Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati mkutano
na waasisi wa Umoja wa Jumuiya za Wanawake katika nchi huru za Afika
(PAWO) tawi la Tanzania walipokutana na Wizara uliolenga kutoa maoni yao
katika uboreshaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia
uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisalimiana na Prof.
Marjone Mbilinyi wakati wa mkutano na waasisi wa Umoja wa Jumuiya za
Wanawake katika nchi huru za Afika (PAWO) tawi la Tanzania walipokutana
na Wizara uliolenga kutoa maoni yao katika uboreshaji wa Sera ya
Maendeleo ya Wanawake na Jinsia uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa na mmoja wa Muasisi
wa PAWO Bibi.Tecla Sumbo mara baada ya kufungua mkutano wa waasisi wa
Umoja wa Jumuiya za Wanawake katika nchi huru za Afika (PAWO) tawi la
Tanzania na Wizara uliolenga kutoa maoni yao katika uboreshaji wa Sera
ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya waasisi wa Umoja wa Jumuiya za Wanawake katika nchi
huru za Afika (PAWO) tawi la Tanzania mara baada ya kufungua mkutano na
Wizara uliolenga kutoa maoni yao katika uboreshaji wa Sera ya Maendeleo
ya Wanawake na Jinsia uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimkabidhi kitenge cha
Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu Mtangazaji wa Zamani wa Redio
Tanzania Bibi. Deborah Mwenda baada ya kufungua mkutano wa waasisi wa
Umoja wa Jumuiya za Wanawake katika nchi huru za Afika (PAWO) tawi la
Tanzania na Wizara uliolenga kutoa maoni yao katika uboreshaji wa Sera
ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya waasisi wa Umoja wa Jumuiya za Wanawake
katika nchi huru za Afika (PAWO) tawi la Tanzania wakiwa na vitenge vya
Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu mara baada ya kufungua mkutano
wao na Wizara uliolenga kutoa maoni yao katika uboreshaji wa Sera ya
Maendeleo ya Wanawake na Jinsia uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.
Picha Zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
*******************************
Na Mwandishi Wetu Dar Es Salaam
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka
watendaji wa Wizara yake upande wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii
kuizingatia tarehe 31 mwezi Julai kila mwaka na kuhakikisha Tanzania
inaadhimisha Siku za Wanawake wa Afrika.
Waziri Ummy
ameyasema hayo leo Jijini Dar Es Salaam wakati wa mkutano na waasisi wa
Umoja wa Jumuiya za Wanawake katika nchi huru za Afika (PAWO) tawi la
Tanzania walipokutana na Wizara katika kutoa maoni yao katika uboreshaji
wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia.
Waziri amesema
kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyo mstari wa mbele katika
kukuza usawa wa kijinsia na kuwezeha wanawake katika Nyanja mbalimbali
hivyo ni muhmu kwa taifa kuadhimisha Siku ya Wanawake wa Afrika ili
kuongeza nguvu katika jitihada hizo za Serikali.
“Kwa kuzingatia
haya ndio maana kama Serikali tumetoa kipaumbele katika masuala ya
kukuza usawa wa kijinsia na kuiweka kuwa ni miongoni mwa ajenda muhimu
za maendeleo za kitaifa na utekelezaji wake utagusa Nyanja mbalimbali”
Alisema.
Ameongeza kuwa
pia msukumo mkubwa umewekwa na Serikali katika suala la kuhusisha
masuala ya kijinsia katika Sera, Mikakati, na Programu za kisekta na
kitaifa, uwezeshaji wanawake na kuzuia na kutokomeza ukatili wa
kijinsia.
“Serikali imekuwa
mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa wanawake wanapata fursa ya
kushiriki kwenye ngazi mbalimbali za maamuzi na uongozi katika nyanja za
kiuchumi, kijamii an kisiasa” alisema.
Waziri
amesisitiza kuwa jitihada zote hizo zisingeweza kutekelezwa kama
kusingekuwa na Umoja wa Jumuiya za Wanawake katika nchi huru za Afrika
(PAWO) kwani wananchama wake wamekuwa wakijitolea kuongoza jitihada hizi
kwa umoja na mshikamano ili kuleta uhuru, amani, haki na utengamano kwa
watu wa Afrika hasa wanawake.
“Hii yote
imewezesha nchi za Umoja wa Afrika ikiwemo Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake ambayo leo hii
tunaona matunda yake” alisema
Akizungumza kwa
niaba ya Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bi. Grace Mwangwa
amesema kuwa ushiriki wa waasisi hao katika mkutano huo utasaidia katika
kupata uzoefu katika nyanja walizokuwa wakizifanyia kazi katika kuleta
amani, utulivu, na kuleta usawa wa kijinsia na ustawi na maendeleo ya
wanawake na wasichana nchini.
Naye Mwenyekiti
wa Umoja wa Jumuiya za Wanawake katika nchi huru za Afrika (PAWO) Bibi.
Leah Lupembe ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuadhimisha Siku
ya Wanawake wa Afrika kila Julai 31 kwani itasaidia jamii ya watanzania
kuelewa kuhusu mapambano na mchango wa wanawake wa Afika katika uhuru na
kuwezesha wanawake kupata fursa sawa katika nyanja mbalimbali.
No comments :
Post a Comment