Tuesday, February 4, 2020

TTB YAPANIA SOKO LA UTALII UINGEREZA, YAMKABIDHI RASMI UBALOZI WA UTALII NICK REYNALD “BONGOZOZO”



Meneja Masoko kutoka Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Meena akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), katika hafla fupi ya kupewa Ubalozi wa Utalii wa Tanzania nchini Uingereza kwa bwana Nick Reynald ‘Bongozozo’ iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, leo Februari 04, 2020, kulia ni Afisa Uhisiano Mkuu TTB, Geofrey Tengeneza na kushoto ni Balozi wa hiari wa Utalii wa Tanzania nchini Uingereza, Bw. Nick Reynald ‘Bongozozo’
Balozi wa hiari wa Utalii wa Tanzania nchini Uingereza, Bw. Nick Reynald ‘Bongozozo’ akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), katika hafla fupi ya kupewa Ubalozi wa Utalii wa Tanzania nchini Uingereza iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, leo Februari 04, 2020, kulia ni Afisa Uhisiano Mkuu TTB, Geofrey Tengeneza na kushoto ni Meneja Masoko kutoka Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Meena
Meneja Masoko kutoka Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Meena(kushoto) akimkabidhi jarida la utalii (Tanzania Unforgetable) Bw. Nick Reynald ‘Bongozozo’(katikati) aliyekabishiwa barua rasmi kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania nchini Uingereza, kulia ni Afisa Uhisiano Mkuu TTB, Geofrey Tengeneza
Meneja Masoko kutoka Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Meena(kushoto) akimkabidhi barua ya utambuzi balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania Bw.Nick Reynald ‘Bongozozo’(katikati) aliyekabishiwa barua hiyo katika Ofisi za TTB Dar es Salaam, leo Februari 04,2020, kulia ni Afisa Uhisiano Mkuu TTB, Geofrey Tengeneza. Picha na Idara ya Habari-MAELEZO
******************************
Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii nchini (TTB), leo imetekeleza agizo la
Waziri wa Wizara hiyo, Dkt.Hamisi Kingwala alilolitoa Jijini Dodoma jana
Februari 03,2020 la kumpa Mwingireza Nick Reynald maarufu kama Bongozozo ubalozi wa utalii wa Tanzania nchini Uingireza.

Akizungumza katika hafla ya kumkabidhi barua ya utambuzi kwa ajili ya kazi hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa TTB, Geofrey Meena alisema
kuwa, Nick Reynald aliyezaliwa Zimbabwe na kuishi Tanzania kwa miaka 18 yaani tangia mwaka 1998 atakuwa balozi mzuri kwa uitalii wa Tanzania kwa sababu
maeneo mengi ya utalii anayajua.

“Nick Reynald ‘Bongozozo’ ameishi hapa nchini kwa miaka mingi kuanzia mwaka 1998 mpaka sasa ni miaka 18 kwa hiyo anauelewa na utalii wa Tanzania, amekuwa
maarufu sana hapa nchini kutokana na mapenzi makubwa kwa Tanzania ambayo yemejidhihirisha katika nyanja nyingi ikiwemo ushabiki wa mpira kwa timu ya Taifa
‘Taifa Stars” pamoja na wachezaji akiwemo Mbwana Samatta anayekipiga kunako klabu ya mpira ya Astoni villa nchini Uingireza”, Alisema Geofrey Meena.

Meena alisema kuwa Bongozozo alivutiwa sana na soka la Tanzania kwa kuwa kuna fujo isiyoumiza na amekuwa akisafiri na Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ katika michuano mbalimbali ikiwemo ile ya AFCON ambayo kwa mwaka 2019 ilifanyika nchini Misri.

TTB imedhamiria kukuza utalii kwa kuongeza watalii kutoka Uingereza kwa kuwa nchi hiyo ni ya pili kwa kuleta watalii wengi nchini ikitanguliwa na Marekani, kwa
takwimu za utalii mwaka 2018, watalii kutoka Uingereza walikuwa 77,199 huku Marekani ikileta watalii 94,876.

“Bodi inayofuraha leo kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya Utalii nchini, kumkabidhi rasmi Nick Reynald ‘Bongozozo’ barua ya uteuzi wa kuwa balozi wa
Hiari wa utalii wa Tanzania nchini Uingereza kama kituo bora cha utalii Afrika na duniani kote”, Alisema Geofrey Meena.

Kwa upande wake Nick Reynald ‘Bongozozo ambaye kwa sasa ni Balozi wa utalii wa Tanzania nchini Uingereza alisema kuwa yeye atakuwa balozi mzuri katika
kutangaza mazuri ya Tanzania na utalii wake duniani kote kupitia mitandao yake ya kijamii ili kuleta watalii nchini.

“Nikizunguka duniani kote kupitia mitandao yangu ya kijamii nitawaambia kuwa Tanzania ni nchi yenye watu wakarimu sana, nitazidi kuipeperusha bendera ya
Tanzania na nitawaeleza sehemu za kitalii zilizoko Tanzania, kwahiyo nimekubali kuitangaza Tanzania kwa watalii wengi duniani”, Alisema Nick Reynald ‘Bongozozo.

No comments :

Post a Comment