimu
katika maeneo, ikiwemo maji na barabara. “Kasi ya uboreshaji barabara
za mitaa iongezwe.”
Pia, Waziri Mkuu amesema
halmashauri ya Jiji la Dodoma iweke utaratibu mzuri wa ufuatiliaji,
utekelezaji na tathmini ya Mpango Kabambe ili kuhakikisha mpango huo
unatekelezwa kikamilifu.
“Hili ni takwa la kisheria kwa
mujibu wa kifungu namba 14(3) cha Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007
ambacho kinaitaka kila mamlaka ya upangaji kutoa taarifa ya utekelezaji
wa Mpango Kabambe kila mwaka katika maeneo yao ya upangaji kwa
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu ameiagiza
halmashauri ya Jiji la Dodoma ianzishe mchakato wa kutambua nyumba zote
zilizojengwa kwenye barabara kwa lengo la kujua idadi kamili, uhalali
wao kuwepo au kama ni wavamizi na baadaye kuandaa utaratibu wa fidia kwa
wananchi wanaostahili.
Kadharika, Waziri Mkuu ametoa wito
kwa viongozi wa Mkoa wa Dodoma, Wizara, Halmashauri, Taasisi, sekta
binafsi, Jumuiya za Kimataifa, wananchi na wadau wengine kuendelea kutoa
ushirikiano katika utekelezaji wa Mpango Kabambe ili kufikia malengo ya
kuwa na jiji bora, lenye mandhari ya kuvutia na litakalokidhi mahitaji
ya kijamii na kiuchumi ya sasa na ya baadae.
Uamuzi wa kuhamishia shughuli za
Serikali Dodoma ulifanyika mwaka 1973 ikiwa ni maelekezo ya Chama cha
TANU kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa utawala
wa awamu ya kwanza chini ya Uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere.
No comments :
Post a Comment