Afisa Mtendaji wa kata ya Iyunga,Abdul Kasukari (kushoto),akiongea na ujumbe wa wafanyakazi wa TBL Wakati wa hafla ya kukabidhi masada wa saruji


Afisa Mtendaji wa kata ya Iyunga,Abdul Kasukari (Kulia) akipokea msaada wa zsaruji kutoka kwa wafanyakazi wa TBL Wakati wa hafla hiyo
******************************
Katika mwendelezo wa mkakati
wake wa kusaidia huduma za kijamii,kampuni ya Tanzania Breweries Limited
(TBL) imetoa msaada wa mifuko 100 ya saruji kufanikisha ujenzi wa
kituo
cha afya cha Iyunga kilichopo mkoani Mbeya.
Msaada huo ulikabidhiwa na Meneja
wa kiwanda cha TBL cha Mbeya,Bw. Godwin Fabian, katika ofisi ya
Mkurugenzi wa jiji la Mbeya ambayo inasimamia ujenzi wa kituo hicho.
Akiongea wakati wa kukabidhi
msaada huo,Godwin Fabian, alisema, kampuni ya TBL, itaendelea kuunga
mkono jitihada za serikali za kuboresha huduma katika nyanja mbalimbali
hususani za sekta ya elimu,afya,na huduma za maji safi na salama.
“Kupitia sera ya kampuni ya
kuifanya “dunia kuwa maridhawa”kampuni imekuwa mstari wa mbele
kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali jamii katika jamii kwenye
maeneo tunayofanyia biashara zetu”alisema Fabian.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa
kata ya Iyunga,Abdul Kasukari, ambaye alipokea msaada huo kwa niaba ya
Mkurugenzi wa jijini alishukuru kampuni ya TBL, kwa msaada huo wa
kusaidia kufanikisha kituo cha afya cha Iyunga.
“Tunatoa shukrani kwa kampuni
yak TBL kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikitoa katika kusaidia
jamii, hii inadhihirisha uwekezaji wenu hapa mkoani Mbeya sio wa
kibishara tu bali kunufaisha wananchi wanaoishi mkoani hapa.”alisema
Kasukari.
No comments :
Post a Comment